Pre GE2025 Waziri Ndumbaro: Serikali haipendi kabisa matamko ya kukurupuka ya TLS

Pre GE2025 Waziri Ndumbaro: Serikali haipendi kabisa matamko ya kukurupuka ya TLS

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)
Mwanaharakati wa haki za binadamu huwa hawezi kuwa msimamizi bora wa taasisi ya kisiasa.
 
Alipokuwa nguli wa Sheria Prof.Kabudi , Mwabukusi alinywea na kupotea kabsa Sasa karudi. Nilisema Kabudi atamdhibiti na kumpoteza Mwabukusi
Huyo Kabudi si ndio waliingia kwenye vikao vya siri na wazungu kujadili mikataba, akatoka na porojo za $300 kama goodwill, huku ripoti fake ya kina Profesor Ossoro ikisema tunadia $192b? Mara akaja na porojo sijui za 50/50, sijui 16% kama mrabaha, yaani sijawahi kuelewa hata anaongea nini, na hizo $300m za goodwill hadi leo hazieleweki zimelipwa kiasi gani, na kila siku tunalipishwa huko nje huku Kabudi kajikausha kama sio yeye alikuwa analeta porojo chini ya dhalimu magu.
 
Wakuu,

Kwahiyo Ndumbaro anasema wanapotoa matamko wanakuwa wametoka usingizini na kuja kuongea ushudi wakati hawana facts?:BearLaugh::BearLaugh::BearLaugh:


Waziri wa Katiba na Sheria, Dkt. Damas Ndumbaro, ametoa wito kwa Chama cha Wanasheria Tanganyika (TLS) kuachana na tabia ya kutoa matamko ya kukurupuka, akisisitiza kuwa Serikali haifurahishwi na mwenendo huo.

Dkt. Ndumbaro ametoa kauli hiyo, Desemba 16, 2024, katika ofisi za Wizara ya Katiba na Sheria, Mtumba, jijini Dodoma, wakati wa hafla ya kusaini mkataba wa makubaliano kati ya Wizara hiyo na TLS. Hafla hiyo pia imehusisha kukabidhi gari jipya kwa chama hicho, ambalo litatumika katika shughuli za kusaidia utoaji wa huduma za msaada wa kisheria kwa wananchi.

Kwa upande wake, Makamu wa Rais wa TLS, Leticia Ntagazwa, amesisitiza kuwa kupokea msaada wa gari kutoka Serikali haimaanishi kuwa chama hicho kimehongwa au kimenunuliwa, akieleza kuwa chama hicho kina jukumu la kuwatumikia Watanzania kwa kuhakikisha haki zao zinalindwa na Mahakama zinawajibika kwa kutenda haki.

Makubaliano hayo yanalenga kuimarisha ushirikiano kati ya Serikali na TLS katika kuhakikisha wananchi wanapata huduma za msaada wa kisheria kwa ufanisi zaidi, sambamba na kuimarisha uwajibikaji wa vyombo vya utoaji haki nchini.
 
BAK Boniface Mwabukusi unasimangwa huku. Tunakuombea Mungu akulinde, maana hawa jamaa Wana majini hatari sana, yanawashusha watu haya kwenye mabasi mchana kweupe.
 
Kwahiyo wanataka TLS wawe watu wa mapambio kumsifu Samia?
 
Nchi haiongozwi kwa sheria, inaongozwa kwa mambo mengi🤔😏🐼
 
Serikali inapotoa rushes ktk vyombo vyake ili isemwe vizuri
 
Waziri wa Sheria na Katiba, Mh. Ndumbaro, amewapa za uso Chama cha Wanasheria Tanganyika kwamba kinatoa matamko ya kukurupuka tu.
===============
Waziri wa Katiba na Sheria, Dkt. Damas Ndumbaro, ameonesha kutofurahishwa na mwenendo wa Chama cha Wanasheria Tanganyika (TLS) kwa kutoa matamko ya kukurupuka dhidi ya serikali. Amesema vitendo na matamko hayo ni vigumu kukubalika na hakuna serikali duniani inayovumilia kushushiwa hadhi yake.

