Waziri Mwijage: Mimi ni 'propagandist' niliyesomea China. Aagiza tani 20,000 ya sukari bandarini itolewe

ASHASEMA NI PROPAGANDIST.MAANA YA HILO NI KUZUBAISHA NA KUWAAMINISHA WATU KUNA MATEGEMEO FULANI YASIYOSHIKIKA.
 
Huyu kweli propagandist ndio maana anatuambia awamu hii imejenga viwanda 60,000 chakushangaza hajatupa takwimu za ajira hivyo viwanda vilizozalisha. Viwanda anajenga kipropagandist mpaka 2020 atakuwa ameshajenga viwanda 200,000 kipropagandist.
 
Mwijage nampenda kufa, unajua unafiki mpaka kapitiliza. Anajua kula na kipofu. Mwijage komaa hapo uliposhika ng'ang'ania. Piga kazi
 
Hawezi kufukuzwa kwa sababu hiyo anayoifanya ndo "kazi yake halisi"
 
Propagandist!?Sasa ndio nimeelewa vile viwanda vipya 3000+
 
Hili jamaa sijui walilitoa wapi!
Hata mimi sijui kwake. Ni muhuni muhuni kama alivyokuwaga Nazir Karamagi enzi zake. Karamagi alikuwa haeleweki eleweki lakini akapewa wizara nyeti ya nishati na madini enzi za JK! Matokeo yake aliacha watu midomo wazi kwenye mikataba ya kihunihuni ya Buzwagi!
 
Ndio maana kwa muda mfupi ameshaonesha kupwaya kwa hali ya juu ma upungufu wa halo ya juu ya weledi kiasi cha kufanya viinimacho bungeni. Ina maana Boss wake aliamini kabisa viwanda vinajengwa kwa propaganda. Huyu alifaa kuwa katibu mwenezi angefaa sana kwa aina ya siasa tulizonazo.
 
Ningekuwa na mamlaka,huyu ndio angekuwa waziri wa kwanza kumfukuza kazi.
Yule ndugu ndio anawataka watu kama hawa wasioweza kufikiri ili kila kitu afanye yeye. Wanaofikiri na kumpa changamoto wanamsumbua.
 
Yaani una tani 43,000 wakati matumizi ya mwezi ni tani 40,000 Waziri anasema ana sukari ya kutosha? Kweli ? What ?
Je viwanda vya hapa nchini vinazalisha kiasi gani kwa mwezi?
=====
Kwa Mwija: Kutumia propaganda kwenye mambo ya msingi kama mahitaji ya sukari nchi, ni hatari kwa mtakabali wa cheo chako!
 
Kati ya mawaziri hovyo kabisaaa anayejua kubwabwaja tu, huyu huenda kiti chake ni kwa faida ya wanaojua kwa nini anabaki tu pale!! !
 
Waliosomea propaganda za kikomunisti si wa kuwaamini hawana ukweli.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…