Waziri Mwigulu: Wanaosema Rais Samia amekopa sana kuliko Awamu zote za nyuma waeleze pia mikopo hiyo inatokana na madeni ya nyuma

Tarehe 30 Machi 2024, Waziri Mwigulu akiwa katika Mashindano ya 7 ya kuhifadhi Qur'aan Tukufu yaliyoandaliwa na Mbunge wa Jimbo la Kondoa, Waziri wa Viwanda na Biashara Ashatu Kijaji katika Viwanja vya Shule ya Msingi Lembo-Masawi, amerusha kijembe kwa wanaosema Rais Samia amekopa sana ndani toka aingie madarakni kuliko awamu zote za nyuma kwa pamoja. Amesema;

"Hivi majuzi nilimsikia ndugu yangu mmoja akiwa Babati, akisema Rais wa Awamu ya 6 ana miaka mitatu na ameshakopa trilioni 30 wakati waliotangulia walikaa miaka 60 na kukopa trilion 60 lakini akasahau kuwafafanulia watu kwamba kwenye hizi trilioni 30 trilioni tatu amegeuza deni la thamani la wazee akatoa fedha kwa njia ya hati fungani ili walipwe wazee, ambao walikopwa zamani miaka ya 93, kwa huruma yake kwa wazee amebadilisha deni lile na kutoa fedha deni lile likaingia kwenye deni la taifa

"Lakini pia amebadilisha madeni ya zamani ya TANESCO, TIPA/TPDC takribani trilioni 3 ili zipate mtaji, madeni yao hayo yakaingizwa pia katika deni la taifa.

"Kutokana na Dunia inavyoenda kuna badiliko la bei ya kubadilisha fedha pamoja na riba kwenye madeni ya zamani, hili tu ni lina thamani ya trilioni 5 mpaka 6. Karibia Trilioni 12 ni za madeni ya zamani sio Rais Kakopa.

"Kwenye trilioni 30 zimebaki trililioni 18, lakini Rais kaachiwa bwawa ambalo lilikuwa limetekelezwa kwa 37%, kaachiwa reli haijavuka Morogoro, reli peke yake ni dola bilioni 10 lakini haijakamilika mpaka mwisho, ambayo imeshachukuliwa ni takribani dola bilioni 6 (takribani trilioni 12 nyingine.

"Sasa ukisema Mwl. Nyerere hakuwa amekopa sana, Hayati Mwinyi hakuwa amekopa sana, Hayati Mkapa hakuwa amekopa sana, pamoja na Awamu ya 4 na ya 5, sasa walikuwa wamejenga reli wapi? Ndio hii Rais Samia amejenga."

Lakini nakumbuka yule mjinga mwenye tumbo kubwa toka Mtama alisema Magu ndo kakopa sana,leo story ni mpya tena
 
Baelezeee papaaa, tomboka malamu.

Pia wakumbuke, miradi kama SGR na Bwawa la Mwalimu haikuwa imepata mkopo wa mradi wote, ilikuwa inakopewa kidogo sana, kama robo tu, mfano reli ilikopewa mpaka sijui kibaha, mama kaifikisha Dodoma mpaka mwanza, sasa ulitaka mtu aliyejenga mara kumi ya JPM aonekane katumia fedha kidogo?

Bwawa la Mwalimu Nyerere, JPM aliacha watu bado wanafyeka majani, leo bwawa lipo, kazi ya nani hiyo? SSH
Ahahaha kwamba aliacha watu bado wanafyeka majani
 
Unashangilia ujenzi wa reli na bwawa la mwalimu nyerere bila kujua chanzo cha fedha? Nyie ndio mnaacha nyumbani hela ya dagaa, unakuta mkeo kapika kuku, unashangilia
Mbona JPM alisema miradi inatumia fedha za ndani?
 
Si ndio maana Chiembe anasema zilikuwa za Kufyeka majani! Itoshe kusema zilikuwa hazitoshi, na hiyo ina maana, Ule uzushi kwamba Hayat Rais Magufuli alitumia fedha nyingi pale, ni uwongo.

Ama ulitaka kusemaje?
 
Yaani huyu jamaa huwa hana mvuto hata wa kuhutubia. Anaongea kama mtu mwenye hang over ya konyagi.
 
Tarehe 30 Machi 2024, Waziri Mwigulu akiwa katika Mashindano ya 7 ya kuhifadhi Qur'aan Tukufu yaliyoandaliwa na Mbunge wa Jimbo la Kondoa, Waziri wa Viwanda na Biashara Ashatu Kijaji katika Viwanja vya Shule ya Msingi Lembo-Masawi, amerusha kijembe kwa wanaosema Rais Samia amekopa sana ndani toka aingie madarakni kuliko awamu zote za nyuma kwa pamoja. Amesema;

"Hivi majuzi nilimsikia ndugu yangu mmoja akiwa Babati, akisema Rais wa Awamu ya 6 ana miaka mitatu na ameshakopa trilioni 30 wakati waliotangulia walikaa miaka 60 na kukopa trilion 60 lakini akasahau kuwafafanulia watu kwamba kwenye hizi trilioni 30 trilioni tatu amegeuza deni la thamani la wazee akatoa fedha kwa njia ya hati fungani ili walipwe wazee, ambao walikopwa zamani miaka ya 93, kwa huruma yake kwa wazee amebadilisha deni lile na kutoa fedha deni lile likaingia kwenye deni la taifa

"Lakini pia amebadilisha madeni ya zamani ya TANESCO, TIPA/TPDC takribani trilioni 3 ili zipate mtaji, madeni yao hayo yakaingizwa pia katika deni la taifa.

