Waziri Nape atembelea Multichoice, awarudishia DSTV 'local channels' baada ya marekebisho ya kanuni

Waziri Nape atembelea Multichoice, awarudishia DSTV 'local channels' baada ya marekebisho ya kanuni

So what? Clouds ina umuhimu gani kwa mazingira ya Tanzania with regard to Uhuru wa kuandika na kutangaza? All is Rubbish as long as hakuna uhuru wa kusema Tanzania! Huyu Clouds sana sana atatangaza mapambio ya Samia basi!....................sana sana
Oh kumbe kiongozi shida yako ni Samia. Pole sana
 
Kwahio hawa TING, STARTIMES, AZAM na wengine waliongia gharama kwenye mitambo ya kurusha matangazo ili waendane na SHERIA NA TARATIBU za nchi kwenye mawasiliano ni WAENDA NA WAZIMU.... Kwahiyo SHERIA imerekebishwa kwa ajili ya DSTV peke yake???
 
Nape anajitekenya na kucheka mwenyewe! Hivi Nape hajui kama DSTV ndio waligoma kuonesha channel bure yani king’amuzi kikiisha hizo channel kama TBC,ITVna TBC 1 zibaki zinaonesha ...

Lakini mwanzo ilikuwa kwamba Zote zinaonekana lakini kifurushi kikikata nazo zinakata!

Sasa serikali ikasema kuwa ni lazima channel zote zioneshwe bure hizo nne Dstv wakagoma kabisa..... na wakazitoa hizo channel!

Sasa hivi sijaelewa kama Dstv wamekubali kuonesha bure kabisa hizo channel kama lengo la serikali....?

Kwa hiyo DSTV ndio wamesurrender wataonesha Channel bure kabisa hazitakata hata kama kifurushi kikikata?
Aa wapi. Kifurushi kikiisha nazo hizo za kibongo wanaziondoa kabisa. Hata kwa azam ndivyo ilivyo
 
Unda tatizo tatua tatizo
Sawa na issue ya wamachinga, yaani jamaa anasema yawezekana wanachoma masoko ili kuwavuta na kuwateka akili kuwatoa kwa mwendazk kuwa alikuwa anawajali na kuwapa nafasi but now machinga (kama kweli walikuwa wao) wamezama mpaka mjengoni ikulu na kunyweshwa juice plus ahadi na kutunukiwa, kesho ni vigeregere na chereko, huyu ndiye tulimtarajia halellujah..!
 
Shida ilikua kwa multichoice au serikali
Maana naona neno “kawarudishia” wakati ving’amuzi shindani vilikua na free local channels
I’m curious 😟😟

TCRA iliwanyooshea kidole kutokana na kuzilipisha ilihali zilipaswa kuwa bure, Serikali imebadili sheria..
 
Aa wapi. Kifurushi kikiisha nazo hizo za kibongo wanaziondoa kabisa. Hata kwa azam ndivyo ilivyo

Sasa hii ziara na watu kushangilia kuna maana gani? Na kama DSTV wakikubali FTA sasa wakina Azam na wengine itakuwaje wao wanakata kifurushi kikiisha?
 
Hapa kwangu nasugua na TBC tu, vipindi nishazoea sasa, Shambani Shambani shambani, mazao bora shaaaambani. [emoji3][emoji3][emoji3][emoji3][emoji3][emoji3][emoji3][emoji3]
Na zile nyimbo za dini na sebene za akina Nyoshi na Tukuyu Sound Band bila kumsahau mzee wa zamadam 😃😃😃

Wallah DStv ikikata unajikuta lazima ununue tu maana ufala unaofuata ni TBCCM mwanzo mwisho mara ufundi sijui VETA, mara usalama barabarani, ungese mtupu haujakaa sawa unaona wanakata matangazo wanaleta Habari mubashara kutoka mkutano wa CCM yaani ilimradi wakukere tu.
 
Hakuna wakati hizo mnaita 'Free Channels' ziliwahi kuwa BURE, kifurushi kikiisha zinapotea….. labda ianze SASA.
Labda Kama hauna DStv decorder lakini hizo channel ukilipia unazipata Kama kawaida na ndio sheria ilivyokuwa inawataka wafanye hivyo na wasizirushe bure endapo kifurushi kitakata sasa wao walikuwa wanarusha ukilipia na usipolipia unaziona bado wakati leseni yao ilikuwa hairuhusu kurusha local channels bure.

What was happening watu labda wanachanganya kidogo, ilikuwa kifurushi kikiisha basi hizi channels za bure ambazo ni local zinabaki kuonekana ila ukilipia utaona channels za ziada za DStv.

Mwakyembe akasema DStv hawana kibali cha kuonyesha local channels bure sababu wao leseni yao ni tofauti. Hata hivyo hhi ilikuwa ni vita ya kibiashara kati ya wauza visimbuzi especially Azam by that time alikuwa amebanwa hawezi kuuza visimbuzi vyake sababu DStv walikuwa wamemiliki sana soko.

Ilipoondolewa channel za bure ambazo ilikuwa hata usipolipia unazipata, hata TBCCM ilikuwa haionekani walikuwa DStv wanazima inabaki channel 100 tu ya matangazo matupu ya kwao.

Baadae naona wakailazimisha DStv waonyeshe TBCCM kwenye channel za bure ambapo sasa ndipo ikabaki pekee kama hauna kifurushi unaangalia mapambio mwanzo mwisho.

Sasa naona Azam ameshapata soko lake wanaamua kubadilisha kanuni ili DStv nao waonyeshe za bure ambazo hata kama utaishiwa kifurushi utabaki nazo hizo za bure Kama zamani au kama Azam na wengine.

Hii ilikuwa Vita tu, sasa naona DStv wameongea na Nape ili nao wawe sawa na Azam na wengine although bei ya vidurushi na visimbuzi wanatofautiana lakini at least itasaidia na wengine tulishidlndwa kuwa na decorder nyingi mtu ana nyumba moja Ila decorder nne madishi yananing'inia juu ya bati kama mpo wapangaji kumi kumbe unaishi familia moja tu.
 
Back
Top Bottom