Waziri Ndejembi akutana na Balozi wa Oman, wajadili masuala ya mafuta na gesi

Waziri Ndejembi akutana na Balozi wa Oman, wajadili masuala ya mafuta na gesi

Roving Journalist

JF Roving Journalist
Joined
Apr 18, 2017
Posts
5,352
Reaction score
15,876
Waziri wa Nishati, Deogratius Ndejembi amekutana na kufanya mazungumzo na Balozi wa Oman nchini Tanzania, Mhe. Saud Al-Shidhani yaliyolenga kuimarisha na kuendeleza ushirikiano kati ya nchi hizo mbili katika sekta ya nishati. Mazungumzo hayo yamefanyika leo, tarehe 17 Februari 2026, katika Ofisi Ndogo za Wizara ya Nishati jijini Dar es Salaam.
WhatsApp Image 2026-02-17 at 13.22.28.jpeg
Katika mazungumzo hayo, wamejadili kuhusu masuala mbalimbali ikiwemo kubadilishana uzoefu wa kitaalamu, mafunzo kwa wataalamu, teknolojia ya uchimbaji pamoja na usimamizi wa miradi ya gesi na mafuta kwa lengo la kuharakisha maendeleo kupitia Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania (TPDC) na Shirika la Maendeleo ya Mafuta la Oman (PDO).
WhatsApp Image 2026-02-17 at 13.22.29.jpeg

WhatsApp Image 2026-02-17 at 13.22.33.jpeg
 
Tanganyika itapata maendeleo ya kweli baada ya kugawa kila kitu
 
Tanganyika itapata maendeleo ya kweli baada ya kugawa kila kitu
Kivipi mkuu?
Au kwakuwa ni waarabu na kasumba bado zimo kwenye vichwa vya waswahili kwamba waarabu ni watu wabaya na waovu, ila mzungu ndio bwana kwa waswahili.
 
Back
Top Bottom