Waziri Pindi Chana, tafadhali anzia Kituo cha Boti za Zanzibar na Viwanja vya ndege. Watu wetu wanatudhalilisha na kutuaibisha sana!

Waziri Pindi Chana, tafadhali anzia Kituo cha Boti za Zanzibar na Viwanja vya ndege. Watu wetu wanatudhalilisha na kutuaibisha sana!

Lord denning

JF-Expert Member
Joined
Jun 3, 2015
Posts
15,819
Reaction score
33,255
Jana blogger maarufu katika Mtandao wa You Tube muingereza Jason Billam amepost kuhusu safari yake kutoka Dar es Salaam kwenda Zanzibar.

Blogger huyu amekuwepo Tanzania kwa muda wa wiki sasa na amekuwa akielezea mengi mazuri kuhusu Tanzania jambo ambalo ni zuri kiutalii

Jambo la kusikitisha kama ilivyo kwa Watalii wengine nyakati tofauti, blogger huyu ameelezea kuhusu tukio la kuwa harassed na watu wa ulinzi ( Security) wakati akiboard meli kwenda Zanzibar katika kituo chetu cha Bandari hapa Dar es Salaam.

Blogger Huyu bila kumung’unya maneno ameelezea kuhusu alivyoombwa fedha elfu ishirini na Ofisa wetu huyo.

Kusema kweli hiki ni kitendo cha aibu sana na kinarudisha sana nyuma jitihada zinazofanywa na Serikali kwenye kukuza Utalii!

Hii si mara ya kwanza kwa watalii kulalamika kuombwa hela/rushwa na watu wetu wanaosimamia mambo ya ulinzi kwenye vituo vyetu

Naomba Waziri Pindi Chana lifuatilie hilo na mtumishi huyu achukuliwe hatua kali za kinidhamu na Mamlaka ili iwe fundisho na tabia hizi zikome mara moja

Unaweza kuangalia video Hiyo ambayo Mtalii huyu aliyekuja Tanzania anelalamika!

528B31CB-3860-435B-8777-0C74C9E47F42.jpeg
 
Huyo nadhani amewekwa kwenda kufanikisha wamasai wafukuzwe ngororongoro ili wamilikishwe waarabu
 
Huyo mzungu naye mzungu njaa. Hiyo ni aliyoombwa ni bakshishi (tips) tuu. Tena ni aibu mpaka aombwe badala ya yeye mwenyewe kujitolea.
 
Huyo mzungu alikuwa hajuj huku kwetu kila mbuzi anakula kwa urefu wa kamba yake, umwambie huyo blogger hayo ndio maneno ya mwenyekiti wako unaempigia debe huku kila siku.
 
Huyo mzungu alikuwa hajuj huku kwetu kila mbuzi anakula kwa urefu wa kamba yake, umwambie huyo blogger hayo ndio maneno ya mwenyekiti wako unaempigia debe huku kila siku.
Lini Mwenyekiti kasema watu watende kinyume na maadili yao ya kazi? Au kiswahili kinakupiga chenga?
 
Walinzi wanatekereza agizo la sa100 la kula kwa urefu wa kamba..

#MaendeleoHayanaChama
 
Hauwezi tenganisha rushwa na utawala wa kikwete FULL STOP wewe mwenyewe mleta mada unalijuwa hilo.
 
Huyo mzungu naye mzungu njaa. Hiyo ni aliyoombwa ni bakshishi (tips) tuu. Tena ni aibu mpaka aombwe badala ya yeye mwenyewe kujitolea.
Mkuu hiyo tips kwa afisa usalama ni kwa kazi gani labda?.

Tuache kulazimisha vitu kwenye mambo ya msingi, maafisa waliopo bandarini kwanza mpaka uonane naye yahitaji muda sasa huyo mpaka kumfuata ndg blogger uoni ni aibu!, Mbona hawatufuati sisi ndg zao kuomba hiyo tip.

Alafu kaa ujue tip huwa aiombwi asee hao jamaa ukimfanyia jambo kwa mazingira mliyopo anakutoa tu, siyo lazima ukajidhalilishe na magwanda ya serikali.
 
Lini Mwenyekiti kasema watu watende kinyume na maadili yao ya kazi? Au kiswahili kinakupiga chenga?
Mwenyekiti wako alitoa hiyo kauli nabhajawahi kuikanusha mpaka leo, usimuwekee maneno mdomo hata kama wewe ni chawa wake.
 
kitendo cha kushika simu yake juu juu anajirekodi hadi anavuka barabara ashukuru sana kwa hilo vinginevyo angepost gazeti hapa kwa kutumia internet cafe akiongeza na tukio jingine la kuporwa simu akiwa anailetea nchi ela.
#bongoNyoso
 
Back
Top Bottom