Waziri Ndejembi: Nchi yetu imeendelea kuwa na uhakika wa upatikanaji wa Mafuta

Waziri Ndejembi: Nchi yetu imeendelea kuwa na uhakika wa upatikanaji wa Mafuta

Waufukweni

JF-Expert Member
Joined
May 16, 2024
Posts
5,383
Reaction score
18,776
Akiwasilisha Makadirio ya mapato na Matumizi ya Wizara kwa mwaka 2026/2027 Bungeni Dododma leo Aprili 22, 2026, Waziri wa Nishati nchini, Deogratius John Ndejembi amesema;

"Nchi yetu pia imeendelea kuwa na uhakika wa upatikanaji wa bidhaa ya mafuta ya petroli; yaani petroli, dizeli, mafuta ya taa na mafuta ya ndege. Pamoja na kuwepo kwa changamoto za upatikanaji wa bidhaa hizi na kuongezeka kwa gharama za upatikanaji wake, kilichosababishwa na vita baina ya Marekani, Israel na Iran."

"Vita hiyo imesababisha kufungwa kwa Mlango Bahari wa Hormuz (Strait of Hormuz) unaopitisha zaidi ya 20% ya mafuta yote duniani, kuathiri visima vya mafuta, mitambo ya kuchakata mafuta ghafi (refineries) na magala ya kuhifadhi mafuta, na hivyo kuathiri mnyororo mzima wa upatikanaji wa mafuta duniani kote."

"Vita hii imeziaathiri sana nchi za Mashariki ya Kati na Falme za Kiarabu kama Saudi Arabia, Bahrain, Oman na Kuwait, ambapo nchi yetu inaagiza kiasi cha 59% ya mafuta yake. Pia, kiasi cha 41% cha mafuta kinatoka nchini India, ambapo nao hutegemea kupata mafuta ghafi kutoka Mashariki ya Kati."

"Hatua zilizochukuliwa na serikali ili kuhakikisha nchi yetu inaendelea kuwa na uhakika wa upatikanaji wa mafuta ni pamoja na kuliwezesha Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania (TPDC), ambalo ni shirika la taifa la mafuta, kuagiza kiwango cha mafuta kinachotosheleza kipindi cha miezi mitatu ijayo."

"Aidha, serikali inaendelea kufuatilia kwa karibu mwenendo wa upatikanaji wa mafuta duniani na itaendelea kuchukua hatua mbalimbali za kimkakati ili kuhakikisha nchi yetu inaendelea kuwa na uhakika wa upatikanaji wa mafuta na hivyo kutoghathiri utekelezaji wa shughuli za kiuchumi na kijamii."

 
Huyu kijana wa Khamenei anasemaje kuhusu ili jambo la mfereji?
 
Changamoto
21 April 2026
Dar es Salaam, Tanzania

INVESTIGATION COVERS MAJOR ISSUE|| ZAMBIANS REVEALS WHAT HAPPENED|| THESE ARE THE AGREEMENTS​

The Zambia Union of Tanker Drivers and Allied Workers ZUTDAW president Shaft Mubanga while in Dar es Salaam says Oil Marketing Companies are not adhering to strict standards of delivering petroleum using tankers to Zambian customers

View: https://m.youtube.com/watch?v=crCE3JSFHCw
ZUTDAW), has been actively engaging in Dar es Salaam to address the welfare of Zambian tanker drivers operating along the Dar-Zambia route. Key issues focus on improving working conditions, addressing security concerns, and ensuring fair treatment for drivers transporting fuel.
 
Changamoto

21 April 202
Dar es Salaam, Tanzania

Makampuni ya ugavi wa mafuta ya Tanzania kwenda Zambia lawamani

View: https://m.youtube.com/watch?v=TNXB0bJeYuA
Baada ya CHAWAMATA kupokea malalamiko ya madereva wa malori ya kusafirisha mafuta kwenda nchi jirani wa chama cha madereva wa Zambia Union of Tanker Drivers and Allied Workers ZUTDAW kukumbana na changamoto wanapowasili sehemu za kushusha mzigo wa mafuta kuwa kuna upungufu wa mafuta waliyoyasafirisha
 
April 2026

Fuel supply remains stable this week, with Zambia holding strong stock levels with daily inflows.


View: https://m.youtube.com/watch?v=fM0oGShZaiY
Fuel supply remains stable this week, with Zambia holding strong stock levels supported by continuous daily inflows. The country currently has 41 days of diesel cover, combining local reserves and fuel in transit, alongside 18 days of petrol cover.

Government has moved to strengthen the system where challenges have been observed. Measures now in place include mandatory declaration of fuel movement by oil marketing companies, enhanced enforcement against stations withholding fuel and the rollout of a real-time tracking system to monitor fuel from depot to pump.

At the same time, efforts to diversify import routes and sources are underway to reduce exposure to global supply disruptions and stabilise costs.
Source : Director Spokeperson
 
Upatikanaji wa uhakika wa mafuta kwa bei ya 3800+ mpaka 4000+, ni ujinga tu na mzigo mzito kwa wananchi. Watuambie hatua walizochukua kuhakikisha bei inapungua.
 
Back
Top Bottom