Waziri Simbachawene: Huwezi kumchukua aliyepata divisheni 1 ili akalinde benki au kucheza gwaride, lazima muelewe jamani

Undata niliukataaga katukatu. Sijawahi jutia kukataa ugali kwa mfumo wa kuwa afande.
 
Maana yake jeshi la polisi limeundwa na vilaza.

Siro na vijana wako mpo? Waziri kasema sifa ya kujiunga na jeshi la polisi lazima mtu awe kilaza.
Kuna misukule tukiandika humu kuwa TanPol ndio jeshi la vilaza kuliko majeshi yote,wanatupinga,haya leo bosi wa TanPol kadhihirisha wazi kuwa sifa kuu ya kujiunga na TanPol ni "ukilaza".
 
Ndio maana taarifa zao za Kiintelejensia huwa zina walakini....
TanPol neno "intelijensia" lipo kinyume chake.
Intelijensia yao eti inaonyesha Mbowe anafadhili ugaidi kwa laki sita!!
 
Weka hapa tusikilize wenyewe.
 
Amekosea sana....kwa hiyo amepigia mstari kauli za watu kuwa jeshi la polisi ni kwa ajili ya watu wenye uwezo mdogo...poor him...
Amewadhalilisha sana polisi sijui kama analijua hili...
Poleni PT.

Asijue jeshi la Polisi ni kuanzia Constable mpaka maafisa wengine wote wa vyeo vya juu hadi IGP anao rub shoulders nao kila uchao kwenye corridos za ofisi za Wizara ya Mambo ya Ndani.
 
😍
 
Angesema jeshi la polisi linaajili viwango vyote vya elimu bila kubagua angeeleweka zaidi kuliko hivyo alivyosema naona huyu soon atawekwa pembeni.
 
Mbona kafafanua vzr tu. Kwa sasa hawataki division ya point za juu.

Wanaotakiwa kwa sasa ni washika mitutu benki.

Wakihitaji wale wa maarifa wataajiri siku zinazo.

Au mimi naelewa vibaya.

Mfano, wewe ukitaka Mfanyakazi wa ndani, ungependa awe na division one and so on..., Au degree!!?
 
Kwa marekani huwezi kuwa General wa jeshi bila kuwa na Masters degree, in fact General David Patreaus aliyeikomboa Iraki kutoka kwenye vita ya wenyewe kwa wenyewei iliyokuwa imeanza kuibuka lakini akakumbwa na kashfa ya ngono ana Ph.D. yule kamanda. Askari wa marekani ni wasomi sana. Kuna mwanafunzi wangu mmoja aligraduate miaka kumi iliyopita akaniomba nimuandikiea barua ya reference kwenda graduate school, sasa hivi ni Brigadier General na kamanda wa special operations huko Arizona- hua tunawasiliana mara kwa mara kila anapohama au kupanda cheo hunitumia message.
 
Lakini kuna kaukweli hapo, ningekuwa Raisi ningemtumbua haraka sana, Waziri hatakiwi kudharau kazi za watu tena police ni wafanyakazi wa umma, ajiuzuru na awaombe polisi msamaha
 
Haohao kesho watakuwa IGP ndiyo maana PGO haipandi
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…