Waziri Pindi Chana, Taifa Stars haihitaji Hamasa na Maombi kwa Mungu bali Maandalizi makubwa na Utayari wa Wachezaji

GENTAMYCINE

JF-Expert Member
Joined
Jul 13, 2013
Posts
60,660
Reaction score
121,325
Binafsi tokea uteuliwe kuwa Waziri wa Wizara ya Sanaa, Utamaduni na Michezo sijaona la maana ulilofanya hata katika Press Conferences zako zote.

Yaani kabisa Waziri mzima unasimama mbele ya watu wenye akili (akina GENTAMYCINE na wengineo hapa JamiiForums) unatuambia tufanye maombi (dua) ili Taifa Stars ishinde dhidi ya Uganda huko Misri na siku nne baadae Tanzania?

Kwahiyo Watanzania tu ndiyo tunatakiwa tumuombe Mwenyezi Mungu Taifa Stars yetu ishinde ila Waganda wao hawahitaji Baraka za Mungu huyu huyu ambaye unatuhimiza Watanzania tumuombe atusaidie?

Nimejaribu kuangalia sehemu (nchi) mbalimbali kama Argentina, Brazil, France, Spain, Germany, Italy na Croatia kuona kama na wao Mawaziri wao wa Michezo huwa wanahimiza Wananchi wao kufunga kula na kunywa kuomba dua kwa Mwenyezi Mungu ili Timu zao zishinde.

Timu ya Taifa inashinda kwa Maandalizi, Mikakati, Uzalendo wa Kweli, Mipango thabiti, Malengo, Kujitoa (Commitment) kwa Wachezaji na Benchi la Ufundi Bora.

Msitulazimishe tuanze kuwadharau.
 
Uwaziri wa michezo Tanzania ni dampo. Wanapelekwa pale wanaoharibu huko kwingine lakini bado Wana konekosheni na wateuaji. Ifike mahali mishahara ya Mawaziri ilipwe kulingana na ukubwa wa wizara.
Katika nchi yenye malengo ya kufanikiwa kimichezo Pindi hawezi hata kuwa mtundika jezi kwenye vyumba vya kuvalia.
 
Kweli wanategemea kina Job watampa mpira Feisal?
Maana pale Airport tuu wamemtenga
 
Back
Top Bottom