Waziri Nape Nnauye aitaka TCRA kuyaagiza Makampuni ya Mawasiliano kusitisha upandishaji wa bei ya Vifurushi

Waziri Nape Nnauye aitaka TCRA kuyaagiza Makampuni ya Mawasiliano kusitisha upandishaji wa bei ya Vifurushi

Tengeneza tatizo..kisha tatua..ili uchukue point tatu kwa wadanganyika..absurd.

#MaendeleoHayanaChama
 
Waziri wa Habari na Teknolojia ya Habari Mhe Nape Nnauye ameiagiza TCRA kuyaagiza makampuni ya simu kusitisha upandishaji wa bei ya Vifurushi mpaka hapo watakapokaa na Serikali kuzungumza kuhusu jambo hilo.

Chanzo: DarMpya

Pia soma
- Gharama za vifurushi vya intaneti zapandishwa tena kimya kimya. Je, ni censorship ya aina yake?
View attachment 2090532

Waziri wa Habari na Teknolojia ya Habari, Nape Nnauye​
Kauli za kisiasa hazisaidii bila KUBADILI sheria za ovyo kwenye sekta ya mawasiliano,ni kazi bure tu.
 
Hahaha nimecheka kwa sauti.

Tunaongozwa na wenye roho nzuri.

Tarehe 17 March tufanye sherehe ya kushukuru utukufu wa Mungu kwa kutuondolea lijitu libaya pale ikulu.

Sasa nchi kimyaàaaaaa. Tumeanza kusahau Yale mabaya
Mpumbavu wewe kabla huyo unayesema mwenye roho mbaya kufa,vifurushi vilikuwa bei poa, kaja shangazi yako kavipandisha makusudi leo hii wanataka kuvishusha ili wapate wajinga kama nyinyi kuja kuwatukuza.
 
Dawa ni ttcl kuacha kushirikiana kifisadi na makampuni binafsi ,viongozi wa ttcl wanapewa pesa na makampuni mengine ili kuhujumu ttcl kama ttcl ingeongozwa vizuri basi makampuni binafsi yasingekuwa na ubavu wa kuvimba watakavyo
 
Kwenye Market forces za demand and supply kila kampuni hulazimisha kuminimize cost na kumaximize profits

Consumer Ndio uwanja wa mapambano hahahaaaa!
 
Waziri wa Habari na Teknolojia ya Habari Mhe Nape Nnauye ameiagiza TCRA kuyaagiza makampuni ya simu kusitisha upandishaji wa bei ya Vifurushi mpaka hapo watakapokaa na Serikali kuzungumza kuhusu jambo hilo.

Chanzo: DarMpya

Pia soma
- Gharama za vifurushi vya intaneti zapandishwa tena kimya kimya. Je, ni censorship ya aina yake?
View attachment 2090532

Waziri wa Habari na Teknolojia ya Habari, Nape Nnauye​

Mwambieni Nape Nnauye kabla ajachukua hatua...awaulize makampuni na TCRA sababu za kupanda kwa vifurushi....
Haiwezekani upandishe kodi na tozo halafu uwalazimishe makampuni washushe bei za vifurushi! Hii itakuwa vichekesho
 
Kwenye Market forces za demand and supply kila kampuni hulazimisha kuminimize cost na kumaximize profits

Consumer Ndio uwanja wa mapambano hahahaaaa!
Hayo mambo ya vitabuni, kwa sasa karibu makampuni yote bei zinafanana na zimepandishwa na serikali wala si makampuni.

Nilikuwa nanunua gb. 7 halotel kwa 5000 tu sasa hivi kwa 10000 ndio napata hizo gb 7, Ni wizi wa mchana.
 
Mimi nasubiri nione kama ng'ombe hatakunywa maji. Tunaumizwa sana wananchi, lakini sina hakika kama Nape anaweza mfunga Paka kengele
 
Naona wanasiasa huwa wanajikita katika upandishaji wa vifurushi katika makampuni ya simu na kuyaacha makampuni ya ving'amuzi!

Kwa mfano, katika Startimes, mwaka 2016 kipindi hela inapatikana, kifurushi cha chini kilikuwa ni TSH 6,000/=, lakini leo hela ngumu kupatikana ni TSH 10,000/= kifurushi cha chini.

Lakini tujiulize, haya makampuni ya simu na ving'amuzi huwa yanapandisha gharama kwa kujitakia tu, au ni serikali ndio huongeza kodi kwa makampuni, hivyo nao huongeza gharama za vifurushi?

Tujiulize, kama zamani wateja walikuwa wachache lakini makampuni yaliweza kutoa ofa nyingi kwa bei nafuu, iweje leo wateja wengi halafu waongeze bei ya vifurushi? Kwani wanataka faida iliyopitiliza au makampuni yameongezewa kodi na serikali?

Sent from my TECNO F1 using JamiiForums mobile app
 
Back
Top Bottom