"Kutokana na Dunia inavyoenda kuna badiliko la bei ya kubadilisha fedha pamoja na riba kwenye madeni ya zamani, hili tu ni lina thamani ya trilioni 5 mpaka 6. Karibia Trilioni 12 ni za madeni ya zamani sio Rais Kakopa.

"Kwenye trilioni 30 zimebaki trililioni 18, lakini Rais kaachiwa bwawa ambalo lilikuwa limetekelezwa kwa 37%, kaachiwa reli haijavuka Morogoro, reli peke yake ni dola bilioni 10 lakini haijakamilika mpaka mwisho, ambayo imeshachukuliwa ni takribani dola bilioni 6 (takribani trilioni 12 nyingine.

"Sasa ukisema Mwl. Nyerere hakuwa amekopa sana, Hayati Mwinyi hakuwa amekopa sana, Hayati Mkapa hakuwa amekopa sana, pamoja na Awamu ya 4 na ya 5, sasa walikuwa wamejenga reli wapi? Ndio hii Rais Samia amejenga."

Ni ujinga Waziri kuendelea kujadili swala la mikopo.

Kukopa Kuna shida gani? Kuna Nchi haikopi?

Kwanza nawashangaa,Tanzania tunatakiwa kukopa zaidi na zaidi Kwa sababu Hawa wote walio na Madeni makubwa hapa wametuzidi Uchumi

View: https://twitter.com/AfricaFactsZone/status/1774535241761173605?t=wX02YsFULP6DZGrCuXG4Xg&s=19

Kopeni zaidi na zaidi ila tuu mikopo ielekezwe kwenye miradi ya kufungua uchumi na siokupendezesha Miji au Huduma za jamii
 
U.S.A wenyewe mpaka leo wanaongoza kwa kudaiwa, plus China, Uingereza

Usijilinganishe nao utakuwa Unakosea .

Wale wanaouwezo wa kulipa kwa wakati.

Walishajiimarisha kiuchumi. Wale ni Ulimwengu wa kwanza sisi tuko wa tatu.

Ni mfano ulinganishe kukopa kwa Baresa tajiri zidi ya kukopa kwa maskini au mtumishi wa umma wa kawaida.

Tajiri ako na alternatives za vyanzo vingi vya cash flows za kuweza kufanya marejesho kwa wakati kuliko maskini.
 
Tarehe 30 Machi 2024, Waziri Mwigulu akiwa katika Mashindano ya 7 ya kuhifadhi Qur'aan Tukufu yaliyoandaliwa na Mbunge wa Jimbo la Kondoa, Waziri wa Viwanda na Biashara Ashatu Kijaji katika Viwanja vya Shule ya Msingi Lembo-Masawi, amerusha kijembe kwa wanaosema Rais Samia amekopa sana ndani toka aingie madarakni kuliko awamu zote za nyuma kwa pamoja. Amesema;

"Hivi majuzi nilimsikia ndugu yangu mmoja akiwa Babati, akisema Rais wa Awamu ya 6 ana miaka mitatu na ameshakopa trilioni 30 wakati waliotangulia walikaa miaka 60 na kukopa trilion 60 lakini akasahau kuwafafanulia watu kwamba kwenye hizi trilioni 30 trilioni tatu amegeuza deni la thamani la wazee akatoa fedha kwa njia ya hati fungani ili walipwe wazee, ambao walikopwa zamani miaka ya 93, kwa huruma yake kwa wazee amebadilisha deni lile na kutoa fedha deni lile likaingia kwenye deni la taifa

"Lakini pia amebadilisha madeni ya zamani ya TANESCO, TIPA/TPDC takribani trilioni 3 ili zipate mtaji, madeni yao hayo yakaingizwa pia katika deni la taifa.

"Kutokana na Dunia inavyoenda kuna badiliko la bei ya kubadilisha fedha pamoja na riba kwenye madeni ya zamani, hili tu ni lina thamani ya trilioni 5 mpaka 6. Karibia Trilioni 12 ni za madeni ya zamani sio Rais Kakopa.

"Kwenye trilioni 30 zimebaki trililioni 18, lakini Rais kaachiwa bwawa ambalo lilikuwa limetekelezwa kwa 37%, kaachiwa reli haijavuka Morogoro, reli peke yake ni dola bilioni 10 lakini haijakamilika mpaka mwisho, ambayo imeshachukuliwa ni takribani dola bilioni 6 (takribani trilioni 12 nyingine.

"Sasa ukisema Mwl. Nyerere hakuwa amekopa sana, Hayati Mwinyi hakuwa amekopa sana, Hayati Mkapa hakuwa amekopa sana, pamoja na Awamu ya 4 na ya 5, sasa walikuwa wamejenga reli wapi? Ndio hii Rais Samia amejenga."

Endelea upiga mwingi mama
 
Back
Top Bottom