Waziri Simbachawene: Huwezi kumchukua aliyepata divisheni 1 ili akalinde benki au kucheza gwaride, lazima muelewe jamani

Hawakubali maelekezo ya kikuda
 
Ndo maana hawa watu wanamataumizi ya nguvu kuliko akili wengi pia wanatumia sigara kubwa! Yaani dunia inahitaji intellijentsia kubwa unajazavilaza wasiojitambua jeshini!
 
Hawa kwa kawaida hawa-dili moja kwa moja na raia; wana profesheni zao maofisini. Vilaza aliomaanisha Mh. Waziri ndio wanatekeleza core functions za jeshi la polisi - ulinzi wa raia na mali zao; kukamata, kupeleleza, na kutoa ushahidi mahakamani hufanywa na vilaza badala ya cream!
 
Jibu limetolewa japo linauma kwa polisi lakini ndo hivyo mjue kuwa mnaajiriwa polisi kwa vile mmefeli ili mkatumie maguvu badala ya akili. Mana akili nyie hamna mmefeli. Wapi Kingai? Naomba niende maliwato naulizwa maswali magumu.
 
Kama ni hivyo majukumu ya kukamata na kushitaki mwaondoshee kwani yapo juu ya uwezo wao, mtafute watu sahihi wakufanya hayo🏋️.
 
Kwa hiyo jeshi la Polisi Tz linajivunia kuwaajiri watu wenye elimu duni huku likiwaacha kimakusudi watu wenye ufaulu mzuri?!

Huu ni uwendawazimu.
 
ni kweli kabisa maana PGO itamuongoza na kuwa askari mzuri kwa jamii sio kwa ccm
 
Kwa nchi makini Simbachawene kufikia asubuhi ya kesho hakupaswa kuendelea kuwa ofisini
Huo mdomo utampoza,nadhani atakuja kukanusha kuwa hakusema hivyo kwenye luninga, kajikaanga kwa mafuta yake mwenyewe
 
Kwa hiyo jeshi la Polisi Tz linajivunia kuwaajiri watu wenye elimu duni huku likiwaacha kimakusudi watu wenye ufaulu mzuri?!

Huu ni uwendawazimu.
Kumbe ndo maana hata waziri wakapewa mwenye elimu ya kuunga unga ili wakaongee lugha moja......
 

Waziri amejibu ki-lay man. Iko hivi;
Kazi za kijeshi huwa zina discipline Fulani ya kuziendea, hapo Uhamiaji wamejitahidi,ufaulu huo wa div 4 walioanzia,kwa Polisi ulikuwa unakunyima sifa,unakuwa umefaulu mno! Katika shughuli za kiulinzi kuna ngazi ya chini kabisa PC,Wdr/Wdrs, sijui constable wa Uhamiaji anaitwaje,na wa Zimamoto, Hawa ndio watendaji wakuu wa Kazi. Na strength imeshaprovide ili triangle ikubali, base pana, vyeo Vya kati slim kidogo kadri vinavyopanda na Vya Juu wachache kabisa.Ktk uajiri hapo wameshatengeneza hesabu ya kufiti mfumo! Hao degree holders Ni candidates wa kuwa maafisa in near feature, form six watakuwa NCOs ( non commissioned officers) hao rafiki zangu ndio watakuwa wawajibikaji wakuu.I can tell you kama wangekuwa na jinsi ya kupata std 7, wangemchukua
(1) nidhamu kazini
(2) muda mrefu zaidi wa kumtumia Ktk level za kiulinzi ambayo ndio INA hitaji watu wengi.kwa maksi zao mpaka wafike Juu kwa mtiririko wa kuanzia, cert( pengine aanzie Ku re sit)mpaka afike kuvuruga matarajio sio Leo.
 
Point yake angeweza kuiweka vizuri zaidi

Waliofaulu zaidi wana demand zaidi hivyo hawakai wanahama hama (retention yao ni ngumu)

Hawa wengine choice ni ndogo hivyo wanadumu na kuwaajiri kuna uhakika wa kudumu nao...

Ni kwamba ajira tu zimekosekana Sio zamani sana watu ilikuwa kuchagua ualimu, polisi, jeshi nesi ilikuwa ni chagua la mwisho (Ni kwamba mambo yamebadilika demand ni kubwa kuliko supply) hata kazi ambayo haiitaji degree mtu ananganganiza kwanini wasimchukue yeye mwenye degree (anasahau kwamba kuna aspects nyingine huenda asiye na degree anamzidi) Yupo over qualified...
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…