Waziri Simbachawene amwagiza IGP kuwapangia kazi nyingine matrafiki wenye vitambi. Je, ni kosa askari kuwa na kitambi?

Waziri Simbachawene amwagiza IGP kuwapangia kazi nyingine matrafiki wenye vitambi. Je, ni kosa askari kuwa na kitambi?

Hizi amri za wanasiasa ndio ufanya jeshi kudharaulika.
Jeshi kudharaulika kisa kuwaambia wenye vitambi wasikae site? Huoni kama kumkuta askari ana mtambi kama zigo la mwizi anaongoza magari hiyo ndio kulitia aibu jeshi! Kumbuka hawajafukuzwa kazi bali kasema kasema wasikae site. Askari na kitambi wapi na wapi? Kitambie mwenzie mwanasiasa.
 
Jeshi kudharaulika kisa kuwaambia wenye vitambi wasikae site? Huoni kama kumkuta askari ana mtambi kama zigo la mwizi anaongoza magari hiyo ndio kulitia aibu jeshi! Kumbuka hawajafukuzwa kazi bali kasema kasema wasikae site. Askari na kitambi wapi na wapi? Kitambie mwenzie mwanasiasa.
Kwani wao sio watu, kitambi ni ziada ya mafuta sababu ya ulaji mbovu.
 
Yaani katika mambo ya msingi anayotakiwa atekeleze na asemee na hili nalo lipo kichwan kwa wazir mwenye mambo mengi na ya msingi yakufanya.!! Taa nyekundu imeanza kuwaka.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Watu wanapimwa na performance base na sio kitambi. Hawa viongozi bwana hata kama kutafuta kiki sio kwa hivi.
 
Kwani wao sio watu,kitambi ni ziada ya mafuta sababu ya ulaji mbovu.
Wao ni watu lkn kulingana na kazi yao waliojichagulia hawapaswi kuwa na vitambi. Na kwanini uwe na ulaji mbovu wenye kusababisha mafuta ya ziada yasiyohitajika ikiwa wewe ni askari? Askari hapaswi kuwa na kitambii ataclow vipi vitani na mtambi ka zigo la mwizi?
 
Kuna wengine mabonge wapo makao makuu ya trafiki mule ndani nazani idara ya uhasibu pale wanakalibua kupasuka. JWTZ waliliona hili wakaanzisha program ya mazoezi.
 
Kitambi ni ishara ya uzembe, tamaa, maradhi, unadhilifu. ASKARI KUA NA KITAMBI NI DHARAU
 
Askari wa JWTZ huwezi kuwakuta wameoasuka hivyo mana wenyewe wanaelewa nini kinatokea ukutwe umejaza mavi tumboni kizembe zembe kama raia inakuaje?
 
Hata yule mlinzi wa rais mwenye kitambi ananikera sana, haonyeshi picha nzuri kabisa anadhalilisha nchi.
 
Waafrika tuna asili ya unene...aache ujinga. Mimi nilipokuwa chini ya miaka 30 nilikuwa nawacheka sana watu wenye vitambi...nilikuwa nawaita manyama uzembe.

Ila sasa kitambi changu karibia kinagusa chini, GYM zote nimemaliza hadi yale madawa ya Forever Living yanaitwa C9.

Kama hayajakukuta shukuru Mungu!

Sent using Jamii Forums mobile app

Si Waafrika wote ni wanene May be kama unazungunzia majority of bantus maana hawa wengi ni wanene na wafupi. Ila cushites na nilotes wengi ni warefu wembamba.
 
Ndio namsikia sasa akitoa maelekezo

kIongOzI Wa BaaDae
 
Waziri wa Mambo ya Ndani ya nchini, Geogre Simbachawene, amemuagiza Mkuu wa Jeshi la Polisi, IGP Simon Sirro, kuwaondoa askari wote wa Usalama Barabarani wenye vitambi na kuwapangia kazi nyingine kwani wamekosa sifa.

Chanzo: Serengeti Post

Halafu Mawaziri wa Tanzania wakiwa Wanadharaulika 24/7 na kuonekana ni Kero na Mizigo kwa aliyewatea wanaona wanaonewa.
 
Back
Top Bottom