Waziri Nchemba: Utoaji risiti za kielektroniki imekuwa kama punguzo la bei, mteja asipopewa risiti anapunguziwa bei

Waziri Nchemba: Utoaji risiti za kielektroniki imekuwa kama punguzo la bei, mteja asipopewa risiti anapunguziwa bei

Kwanini mnahangaika na mauzo? Hangaikeni na manunuzi. Hili halitakiwi sababu litawagusa mpaka wakubwa wenye biashara. Mkicontrol manunuzi mtajua nani ana nini wakati gani.
 
Kwann mtushirikishe kwenye ulipaji Kodi na sio na kwenye matumizi ya Kodi zetu
 
Dabo tax,ni wizi mtupu bidhaa Moja Kodi mara sita.
Ukiingia bandarini Kodi,ukipeleka godown Kodi akija wa jumla Kodi,wa jumla akiuuza wa rejareja kodi wa reja akiuuza Kodi huu SI wizi,kwann Kodi isiwe Moja TU bandarini au ipunguzwe zaidi
 
"Matumizi ya mashine za kielekroniki kwa ajili ya kodi na kutoa risiti bado imekuwa ni changamoto kwa wananchi, kwasasa utoaji wa risiti umekuwa kama punguzo la bei manake mtu asipopewa risiti anapunguziwa bei tofauti na akidai risiti jambo ambalo linasababisha bidhaa nyingi kuuzwa nje na bei inayofahamika na TRA na hapa nataka niwakumbushe watanzania kuwa suala la kodi sio la TRA peke yake ni jambo la watanzania wote"

View attachment 2918088
Mimi kama Mimi nikipunguziwa bei nachangamkia fulsa.sababu hzo hela zenyewe wanalipana posho Tu huko na mishahara mkubwa Bila kuwakumbuka walipa kodi.mfano mwanza swala la barabara kila Pande mbovu.barabara ya nyamongoro stand kwenda nyamongolo kwenyewe barabara imechimbika inaweza sema hakuna serikali.kwa jumla ni maudhi sana.mm na Kodi mmmm[emoji125][emoji125][emoji125][emoji125]
 
Mmehamasisha matumizi ya cash kwa kuweka tozo za kipumbavu kwenye miamala ya kieletronic, vuneni matunda ya upumbavu wenu na huyo waziri weny wa fedha asiye na maono.
Sielewi kwanini bado BOT wana entertain matumizi ya cash, yanayopelekea watu wengi kukwepa kodi, hasa wafanya biashara.

Kwanini hatujifunzi hata kwa wenzetu Kenya??
 
Tatizo ni matumizi makubwa ya Serikali kaka.
Kariakoo janja nyingi sana, pia machinga lazima watengenezewe mfumo, maana bidhaa ya dukani na machinga anayo hiyo hiyo, hili linatengeneza mwanya mkubwa mno wa wizi, ni loop nzuri mno ya ukwepaji kodi.
MFUMO NILIOUBUNI UKIFANYIKA KILA ROBO YA MWAKA SEREKALI ITAWEZA PATA TRILION 2+.KWA KARIAKOO PEKEE.
 
Mtazame jinsi anavyosoma karatasi...hakuna element yoyote kwamba yupo serious.
Hayo mambo anayosoma hivi kweli kabisa kwa mtu mwenye PHD anahitaji kukodolea macho mstari kwa mstari?...vitu obvious ambavyo vinajulikana...
Mi kila siku najitahidi nikwepe kodi
 
Kariakoo janja nyingi sana, pia machinga lazima watengenezewe mfumo, maana bidhaa ya dukani na machinga anayo hiyo hiyo, hili linatengeneza mwanya mkubwa mno wa wizi, ni loop nzuri mno ya ukwepaji kodi.
MFUMO NILIOUBUNI UKIFANYIKA KILA ROBO YA MWAKA SEREKALI ITAWEZA PATA TRILION 2+.KWA KARIAKOO PEKEE.
Mkuu, naamini mfumo ulioubuni na kuupendekeza ni mzuri, Lakini vipi matumizi mabaya ya fedha na ubadhirifu unaofanywa na Serikali, unadhani kutakuwa na maendeleo kama hakuna udhibiti kwenye matumizi ya Serikali? 🤔
 
Kazi ya Govt Exchequer, nimependa mdhibiti wa Kenya, Mwigulu ajifunze Kenya, amwalike(mwana mama huyu) ili wapate experience!
 
Akemee ufisadi na matumizi mabaya ya hicho kidogo cha kodi kinachopatikana..
 
Kazi ya Govt Exchequer, nimependa mdhibiti wa Kenya, Mwigulu ajifunze Kenya, amwalike(mwana mama huyu) ili wapate experience!
Tatizo kubwa la viongozi wetu ni kiburi na dharau. Mtu akiishaaminiwa na kukabidhiwa mamlaka ya Dola anageuka kuwa Mungu mtu.
 
Mkuu, naamini mfumo ulioubuni na kuupendekeza ni mzuri, Lakini vipi matumizi mabaya ya fedha na ubadhirifu unaofanywa na Serikali, unadhani kutakuwa na maendeleo kama hakuna udhibiti kwenye matumizi ya Serikali? [emoji848]
Mama abduli ataenda kununulia saa hata ya billion 5 au hata kikuku cha mili 20
 
Wakitaka hiyo isitokee kila mfanyabiashara alipe VAT, haiwezekani tuwe na tabaka 2 kuna wenye ulazima wa kulipa VAT na wasio na ulazima wa kulipa VAT, vilevile serikali yenyewe haitaki kulipa VAT na ndio usababisha ukwepaji wa kodi hasa huku ngazi za halmashauri.
 
Tanzania inateswa na mfumo wa ukusanyaji tu, hasa hizi level / ngazi mbalimbali za wafanyabiashara.,umachinga unapoteza almost 25% ya mapato halisi, kwa kuuza bidhaa zenye hadhi ile ile inayoptikana madukani,bila mfumo rasmi,pia machinga hutumiwa na wafanyabiashara wakubwa kwa kupewa mali wauze, labda sasa machinga wawe wanabanwa kwa kuulizwa risiti walikonunulia mali, hizi meza kariakoo ni drop points za wafanyabiashara wenye magodown pekee wasiohitaji kuwa na maduka,ndio maana Kenya wanatumia mfumo wa makadirio zaidi,
Shop number
Jina la mfanyabiashara
NIDA yake
Contact zake
GPS position yake
 
Back
Top Bottom