Stephano Mgendanyi
JF-Expert Member
- May 16, 2020
- 2,833
- 1,301
WAZIRI NDUMBARO AHIMIZA MABADILIKO CHUO CHA MICHEZO MALYA
Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Dkt. Damas Ndumbaro amewataka watuishi wa Chuo cha Maendeleo ya Michezo Malya wafanye mabadiliko katika utendaji kazi wao ili waendane na kasi ya mabadiliko ya sekta hiyo hapa nchini.
Mhe. Ndumbaro amesema hayo alipofanya ziara chuoni hapo Julai 1, 2024 kukagua maendeleo ya taaluma na miundombinu ya chuo hicho.
Ammkizungumza na watumishi wa chuo hicho amewataka wabadilike katika utendaji kazi wao na kuepuka kufanya kazi kwa mazoea ili waongeze thamani ya kile wanachokifanya.
Aidha, katika ziara hiyo Waziri Ndumbaro ametembelea na kukagua ujenzi wa Akademia ya michezo ambapo ameagiza mshauri elekezi ahakikishe anamsimamia vizuri Mkandarasi ili kazi hiyo ifanyike kwa ubora.
Katika hatua nyingine Waziri Ndumbaro ametembela ujenzi wa hosteli mpya za wanafunzi ambazo ujenzi wake umefikia asilimia 84% pamoja na kuzungumzo na Wanachuo. @chuochamaendeleoyamichezo