Waziri Mwigulu: Tunatazamia kuwakopesha Wafanyakazi wenye sifa Magari ili kupunguza Matumizi ya Serikali

Waziri Mwigulu: Tunatazamia kuwakopesha Wafanyakazi wenye sifa Magari ili kupunguza Matumizi ya Serikali

Swali la nyongeza kwa mh waziri
Natoa pongezi kwa wakurugenzi na wakuu wa idara kukopeshwa magari.

Je ? Ni lini serikali itafikiria kuwakopesha watendaji wa vijiji angalau baiskeli ili kuwaeezesha kuzungukia vijiji na kupeleka taarifa ofisi ya kata?
 
Napendekeza waanzie juu kabisa. Ile misafara waweke mafuta wenyewe. Yakiharibika wakomae wenyewe kurekebisha.
 
Salaam, Shalom!

Waziri wa Fedha ndugu Mwigulu nchemba amesema, Serikali imepanga kuwakopesha watumishi wa Serikali wenye sifa Ili kupunguza Mzigo Kwa Serikali.

Hatua hiyo ya kuwakopesha watumishi wenye sifa magari Ili wahusike wao kuyafanyia service, Kwa jicho la udadisi unalenga kuondokana na Ununuzi wa ma V8 Kwa DC,Wakurugenzi, RC na viongozi wengi sababu kuu ni kwamba, mishahara Yao haitotosha kuyamaintain.

DC Kwa Mfano, mwenye mshahara chini ya 3m Kwa mwezi, kamwe hatokubali kukopa v8 la 600 ml. Gari Rahisi Kwa DC kukopa na kulipa ni Clugger au Toyota Mkonga.

Ni hatua njema kufanya maamuzi hayo ingawa ni Kwa kuchelewa. Mzigo wa madeni ni mkubwa hivyo Serikali italazimika kujifunga mkanda zaidi.

Hatua hizo ziende mbali Kwa kupunguza au kupiga MARUFUKU safari za nje Kwa watumishi wa Serikali.

Hongereni Kwa kuwaza positive sababu MKULIMA, machinga au Mwananchi maskini mwenye kutegemea uwezesho wa TASAF asingeweza kumnunulia DC au RC gari la kifahari aina ya V8 ya zaidi ya 600 ml.

Karibuni 🙏.
 
Ok......Sasa mtu akopeshwe gari, service apeleke mwenyewe, mafuta ajaze mwenyewe halafu akubali liendeshwe na mtu mwingine? Ambaye huenda ana uendeshaji mbaya itakayompelekea bosi kwenda gereji kila mara kwa pesa zake? Difficult.
Mshahara wa DC ,RC, Wakurugenzi, utaendelea kulipwa na Serikali.

Aina ya magari ndo itabadilika.

Land cruiser mkonga mbona ni gari poa tu.
 
Maneno matamu lakini utekelezaji ni zero, hata Pinda alisema V8 zisinunuliwe lakini matokeo yake ndiyo zikazidi, kwenye nchi yetu watu wanaotakiwa kutumia magari ya umma. 1. Rais, 2.PM, 3.Spika na 4.Jaji Mkuu, wengine wote wanatakiwa kutumia public transport.
 
Yaani ukopeshe mtu gari ya 600mil 😃
Kwani lazima atumie la 600ml? Kila mtu atakopa gari kadiri ya uwezo wake. Nchi nyingi wanafanya hivyo. Mambo ya kuwa na magari mengi ya serikali ni kizamani sana. Hatua hii kama itatekelezwa itaenda kuokoa mabilioni mengi ya serikali. V8 kwa sasa hazihitajiki kutokana na maboresho makubwa ya mtandao wa barabara nchi. Let us be fair to the tax papers.
 
DED mwenye kupokea 3m aweza vp kubali kukopshwa V8 ya 600ml.

Habari ya V8 ndo imeishia hapo,

Land cruiser mkonga inarudi mzigoni.

Na Bado, tunakoelekea hatujafika.
Kila level Ina category ya magari.V8 Kwa DED inafanya nini?

Posho wanazopata kwenye safari Zinazidi salary zao hizo
 
Back
Top Bottom