FATHER OF HISTORY
JF-Expert Member
- Aug 15, 2012
- 915
- 638
Kama yeye Ni propagandist ndiyo apige propaganda kwenye duals nyeti la sukari?
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Mwijage nampenda kufa, unajua unafiki mpaka kapitiliza. Anajua kula na kipofu. Mwijage komaa hapo uliposhika ng'ang'ania. Piga kaziWaziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Charles Mwijage amesema nchi ina sukari ya kutosha na kilichojitokeza ni propaganda ya watu wasioitakia mema.
Akihitimisha hoja ya bajeti ya wizara yake ya mwaka 2018/19 leo Mei 11, 2018 bungeni, Mwijage amesema tayari ameagiza Shirika la Viwango Tanzania (TBS) na Mamlaka ya Chakula la Dawa Tanzania (TFDA) kuiondoa sukari yote iliyopo bandarini.
Amesema yeye ni mcha Mungu na asingependa kuona Waislamu wanaotarajia kuingia katika mfungo wa Ramadhani wanapata shida ya kupata sukari.
Waziri Mwijage amesema hakuna tatizo la sukari kwani kuna akiba ya sukari tani 43,000 iliyopo katika stoo.
“Lakini Tanzania tunatumia tani 40,000 kwa mwezi,” amesema.
Amesema amewaagiza mameneja wa TBS na TFDA kuhakikisha tani 20,000 ya sukari iliyopo bandarini inaondolewa.
“Viwanda vya sukari vyote bado kama wiki tatu vinaanza kuzalisha. Suala la sukari lilikuwa ni propaganga na mimi ni ‘propagandist’ niliyesomea China,” amesema.
Kuhusu mazingira ya uwekezaji, Mwijage amesema amekuwa akipigania kuyafanya kuwa rafiki na kuwaomba wabunge wanapobaini kuwapo kwa changamoto zozote waziwasilishe kwake na hatua zitachukuliwa.
Pia, amesema amepokea maoni na ushauri wote uliotolewa na wabunge na kuahidi kuufanyia kazi.
Tupo kwenye "right track" viwanda 3500 vimejengwa[emoji14]Hivi kuna kiwanda hata kimoja kimeanza kujengwa? Ukiacha kiitikio cha viwanda, viwanda
Nilisikia hiyo kauli, vimejengwa mkoa gani, na vinazalisha nnTupo kwenye "right track" viwanda 3500 vimejengwa[emoji14]
Watanzania tutembee kifua mbeleTupo kwenye "right track" viwanda 3500 vimejengwa[emoji14]
Hata mimi sijui kwake. Ni muhuni muhuni kama alivyokuwaga Nazir Karamagi enzi zake. Karamagi alikuwa haeleweki eleweki lakini akapewa wizara nyeti ya nishati na madini enzi za JK! Matokeo yake aliacha watu midomo wazi kwenye mikataba ya kihunihuni ya Buzwagi!Hili jamaa sijui walilitoa wapi!
Yule ndugu ndio anawataka watu kama hawa wasioweza kufikiri ili kila kitu afanye yeye. Wanaofikiri na kumpa changamoto wanamsumbua.Ningekuwa na mamlaka,huyu ndio angekuwa waziri wa kwanza kumfukuza kazi.
Je viwanda vya hapa nchini vinazalisha kiasi gani kwa mwezi?Yaani una tani 43,000 wakati matumizi ya mwezi ni tani 40,000 Waziri anasema ana sukari ya kutosha? Kweli ? What ?
Waliosomea propaganda za kikomunisti si wa kuwaamini hawana ukweli.Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Charles Mwijage amesema nchi ina sukari ya kutosha na kilichojitokeza ni propaganda ya watu wasioitakia mema.