Waziri Ndejembi ataka uadilifu na kutenda haki kwa watumishi wa sekta ya ardhi

Joined
May 14, 2024
Posts
94
Reaction score
75
Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. Deogratius Ndejembi amewataka watumishi wa sekta ya ardhi nchini kuongeza uadilifu na kutenda haki katika utekelezaji wa majukumu yao sambamba na kuongeza kasi katika utendaji kazi.
IMG_20240727_144337.jpg

Mhe. Ndejembi namesema, suala la ardhi ni gumu na linahitaji watumishi kuwa makini ambapo amesisitiza kuwa ni lazima watumishi wa sekta ya ardhi watende haki huku wakizingatia kuwa kuna sheria, kanuni na miongozo inayowaoongoza katika utendaji kazi.

Aidha, Mhe. Ndejembi amesema, yale yote mazuri yaliyofanywa na mtangulizi wake ikiwemo Klinik za Ardhi atayaendendeleza kwa lengo la kuleta ufanisi wa wizara.

‘’Sikuja kutengua torati, yote aliyoyaanzisha mtanguluzi wangu ikiwemo klinik za ardhi zitaendelea na vile vile anayehisi jambo lake limekwama ajitokeze na atahudumiwa’’ amesema Mhe. Ndejembi.

Mhe. Ndejembi ametoa kauli hiyo tarehe 26 Julai 2024 wakati akizungumza na viongozi pamoja na watumishi wa Wizara ya Ardhi mkoa wa Dar es Salaam mara baada ya kutoka kuapishwa kushika nafasi hiyo kutoka kwa mtangulizi wake Mhe. Jerry Silaa.

Sambamba na hayo Waziri huyo wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi ametaka kuimarishwa kwa mifumo ndani ya wizara ili migogoro ya ardhi isiendelee kujitokeza.

Mhe. Ndejembi ameapishwa na Rais Mhe. Dkt Samia Suluhu Hassan kuwa Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi akitokea Ofisi ya Waziri Mkuu (Kazi, Ajira na Watu wenye ulemavu).
 
Hahahah!! Chura mwenyewe Dalali

KAZI ni kipimo cha UTU
 
Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. Deogratius Ndejembi amewataka watumishi wa sekta ya ardhi nchini kuongeza uadilifu na kutenda haki katika utekelezaji wa majukumu yao sambamba na kuongeza kasi katika utendaji kazi.
View attachment 3053701
Mhe. Ndejembi namesema, suala la ardhi ni gumu na linahitaji watumishi kuwa makini ambapo amesisitiza kuwa ni lazima watumishi wa sekta ya ardhi watende haki huku wakizingatia kuwa kuna sheria, kanuni na miongozo inayowaoongoza katika utendaji kazi.

Aidha, Mhe. Ndejembi amesema, yale yote mazuri yaliyofanywa na mtangulizi wake ikiwemo Klinik za Ardhi atayaendendeleza kwa lengo la kuleta ufanisi wa wizara.

‘’Sikuja kutengua torati, yote aliyoyaanzisha mtanguluzi wangu ikiwemo klinik za ardhi zitaendelea na vile vile anayehisi jambo lake limekwama ajitokeze na atahudumiwa’’ amesema Mhe. Ndejembi.

Mhe. Ndejembi ametoa kauli hiyo tarehe 26 Julai 2024 wakati akizungumza na viongozi pamoja na watumishi wa Wizara ya Ardhi mkoa wa Dar es Salaam mara baada ya kutoka kuapishwa kushika nafasi hiyo kutoka kwa mtangulizi wake Mhe. Jerry Silaa.

Sambamba na hayo Waziri huyo wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi ametaka kuimarishwa kwa mifumo ndani ya wizara ili migogoro ya ardhi isiendelee kujitokeza.

Mhe. Ndejembi ameapishwa na Rais Mhe. Dkt Samia Suluhu Hassan kuwa Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi akitokea Ofisi ya Waziri Mkuu (Kazi, Ajira na Watu wenye ulemavu).
Kwa dar es salaam ni ngumu sana.
Pale Halimashauri yupo mnyakyusa mmoja anaitwa Lugano Mwambuluma ni tatizo sana. Yeye ndio anaamua kibali kipi kiende wizarani na kipi kisiende kwa sababu za rushwa.

Wizarani kuna bwana mmoja anaitwa Masatu ni shida sana. Bila laki kadhaa, hawezi kuruhusu muamala wako uende kwa Kamishina kupata approve.

Kiufupi wizara ya ardhi ni wizara mbovu sana.
 
Back
Top Bottom