Salaam, Shalom!
Waziri wa Fedha ndugu Mwigulu nchemba amesema, Serikali imepanga kuwakopesha watumishi wa Serikali wenye sifa Ili kupunguza Mzigo Kwa Serikali.
Hatua hiyo ya kuwakopesha watumishi wenye sifa magari Ili wahusike wao kuyafanyia service, Kwa jicho la udadisi unalenga kuondokana na Ununuzi wa ma V8 Kwa DC,Wakurugenzi, RC na viongozi wengi sababu kuu ni kwamba, mishahara Yao haitotosha kuyamaintain.
DC Kwa Mfano, mwenye mshahara chini ya 3m Kwa mwezi, kamwe hatokubali kukopa v8 la 600 ml. Gari Rahisi Kwa DC kukopa na kulipa ni Clugger au Toyota Mkonga.
Ni hatua njema kufanya maamuzi hayo ingawa ni Kwa kuchelewa. Mzigo wa madeni ni mkubwa hivyo Serikali italazimika kujifunga mkanda zaidi.
Hatua hizo ziende mbali Kwa kupunguza au kupiga MARUFUKU safari za nje Kwa watumishi wa Serikali.
Hongereni Kwa kuwaza positive sababu MKULIMA, machinga au Mwananchi maskini mwenye kutegemea uwezesho wa TASAF asingeweza kumnunulia DC au RC gari la kifahari aina ya V8 ya zaidi ya 600 ml.
Karibuni 🙏.