Soma Pia: Waziri wa Katiba na Sheria (Ndumbaro): Tanzania inaendelea kwa sababu kuna Haki, Usawa na Amani

Ni katika muktadha huo, Dkt. Ndumbaro ametoa wito kwa TLS kuboresha mahusiano na Serikali kwa kuongeza majadiliano kati ya pande hizo mbili. Amesema hayo Jijini Dodoma wakati wa utiaji saini wa hati ya makubaliano ya utoaji huduma za kisheria kwa wananchi kati ya serikali na TLS.


Nchi ya machawa sasa. Hai ongezwi kwa sheria pekee bali nini !!
 

WAZIRI DKT. NDUMBARO AONYA MATAMKO TLS

WAZIRI wa Katiba na Sheria Dk. Damas Ndumbaro amekitaka Chama cha Wanasheria wa Tanganyika (TLS) kuacha kutoa matamko yanayovunja hadhi ya serikali badala yake kutumia busara katika kuikosoa na kuielekeza kwa kukaa pamoja mezani.

Dk. Ndumbaro amesema hakuna serikali yoyote duniani ambayo itavumilia kushushiwa hadhi yake akitolea mfano wan chi za Marekani, Ulaya na China na kusema kuwa matamko ama vitendo vyovyote vyenye uashiri wa kuivunjia hadhi serikali havitakubalika.

“Kuna wakati tunaweza kuwaambia kwamba hiki sisi hatujapenda, lakini kuna wakati sisi tunaweza tukakaa kimya tu, tukasubiri, aah sawa na sisi tunawasubiri kwenye kona Fulani tutakutana tu. Kama TLS mnadhani serikali imekosea milango iko wazi badala ya kukimbilia kwenye vyombo vya habarimnatoa matamko ya ajabu ajabu njooni tuongee.” Alisema Waziri Dk. Ndumbari alipozungumza na viongozi na wanachama wa chama hicho wakati wa hafla ya kusaini makubaliano ya ushirikiano baina ya serikali na chama hicho mkoani Dodoma jana.

Katika hafla hiyo, pia wizara ilikabidhi gari jipya aina ya Toyota Landcruiser Prado kwa chama hicho kwa lengo la kusaidia utendaji kazi wa chama hicho katika kutoa msaada wa kisheria kwa wananchi.

Kwa upande wake Makamu wa Rais wa TLS, Laetitia Ntagazwa alisema matamko yanayotolewa na TLS yanategemea na tabia ya kiongozi aliyepo wakati huo kwa maana kila mmoja amelelewa kwenye makuzi tofauti na kwamba ndani ya chama hicho viongozi ambao ni wanaharakati na wasio wanaharakati hivyo lazima itokee wakati kuwa na mihemko kwa mtu husika.

“Kimsingi katika uongozi wetu kuna wengine ndani yetu ni wanaharakati lakini kuna wengine pia sio wanaharakati kwa hiyo ni lazima utegemee kwamba kuna wakati inawezekana kiongozi wa awamu fulani akawa na mihemko lakini mihemko ile haiondoi sifa na wajibu wa chama cha wanasheria wa Tanganyika wa kuhudumia umma wa watanzania. Kwa hiyo tuseme tu kwamba serikali inapaswa pia kutuelewa kwamba tunapokuwa tunafanya hayo wakati mwingine hatufanyi kwa nia ovu, tunafanya kwa nia ya kuwakumbusha ili kuhakikisha kwamba umma wa watanzania unafurahia maisha.” Alisema Wakili Ntagazwa.
 

Attachments

  • Screenshot 2024-12-17 at 10-58-35 Instagram.png
    Screenshot 2024-12-17 at 10-58-35 Instagram.png
    763 KB · Views: 1
Back
Top Bottom