Waziri Selemani Jafo amsema Mkurugenzi wa SCOL Building Contractors Limited hadi akaanguka na kuzimia

Waziri Selemani Jafo amsema Mkurugenzi wa SCOL Building Contractors Limited hadi akaanguka na kuzimia

Mchaga na uinjinia wa barabara ni wapi na wapi. Fani ya mchaga ni kupita juu barabara akiwa na bidhaa mkononi kwenda kuuza, hamuoni hata ndula alizotinga ?

Acha ujinga we nyang'au!
Una ugomvi gani na Wachaga we mwehu? Katika Makabila ya Tanzania Wachaga ndo wamekwenda shule kuliko makabila mengine na ndio maana utakuta wako kwenye Taasisi nyingi za Serikali na wengine wana Makampuni yao kama huyu SKOL.Kama unataka kujua Wachaga ni watu tofauti angalia LEGACY aliyoiacha Mzee Mengi!
 
Minaki moja siyo
Haka kajamaa bhana kana maneno mengi tangu school.
Kiranja wangu wa chakula, alikuwa hakauki jikoni kuonja onja chskula.
Kuna wakati tuligomea msosi maharage hayakuiva, yeye alijifungia ndani jikoni akila kwa walibzi, watu walimmainfi sana. huyu
 
Lushindo lwa awamu ya chato
Kule Sumaye kakimbia anadai kakiona cha Moto huku Mkandarasi kazimia mbele ya Waziri [emoji1787][emoji1787] Hakika tutaona mengi mno ndani ya hiki kishindo cha5 duuhh
 
Nimeikuta sehemu
Nalog off
 

Attachments

  • IMG-20191206-WA0007.jpg
    IMG-20191206-WA0007.jpg
    38.1 KB · Views: 4
Hahaha huyu hatupwi kwenye jehanam ya moto,atajitupa mwenye jehanam ya moto
 
Mchaga na uinjinia wa barabara ni wapi na wapi. Fani ya mchaga ni kupita juu barabara akiwa na bidhaa mkononi kwenda kuuza, hamuoni hata ndula alizotinga ?
Huyo anauwezo wa kukulisha ww na familia yko mpk mseme inatosha!
Usimchukulie poa

Ova
 
Acha ujinga we nyang'au!
Una ugomvi gani na Wachaga we mwehu? Katika Makabila ya Tanzania Wachaga ndo wamekwenda shule kuliko makabila mengine na ndio maana utakuta wako kwenye Taasisi nyingi za Serikali na wengine wana Makampuni yao kama huyu SKOL.Kama unataka kujua Wachaga ni watu tofauti angalia LEGACY aliyoiacha Mzee Mengi!
Alafu huyo boya utakuta hpo alipo hana hata laki 2 lkn anabakia kumponda masawe

Ova
 
Mchaga hata ukimkuta anapalilia mahindi usimchukulie poa, ukifika kwake utaulizia mwenye nyumba kumbe ndiye mmiliki
Huyo anauwezo wa kukulisha ww na familia yko mpk mseme inatosha!
Usimchukulie poa

Ova
 
Just imagine, yaani mkandarasi anasemwa na waziri kwa kuchelewesha kazi hadi mkandarasi anazimia kabisa, huu si uuaji jamani? Na ni udhalilishaji pia, hayo ni maoni yangu. Angalia video hapo mwishoni kabisa.
---


Mkurugenzi wa kampuni ya SCOL Building Contractors Limited Vicent Massawe, ameanguka na kuzirai mbele ya Waziri wa TAMISEMI, Selemani Jafo baada ya kubanwa kuhusu ucheleweshaji wa ujenzi wa barabara ya Martin Luther hadi Swaswa mjini Dodoma.

Tukio hilo limetokea jana Jumatano Desemba 4, 2019 baada ya Jafo kutembelea ujenzi wa barabara hiyo yenye urefu wa kilomita nane iliyotakiwa kukamilika Agosti lakini ukaongezwa muda hadi Oktoba, 2019. Alizirai baada ya kuelezwa na Jafo kuwa kusuasua kwake kutasababisha asipewe kazi nyingine za ujenzi wa barabara

======

Dodoma. Mkurugenzi wa kampuni ya Scol Building Contractors Limited ameanguka na kuzirai mbele ya Waziri wa Tamisemi, Selemani Jafo baada ya kubanwa kuhusu ucheleweshaji wa ujenzi wa barabara ya Martin Luther hadi Swaswa mjini Dodoma.

