Pre GE2025 Waziri Ridhiwani akabidhi hundi ya mil 730 kwa vijana, wanawake na wenye ulemavu Muheza

Pre GE2025 Waziri Ridhiwani akabidhi hundi ya mil 730 kwa vijana, wanawake na wenye ulemavu Muheza

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)

The Watchman

JF-Expert Member
Joined
Nov 7, 2023
Posts
896
Reaction score
1,427
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu - Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu Mhe. Ridhiwani Kikwete (Mb) amekabidhi hundi ya shilingi Milioni 730 kwa Vikundi 74 vya Vijana, Wanawake na Watu wenye Ulemavu inayotokana na asilimia 10 ya mapato ya Halmashauri ya Muheza Jijini Tanga.

Akizungumza wakati wa kukabidhi hundi hiyo, amesema utaratibu wa kutoa Mkopo kwa makundi hayo umekamilika hivyo kikundi au mtu mmoja anayekidhi vigezo ataanza kunufaika na Mkopo huo.

Soma pia: Special Thread: Mijadala na Matukio ya Uchaguzi Mikoa yote Tanzania Bara na Zanzibar kuelekea Uchaguzi Mkuu 2025

Mhe. Ridhiwani amebainisha kuwa, mkopo huo utatolewa kwa waliokidhi vigezo na waliopewe elimu ya matumizi ya pesa hiyo ili kuepuka changamoto zilizokuwepo awali ikiwepo kubadilisha matumizi ya Mkopo huo na kufanyia mambo mengine hivyo kupelekea wakopaji kutorejesha pesa hizo kwa wakati na kushindwa kulipa kabisa.

Amesema Serikali ya Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania inayo pesa ya kutosha kwa ajili ya utoaji wa Mikopo ya asilimia 10 iwapo kikundi au mtu mmoja mmoja atakidhi vigezo vilivyowekwa.

Katika hatua nyingine, Mhe. Ridhiwani amewasisitiza wanufaika wa mkopo huo kurejesha pesa hizo kwa wakati ili watu wengine waweze kukopeshwa na kuanzisha ama kuendeleleza shughuli za uzalishaji.
c5312d141e4d8f771a9dfe935dce2f7c.jpg
 
Back
Top Bottom