Precious Diamond
JF-Expert Member
- Jun 9, 2023
- 593
- 1,376
Tarehe 30 Machi 2024, Waziri Mwigulu akiwa katika Mashindano ya 7 ya kuhifadhi Qur'aan Tukufu yaliyoandaliwa na Mbunge wa Jimbo la Kondoa, Waziri wa Viwanda na Biashara Ashatu Kijaji katika Viwanja vya Shule ya Msingi Lembo-Masawi, amerusha kijembe kwa wanaosema Rais Samia amekopa sana ndani toka aingie madarakni kuliko awamu zote za nyuma kwa pamoja. Amesema;
"Hivi majuzi nilimsikia ndugu yangu mmoja akiwa Babati, akisema Rais wa Awamu ya 6 ana miaka mitatu na ameshakopa trilioni 30 wakati waliotangulia walikaa miaka 60 na kukopa trilion 60 lakini akasahau kuwafafanulia watu kwamba kwenye hizi trilioni 30 trilioni tatu amegeuza deni la thamani la wazee akatoa fedha kwa njia ya hati fungani ili walipwe wazee, ambao walikopwa zamani miaka ya 93, kwa huruma yake kwa wazee amebadilisha deni lile na kutoa fedha deni lile likaingia kwenye deni la taifa
"Lakini pia amebadilisha madeni ya zamani ya TANESCO, TIPA/TPDC takribani trilioni 3 ili zipate mtaji, madeni yao hayo yakaingizwa pia katika deni la taifa.
"Kutokana na Dunia inavyoenda kuna badiliko la bei ya kubadilisha fedha pamoja na riba kwenye madeni ya zamani, hili tu ni lina thamani ya trilioni 5 mpaka 6. Karibia Trilioni 12 ni za madeni ya zamani sio Rais Kakopa.
"Kwenye trilioni 30 zimebaki trililioni 18, lakini Rais kaachiwa bwawa ambalo lilikuwa limetekelezwa kwa 37%, kaachiwa reli haijavuka Morogoro, reli peke yake ni dola bilioni 10 lakini haijakamilika mpaka mwisho, ambayo imeshachukuliwa ni takribani dola bilioni 6 (takribani trilioni 12 nyingine.
"Sasa ukisema Mwl. Nyerere hakuwa amekopa sana, Hayati Mwinyi hakuwa amekopa sana, Hayati Mkapa hakuwa amekopa sana, pamoja na Awamu ya 4 na ya 5, sasa walikuwa wamejenga reli wapi? Ndio hii Rais Samia amejenga."