Waziri Nape atembelea Multichoice, awarudishia DSTV 'local channels' baada ya marekebisho ya kanuni

Waziri Nape atembelea Multichoice, awarudishia DSTV 'local channels' baada ya marekebisho ya kanuni

Replica

JF-Expert Member
Joined
Aug 28, 2017
Posts
1,681
Reaction score
8,887
Waziri wa habari, Nape Nnauye ametangaza kurejeshwa kwa 'Free local channels' kwenye king'amuzi cha DSTV alipofika ofisi za Multichoice Tanzania akiyataja kama maagizo ya Rais Samia kurekebisha kanuni na Sheria.

Agosti 12, 2018 DSTV ililazimika kuondoa chaneli za FTA baada ya mamlaka ya mawasiliano nchini kuipiga mkwara wa uwezekano wa kuifutia leseni endapo itaendelea kwani ilikuwa hairuhusiwi kulipia chaneli hizo zinazopaswa kuwa bure.

Uamuzi huu pia iliwadhuru wote waliokuwa wanaendesha ving'amuzi kwa mfumo wa 'DHT' ambao iliwajumuisha pia Azam na Zuku ambao wenyewe waliamua kufata masharti na baadae kuruhusiwa.

Waziri wa mawasiliano wa wakati huo, Dkt. Mwakyembe akitoa sababu za kuzuia, alisema leseni ya kampuni hizo tatu ilikuwa na maudhui ya kulipia(Pay TV) hata kwa chaneli za FTA na pesa ikiisha zinazimwa kama luku. Pia alisema miundombinu yao ya urushaji matangazo haiko nchini.

Mwakyembe alisema waandaji wa maudhui(TV Stations) wana uhuru wa kuchagua TV zao ziwe za umma au kulipia na wakichagua za umma mapato yao yanatokana na matangazo ya biashara pekee bila kumtoza mteja kitu ambacho alisema DSTV walikiuka.

Pia, soma=> Waziri Mwakyembe: Azam, Zuku na DSTV walirusha maudhui ya ndani kinyume na leseni zao! Lazima warejeshe fedha zote walizowatoza Wananchi

7693ff2607f94d9eaa0dd11e7c671b76-0001.jpg
7693ff2607f94d9eaa0dd11e7c671b76-0002.jpg
7693ff2607f94d9eaa0dd11e7c671b76-0003.jpg
 

Attachments

Nape Nnauye katangaza Leo....

Kwa wale waliokuwa wameweka Ving'amuzi vya DSTV kabatini Sasa Muda wa Kuvirejesha Tena mezani Ndio hu

#BREAKING: Waziri wa Habari Nape Nnauye leo ametangaza rasmi kurudishwa kwa TV channels za bure kwenye king’amuzi cha DSTV mfano CloudsTV, ITV n.k baada ya kutembelea ofisi za Multichoice Tanzania (DStv) Dar es salaam.

“Moja ya maagizo ya Mh. Rais Samia ni kuboresha mawasiliano, sasa katika maboresho tunazo baadhi ya kanuni, sera na sheria ambazo inabidi tuwe tunazibadili mara kwa mara ziendane na kasi ya mabadiliko ya sayansi na teknolojia duniani"— Nape.

"Leo pamoja na kuwashukuru DSTV Tanzania kwa kazi nzuri mliyofanya na kutambua mchango wenu kwenye sekta yetu nikasema leo nitangaze moja ya mabadiliko tuliyoyafanya kwenye kanuni zetu, kuna kanuni namba 18 ya mwaka 2018 inayohusiana na miundombinu ya utangazaji wa kidigitali, tumeifanyia marekebisho ili kuruhusu Channel za TV ambazo hazilipiwi (mfano CloudsTV, ITV n.k) ziweze kuonekana kwenye king'amuzi cha DSTV"— Nape.
 
Nimeiona hii habari kule twita, clouds tv ni moja kati ya local chaneli iliyorudishwa baada ya mabadiliko madogo ya sheria yaliyofanywa na waziri Nape Nnauye. Kurudi kwa chaneli mtatangaziwa tarehe rasmi.

8BF1E543-B89B-45DA-B667-9F01D1F10A61.jpeg


480B0749-FB34-4E19-B606-E304C80CB988.jpeg
 
Back
Top Bottom