Waziri Nape: Hatujaibania starlink kutoa huduma ya intaneti, Elon Musk bado hajakidhi vigezo tulivyomuwekea

Ndaga malafyale umeeleza ukweli kabisa

Magu was right sana yani angemaliza kipindi chake cha pili mambo Tz yangekuwa 🎂🍨🍦
 
Hio ofisi wanaitaka iwepo ili iwe rahisi ku manipulate hizo huduma na kwenda kuomba rushwa. Viongozi wetu tunawajua jinsi akili zao zilivyo mbovu.

Kuna uwezekano mkubwa kabisa ana payroll yake toka Voda, Halotel, Tigo na Zantel ili kuyalinda maslahi ya hizo kampuni na unyonyaji wao kwa raia hili wala halijifichi. Ndio maana hawezi kubali kumleta starlink maana akienea mtaani tu itakula kwao mazima.

Kila watu 4 wakiji organize kulipa dollar 60 kila mtaa hakutakuwa na biashara ya bundle tena.
 
Eti kumlinda Mtanzania 😂
Jamaa wanajifanya wana upendo sana na Mtanzania 🤣 inapofikia swala la maslahi yao kuguswa. Hili halina tofauti na tabia ya mama wa kambo kujifanya anakupenda pindi ndugu zako wakija na kukupakulia minyama wakati kitendo cha ndugu kuondoka tu utapigwa kabichi marage hadi uchakae.
 
sisi tunataka huduma, mambo ya ofisi yanakujaje sasa?
Aulizwe ofisi za whatsapp Tanzania ziko wapi🤣? Je, ni watanzania wangapi washawahi kulalamikia huduma za whatsapp toka ilipoanza kutumika rasmi mwaka 2009?

Facebook iko toka 2004 nani amewahi kulalamika juu ya facebook na huduma zake? Maboresho yanafanyika kila siku na watu wanainjoy, customer support iko live 24/7 na ni online tu.

Sahizi kuna instagram nafikiri toka 2012 imeanza kutumika rasmi duniani. Nani kawahi kulalamikia mamlaka kwamba instagram haifai? 😂 Watu wanafanya biashara zao fresh tu nani ambaye amelalamika kwa ofisi ya waziri.

Hayo ni makampuni ya kimarekani kama ilivyo starlink. Wenzetu hawana ubabaishaji kwenye huduma wamenyooka sasa kama mlitegemea kumpelekesha Elon Musk hio ni ndoto.
 
Isije kuwa akakataa ubia na wenye nchi, angalia = voda(ccm), Airtel (serikali), halotel(serikali) tigo(rosti tamu=ccm) au siyo hivyo jamani?
Mmarekani hawezi kupelekeshwa na ndezi wa CCM. 🤣 Hilo sahahu kabisa tena mtu mwenyewe ni billionaire. Elon kanyooka hawezi fanya kazi na mpuuzi wala hana njaa hizo.
 
Ukishasikia kumlinda Mtanzania au kwa maslahi mapana ya taifa jua hapo kuna ukakasi😁
🤣 Kuna mambo mawili ukiyasikia toka kwa mwana CCM fahamu fika kuwa upigaji unavishwa koti.

1. Amani ya nchi ni muhimu hatuwezi ruhusu watu wachache walete taharuki.

2. Kumlinda Mtanzania ni muhimu kwa maslahi mapana ya taifa.
 
Nape wacha siasa, Elon Musk ofisi ya nini hapa Tanzania? Si anaweka mawakala tu kama wanavyofanya konnect.

Sema mpaka awe na God Father wa uhakika. Mpeni Rostam tu, hakuna zaidi, yupo kwenye sector hiyo na anajuwa kula na vipofu.
Akipewa Rostam huduma itakuwa ya kinyonyaji tu kama ilivyo kwa hao akina Voda na wenzake.
 
Rostam ana hisa kwenye makampuni ya masiliano
 
🤣 Kuna mambo mawili ukiyasikia toka kwa mwana CCM fahamu fika kuwa upigaji unavishwa koti.

1. Amani ya nchi ni muhimu hatuwezi ruhusu watu wachache walete taharuki.

2. Kumlinda Mtanzania ni muhimu kwa maslahi mapana ya taifa.
Ukishasikia maneno matamu inabidi umuangalie msemaji kwa mashaka

 
Mzigo mwingine unaofuja pesa za walipa kodi ni huu..

Uwezo mdogo mipasho mingi maswali yamezidi kafunga section ya comments kama mwenzie wa afya.

Huyu niliwahi kumuuliza swali nashtukia kaniblock.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…