Waziri Nchemba: Utoaji risiti za kielektroniki imekuwa kama punguzo la bei, mteja asipopewa risiti anapunguziwa bei

Mtazame jinsi anavyosoma karatasi...hakuna element yoyote kwamba yupo serious.
Hayo mambo anayosoma hivi kweli kabisa kwa mtu mwenye PHD anahitaji kukodolea macho mstari kwa mstari?...vitu obvious ambavyo vinajulikana...
Usimuonee jamaa kana kwamba hukupata kuona summary ya thesis yake ya hiyo ndigrii. Msamehe bure.
 
Na waziri naye analalamika badala ya kuja na solution!!!
 
NINGELIKUWA KIONGOZI, MADUKA YA KARIAKOO NINGEYATENGENEZEA MFUMO ULE WA ZAMANI, KUYAKADIRIA KODI, KUYAPA NAMBA MAALUM ITAKAYOKUWA INAAMBATANA NA SIMU YA MUHUSIKA, NID, N. K, MADUKA YA KARIAKOO YAKADIRIWE KODI,
°HATUKOSI MADUKA, MIL 3, YA KIWANGO AMBAYO YATAKADIRIWA MIL 10 KWA MWAKA, HII INGESAIDIA KUTOKUKWEPA KULIPA MAANA WATAKUWA WAKO COMMITED KWA HILI, TATIZO LA KARIAKOO, WAJANJA NI WENGI MNO AND ARE SO BRIGHT.
N. B, biashara kubwa iliyopo kariakoo ni chukua hapa, uza kule!, yaani mwenye duka anachukuwa bidhaa duka lingine analetea mteja lakini anafremu!
 
Unaposikia CAG akisema Mabilioni yamepigwa na hakuna hatua zozote zinazochukuliwa hivi unakuwa na hamu tu ya kulipa kodi?

👆 naombeni majibu tafadhali.
 

Yeye na wnamCCM wenzake wangeanza kwa kuonyesha mfano.

Kwa vile CCM wameamua kula kwa urefu wa kamba zao na wananchi nao huo ndiyo urefu wa kamba zao.

Siku wakibadilika na sisi wananchi tutabadilika.
 
Kabisa. Pia kusafiri kwenye ndege, wasafiri kwenye madaraja ya kawaida. Wabunge wapunguzwe idadi, hawa wa viti maluum waondolewe pia. Kuna areas nyingi sana kupunguza matumizi ya serekali. Bila hivyo. mwananchi endelea kukwepa kodi kadiri uwezavyo.
 
Mfumo wa kodi wa kwetu ni wa kijinga sana kadri unavyoongeza lulipa kodi ndo unawekewa makadirio makabwa mafano 10% ya nyumba ya 1000000 sio sawa na 10 % ya 200, 000 sasa nani anataka

Sent from my SM-A037F using JamiiForums mobile app
 
Na ukijifanya kutoa risiti kaam wanavyotaka nakuhakikishia baada ya 3month unafunga hiyo biashara

Sent from my SM-A037F using JamiiForums mobile app
 
nikifikiriaga habari za Cag na icho anachokisoma waziri naona kama vile kichekesho cha Joti na Mpoki
 
Mara zote CAG anaposoma taarifa ya mahesabu ya serikali hua kuna ufisadi na ujambazi mkubwa hua unatajwa wa mabilioni ya fedha lakini hakuna yoyote ambae amewahi kushikwa na kufungwa kwa wizi huo na kinachoibwa ni Kodi zetu sisi, sasa ya nini kulipa Kodi na nikijua kabisa itaibwa na mwizi mtamficha hatochukuliwa hatua yoyote 🤔🤔si bora nikwepe tuu Kodi tukose wote
 
Ni kichekesho kuona waziri akilalamika wananchi kuiba Kodi lakini hashangai viongozi wenzake kukwapua Kodi za watanzania hivi niulize nyie viongozi wa ccm ni lini mtaacha ubinafsi? Akiiba mwanachi mnaumia mkiiba nyie ni sawa pumbafu kabisa
 
Tatizo ni matumizi makubwa ya Serikali kaka.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…