Waziri Silaa atinga Kariakoo, asema jengo lililouzwa lina Waqfu uliosajiliwa wizarani. Amshauri mnunuzi akamalizane na aliyempa hela

Waziri Silaa atinga Kariakoo, asema jengo lililouzwa lina Waqfu uliosajiliwa wizarani. Amshauri mnunuzi akamalizane na aliyempa hela

Somo alilotoa mheshimiwa Jerry Silaa kwa dakika 45 katika clip na ushauri wake kuwa tukiwakuta wasimamizi wa mirathi walioteuliwa na wanafamilia, tuwatafute pia warithi halali walioandikwa ili tusinunue jengo lenye mgogoro, nyumba bila kuwashirikisha warithi wote halali ama sivyo tutaingia katika mchakato mrefu usiomalizika huku tayari tumetoa mamilioni ya fedha tukidhani msimamizi wa mirathi ana maamuzi yote :

Tukienda Mahakama Kuu masijala ndogo ya One Stop Judicial Center Temeke Dar es Salaam kuna mifano ya kesi nyingi za wasimamizi za mirathi n.k zinavyoamuliwa

SOMA ZAIDI KUTOKA LINK HII:
One Stop Judicial Center Temeke - TanzLII
 
Mkinga lazima adai bilioni kadhaa zake zirudishwe, waliouza kama walishatumbua zote, watazitapika.
Au jengo apewe aliyonunua kwa masharti hiyo flow iliyowekwa waqfu mkinga aahe kama palivyo

Ghorofa msingi wake ni kuhimili floor 10 kwenda juu, marehemu Mzee Aldini aliweza kujenga hizo floor 5.

Labda mfanyabiashara aliyenunua 'jengo' anaweza kupewa 'viwanja' juu ya ghorofa aendeleze floor tano zingine juu ya hilo jengo huku warithi na madrasa wakibakia na floor tano za chini zilizopo sasa.

Ila mchakato ni mrefu na pia pesa zaidi inatakiwa ili kumaliza mgogoro.
 
Msomi mwanasheria Jerry Silaa anasema kazi ya msimamizi wa mirathi ni tofauti na tunavyodhania kuwa kazi yake kuu ni kuuza mali nasi tunakimbilia kununua bila kwanza kutafakari kwa kina mazingira, na wasimamizi wengi hujivika jukumu hilo bila kujua ni tatizo kubwa kisheria.
Kwa hiyo kumbe,wasimamizi wengi wa mirathi,hutumia dhuluma kuuza nyumba za mirathi bila kuwashirikisha warithi wote.
 
Msomi mwanasheria Jerry Silaa anasema kazi ya msimamizi wa mirathi ni tofauti na tunavyodhania kuwa kazi yake kuu ni kuuza mali nasi tunakimbilia kununua bila kwanza kutafakari kwa kina mazingira, na wasimamizi wengi hujivika jukumu hilo bila kujua ni tatizo kubwa kisheria.
Ndio inavyosemwa mitaani,na pia mawakili wengi wanawaambia wasimamizi wa mirathi kuwa unaweza kuuza chochote cha mirathi bila kustakiwa,kuuza shamba,viwanja nyumba,nk.
 
Hongera Kwa Waziri kutatua mgogoro huo.

Kununua Mali ya urithi huwa na changamoto nyingi hasa kama ndugu wengine wanakuwa hawajaridhia.

Nimewahi kupata shida ya hivyo, bila kutumia connection nilikuwa napoteza hela yangu hivi hivi 🙌
Kauli ya waziri siyo sheria, aende mahakamani kudai haki.
 
Aldini family ni familia fulani ya watoto wa mjini mjini yaani janja janja sana kiasi kuwa bado sina imani na hayo madai nahisi mkinga wa watu anaweza kuwa anaigiziwa move asiyoijua .
Hela yake mkinga kulipwa ni majaliwa ila kwa mkono wa chuma akisimama imara watalipa .
Note :watoto wa mjini tunaogopa uchawi sana .
Mfungo mwema ndugu zangu katika imani.
 
Hao ndugu wote watata
Dada yao nae muhuni tu.
Mahakama iwagawanyishe mapema maana watalogana hapo hadi waishe.
 
Maamuzi ya waziri yana mushkeli
Kuna waliouza .Wana umiliki halal kwenye sehemu ya hilo jengo .Sababu walipewa mirathi. Uamuzi ulitakiwa kuwa hivi

Mosi Eneo la Madrasa libaki lilivyo
Pili waliouza hilo ghorofa wahesabike waneuza kihalali kwa mkinga maeneo yao waliyopewa na marehemu hizo floor zao.Zihesabike kuwa ni mali ya huyo mkinga.Sababu wameuza Chao.Na mkinga apewe hati za hizo units za hao waliouza sio wao wapewe kama waziri alivyoamua
Yule aligoma kuuza abaki na unit yake

Lakini kuchukulia kama mkinga hana chake sijui aende mahakamani sio sahihi.Yeye ni mumiliki halal wa units zote za hao warihi wenye units zao waliomuuzia.Waliogoma sio kesi wabaki na zao .Ila mkinga ndie apewe hati za umiliki wa hizo units za wauzaji
 
Mporipori mkinga kaingizwa jau.. hii imekula hadi ajae kuipata hiyo hela watakula wajukuu wake sio leo yaani
 
Mporipori mkinga kaingizwa jau.. hii imekula hadi ajae kuipata hiyo hela watakula wajukuu wake sio leo yaani
Hahitaji kulipwa pesa kuna wanaokubaki waliuza Achukue floor zao na fremu zao.Sababu hawakatai kuwa hawakuuza.Madrasa ibaki lakini msikiti ukiamua madrasa iende wapi uamuzi wao sababu ndio walikabidhiwa huo wakfu

Huyo dada yao ambaye anasema hakushirikishwa abaki na floor yake na fremu zake
 
kwenye watoto 11 sio huyo dada peke yake aliyekubali kuuza..Na wakfu ulishaandikwa sio suala la hiyari ya msikiti ni la lazima ubaki kama alivyoagiza marehemu.. Huyo Imam aliyeuza hata kamati ya msikiti wanamkana
 
Back
Top Bottom