Precious Diamond
JF-Expert Member
- Jun 9, 2023
- 593
- 1,376
Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Jerry Silaa amewataka waumini wa Kanisa la Kiinjili na Kilutheri Tanzania (KKKT) kuhakikisha wanamuombea Rais Samia katika kazi yake ya kuliongoza taifa.
Silaa ameyasema hayo leo Jumapili, Machi 31, 2024 alipofungua harambee ya kuchangia upanuzi wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT) Usharika wa Chanika jijini Dar es Salaam.
Kauli yake hiyo inatokana na kile alichoeleza, Rais Samia alishiriki sherehe za kumsimika Mkuu wa KKKT, Dkt. Alex Malasusa, hatua ambayo inathibitisha upendo wa mkuu huyo wa nchi kwa waumini wa kanisa hilo.
"Nawaomba sana washarika wenzangu tumuombee Rais wetu, Mungu ampe nguvu, hekima na busara ya kuliongoza taifa letu. Nakuomba ufikishe salamu zangu kwa Baba Askofu na washarika wenzangu, kutumia Pasaka, maombi na Ibada zetu kumuombea Rais wetu, Samia Suluhu Hassan," amesema.
Jambo TV