Labda Kama hauna DStv decorder lakini hizo channel ukilipia unazipata Kama kawaida na ndio sheria ilivyokuwa inawataka wafanye hivyo na wasizirushe bure endapo kifurushi kitakata sasa wao walikuwa wanarusha ukilipia na usipolipia unaziona bado wakati leseni yao ilikuwa hairuhusu kurusha local channels bure.
What was happening watu labda wanachanganya kidogo, ilikuwa kifurushi kikiisha basi hizi channels za bure ambazo ni local zinabaki kuonekana ila ukilipia utaona channels za ziada za DStv.
Mwakyembe akasema DStv hawana kibali cha kuonyesha local channels bure sababu wao leseni yao ni tofauti. Hata hivyo hhi ilikuwa ni vita ya kibiashara kati ya wauza visimbuzi especially Azam by that time alikuwa amebanwa hawezi kuuza visimbuzi vyake sababu DStv walikuwa wamemiliki sana soko.
Ilipoondolewa channel za bure ambazo ilikuwa hata usipolipia unazipata, hata TBCCM ilikuwa haionekani walikuwa DStv wanazima inabaki channel 100 tu ya matangazo matupu ya kwao.
Baadae naona wakailazimisha DStv waonyeshe TBCCM kwenye channel za bure ambapo sasa ndipo ikabaki pekee kama hauna kifurushi unaangalia mapambio mwanzo mwisho.
Sasa naona Azam ameshapata soko lake wanaamua kubadilisha kanuni ili DStv nao waonyeshe za bure ambazo hata kama utaishiwa kifurushi utabaki nazo hizo za bure Kama zamani au kama Azam na wengine.
Hii ilikuwa Vita tu, sasa naona DStv wameongea na Nape ili nao wawe sawa na Azam na wengine although bei ya vidurushi na visimbuzi wanatofautiana lakini at least itasaidia na wengine tulishidlndwa kuwa na decorder nyingi mtu ana nyumba moja Ila decorder nne madishi yananing'inia juu ya bati kama mpo wapangaji kumi kumbe unaishi familia moja tu.