Waziri Mwijage: Mimi ni 'propagandist' niliyesomea China. Aagiza tani 20,000 ya sukari bandarini itolewe

Waziri Mwijage: Mimi ni 'propagandist' niliyesomea China. Aagiza tani 20,000 ya sukari bandarini itolewe

Hivi punde

JF-Expert Member
Joined
Apr 1, 2017
Posts
2,554
Reaction score
8,587
Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Charles Mwijage amesema nchi ina sukari ya kutosha na kilichojitokeza ni propaganda ya watu wasioitakia mema.

Akihitimisha hoja ya bajeti ya wizara yake ya mwaka 2018/19 leo Mei 11, 2018 bungeni, Mwijage amesema tayari ameagiza Shirika la Viwango Tanzania (TBS) na Mamlaka ya Chakula la Dawa Tanzania (TFDA) kuiondoa sukari yote iliyopo bandarini.

Amesema yeye ni mcha Mungu na asingependa kuona Waislamu wanaotarajia kuingia katika mfungo wa Ramadhani wanapata shida ya kupata sukari.

Waziri Mwijage amesema hakuna tatizo la sukari kwani kuna akiba ya sukari tani 43,000 iliyopo katika stoo.

“Lakini Tanzania tunatumia tani 40,000 kwa mwezi,” amesema.
Amesema amewaagiza mameneja wa TBS na TFDA kuhakikisha tani 20,000 ya sukari iliyopo bandarini inaondolewa.

“Viwanda vya sukari vyote bado kama wiki tatu vinaanza kuzalisha. Suala la sukari lilikuwa ni propaganga na mimi ni ‘propagandist’ niliyesomea China,” amesema.

Kuhusu mazingira ya uwekezaji, Mwijage amesema amekuwa akipigania kuyafanya kuwa rafiki na kuwaomba wabunge wanapobaini kuwapo kwa changamoto zozote waziwasilishe kwake na hatua zitachukuliwa.

Pia, amesema amepokea maoni na ushauri wote uliotolewa na wabunge na kuahidi kuufanyia kazi.
 
Yaani una tani 43,000 wakati matumizi ya mwezi ni tani 40,000 Waziri anasema ana sukari ya kutosha? Kweli ? What ?

Jamani Mh. Rais fukuza huyu mtu he is very short sighted, ndio naona sasa. Yeye ndie anatakiwa aje na sera na mikakati mipya ya Tanzania ya viwanda, sasa anawataka wabunge wamletee mikakati..

Omg, huyu Mwijage mbona haendani na vision ya mh. Rais wetu kabisa
 
Ni mpiga zumari wa Faru John.
 
Mwijage hawezi kufukuzwa na mkuu jiwe kwani huyu ni kipz chake kama alivyowahi kusema mkuu kwamba yeye hapangiwi
 
Sijui JPM alimuokota wapi huyu Mwijage? Sijui walisoma wote na ni washkaji? Jamaa ni kama comedian flani hivi. Majibu yake mara nyingi hayana substance.
 
Hivi kuna kiwanda hata kimoja kimeanza kujengwa? Ukiacha kiitikio cha viwanda, viwanda
Walisema ukiwa na cherehani nne, machine tatu za kutengeneza juice, barber shop etc, ni "viwanda" hivyo. Nadhani tupo pazuri and in the right tarakii kwa "viwanda" sampuli hii
 
Back
Top Bottom