Tukio hilo limetokea leo Jumatano Desemba 4, 2019 baada ya Jafo kutembelea ujenzi wa barabara hiyo yenye urefu wa kilomita nane iliyotakiwa kukamilika Agosti lakini ukaongezwa muda hadi Oktoba, 2019. Alizirai baada ya kuelezwa na Jafo kuwa kusuasua kwake kutasababisha asipewe kazi nyingine za ujenzi wa barabara.

Kutokana na kuchelewa huko mkandarasi huyo amekatwa Sh80 milioni na Wakala wa Barabara za Vijijini na Mijini (Tarura).

Licha ya kujitetea kuwa wamejenga katika miradi mingi nchini ikiwemo katika jimbo la Kisarawe ambalo mbunge wake ni waziri huyo wa Tamisemi, waziri huyo alikataa na kubainisha kuwa uwezo wa kampuni hiyo ni mdogo.

Baada ya hoja hiyo kupanguliwa na Jafo, mkurugenzi huyo alijitetea kuwa anakwamishwa na upatikanaji wa malighafi.

“Si watu wengi wanaweza kutumia hii nyenzo, hili jiwe hili linatoka Lugoba, Sisi tunataka tufanye kazi nzuri,” alijitetea mkurugenzi huyo.

“Umeshatembelea kazi za wenzako ukafanya ulinganisho ,” amehoji Jafo na huku mkurugenzi huyo akikosa jibu.

Hali hiyo ilimfanya Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Dk Binilith Mahenge kusema inawezekana kuna kinachomfanya kuchelewesha kazi, ndio maana anashindwa kusema ukweli.

“Katika sehemu ambayo sina shaka na mkurugenzi wangu, mhandisi wa Mkoa wa Dodoma wala mkuu wangu wa Mkoa ni eneo hili la usimamizi wa miradi kwa sababu miradi inaenda vizuri sana,” amesema Jafo.

Jafo amesema katika mradi huo changamoto ipo kwa mkandarasi, akibainisha kuwa Dodoma wamejenga barabara nyingi zimekamilika katika muda mfupi.

“Injinia kuna miradi mingine mmempatia hapa Dodoma,” amehoji Jafo na kujibiwa kuwa hakuna miradi mingine aliyopewa.

Alitoa agizo kwa viongozi wa Dodoma kutompatia mradi mwingine mkandarasi huyo huku akitilia shaka kasi yake ndogo na ubora wa barabara.

Jafo aliagiza mkandarasi huyo kuendelea kukatwa fedha hadi kazi itakapokamilika, kwamba ujenzi wa barabara hiyo unatakiwa kukamilika Desemba 30, 2019.

“Hizo blablaa zako za kokoto zinatoka mbali na nini sitaki kuzisikia, wenzako wote wanatengeneza barabara wanatoa wapi. Labda huna mtaji. Wakazi wa hapa wameteseka sana na madimbwi ndio maana tukasema tuunganishe hii barabara,” amesema Jafo.

Waziri huyo amesema ikiwa mradi huo hautakamilika Desemba 30 atawapiga marufuku wataalam wake wote kumpa kazi nchini.

“Wewe unakuja hapa ndio injinia ama mkurugenzi mbona sikuelewi. Ikifika tarehe 30 kazi hii isipokamilika hamtapata kazi yoyote nchini,” amesema Jafo na ghafla mkurugenzi huyo akaishiwa nguvu na kuanguka na Jafo kumtaka asimame na kusisitiza kuhusu Serikali kutotaka kufanya kazi na Mkandarasi mbabaishaji.

Chanzo: Mwananchi

Huyu mkurungenzi kweli hakistahili kuoewa hii kazi....maneno ya kawaida kabisa hayo anazimia kweli🤣🤣🤣🤣🤣
 
Back
Top Bottom