Waziri Mwigulu: Tunatazamia kuwakopesha Wafanyakazi wenye sifa Magari ili kupunguza Matumizi ya Serikali

Waziri Mwigulu: Tunatazamia kuwakopesha Wafanyakazi wenye sifa Magari ili kupunguza Matumizi ya Serikali

Swali la nyongeza kwa mh waziri
Natoa pongezi kwa wakurugenzi na wakuu wa idara kukopeshwa magari.

Je ? Ni lini serikali itafikiria kuwakopesha watendaji wa vijiji angalau baiskeli ili kuwaeezesha kuzungukia vijiji na kupeleka taarifa ofisi ya kata?
Hizo taarifa zao zinatusaidia nini, wakae nazo tu, wambie watumie whatsapp au email, simple tu.
 
Awamu ya sita ikimaliza utawala wake nchi itakuwa imefilisika na hakutakuwa na maisha daraja ya kati ila ni matajiri saana maana ya wafanyakazibiashara na mafukara wa kutupwa!
Sema CCM inaliangamiza taifa, wakati siku zote tunapiga kelele ccm ni janga la taifa mlituona si wazalendo haya leo kipo wapi?? Nabado Kipara wewee
 
Hapo kwenye public transport Bado Kuna hatua kadhaa Ili kupafikia.

Mkwamo wa kiuchumi unakuja ndo unawalazimisha kuchukua hatua hizo.

Tukiondokana na V8 Kwa DC,RC, KATIBU WAKUU NA WASAIDIZI MAWIZARANI, wakakopeshwa Toyota land cruiser mkonga, mbona itapunguza Mzigo Kwa wananchi!!
Kwanza huwa wanafanya nini hao DC na DAS, mwenye kujua kazi zao atujulishe.
 
Hivi hii nchi bado kama vile watu mnakuwa na ugeni na Hawa viongozi wetu. Hayo maneno ya waziri ni kauli tu lkn hamna litakalotekelezwa na haitowezekana
 
“Mtazamo wa Serikali ni kuendelea kupunguza masuala ya matumizi ya magari [...] Badala ya serikali kuwa inamiliki haya magari, tunataka watumishi wanaopata sifa ya kuwa na magari wakopeshwe yawe ya kwao ili kuipunguzia serikali mzigo wa kuyaendesha magari, kuyapatia ‘service’ pamoja na vitu vingine vinavyotakiwa.” – Dkt. Mwigulu Nchemba.
20231108_141858.jpg
watumi
Gari la mil 150 ,unakopeshwa Kwa mil 7.
Tanzania Nchi ya Mito ya asali, maziwa
 
DED mwenye kupokea 3m aweza vp kubali kukopshwa V8 ya 600ml.

Habari ya V8 ndo imeishia hapo,

Land cruiser mkonga inarudi mzigoni.

Na Bado, tunakoelekea hatujafika.

Serikali gari haiuzwi kwa bei ya kununulia.
Inashuka vibaya mno na inaweza kununuliwa kwa bei ya nyanya
 
Ukisoma btn the lines,

V8 zitabaki Kwa Rais na Pm bas, wengine watarudi kwenye Land cruiser mkonga.

Na kinachosikitisha, wanachukua hatua hizo Leo, Si kwamba wanasikiza wananchi no, ni kwamba madeni yamewaelemea.

Hardtop ndio gari ya kazi. it was designed kwenda kokote wkt wowote with minimal maintenance.
Na hii ndio inawafaa wakurugenzi
 
Serikali iliwahi kusema inatumia Bil.550 Kwa mwaka Kuagiza magari, vipuri, mafuta na matengenezo Kila mwaka.

--
Akijibu swali la Mbunge Asia Abdulkarim Halamga aliyehoji sababu za Serikali kutumia Wakala wa Huduma za Ununuzi Serikalini (GPSA) ambaye ananunua Magari kwa gharama kubwa kuliko bei ya Soko la Dunia, Waziri wa Fedha, Dkt, Mwigulu Nchemba amesema Serikali inatazamia kuanza kuwakopesha Watumishi wenye sifa ili kuondoa mzigo wa Mafuta na Matengenezo Serikalini.

Kuhusu utaratibu wa kuagiza Magari moja kwa moja Viwandani badala ya kutumia Mawakala, Dkt. Mwigulu amesema "Kuna baadhi ya mazingira yanaruhusu Serikali kununua kwa mawakala, pia, baadhi ya Viwanda havipendi wanunuzi waende moja kwa moja Viwandani".

Kwa mujibu wa taarifa iliyowasilishwa na Wizara ya Fedha Bungeni mwaka 2022, Serikali ilikuwa na Magari 15,742, Pikipiki 14,047 na Mitambo 373 huku ikitumia zaidi ya Tsh. Bilioni 500 kila mwaka kwaajili ya Ununuzi wa Magari mapya, Mafuta, Vipuri na Matengenezo.



My Take
Naona Kuna kigugumizi Cha kuchukua maamuzi.

Toka mwaka juzi mnaongelea hili jambo na hamfiki Muafaka.

Semeni kama Serikali kwamba deadline itakuwa lini? Na Je Madereva mtaajiri wa Umma au Kila boss na dereva wake?
BOT mbona wanafanya na mambo yako poa
 
DED mwenye kupokea 3m aweza vp kubali kukopshwa V8 ya 600ml.

Habari ya V8 ndo imeishia hapo,

Land cruiser mkonga inarudi mzigoni.

Na Bado, tunakoelekea hatujafika.
Hiyo gari mkonga ni nzuri sana!

Ukisikilizia injini yake iluunguruma kama simba.
 
SWALI: Sababu za Serikali kutumia Wakala wa Huduma za Ununuzi Serikalini (GPSA) ambaye ananunua Magari kwa gharama kubwa kuliko bei ya Soko la Dunia.

JIBU: Serikali inatazamia kuanza kuwakopesha Watumishi wenye sifa ili kuondoa mzigo wa Mafuta na Matengenezo Serikalini.

😁​
 
Back
Top Bottom