Waziri Simbachawene jiuzulu, una-underperfom. Ajali zitamaliza Watanzania

Waziri Simbachawene jiuzulu, una-underperfom. Ajali zitamaliza Watanzania

Rasterman

JF-Expert Member
Joined
Feb 24, 2015
Posts
33,894
Reaction score
44,117
Habari za asubuhi wana JamiiForums

Kwa maslahi ya taifa naona tujadili hili swala. Naona halizungumzwi mahali popote ukiachilia matatizo mengi tuliyonayo kama taifa kwa sasa.

Kumezuka tatizo la ajali za kila mahala takribani ajali 4-5 kwa siku zinaripotiwa kwenye mitandao ya kijamii zikihusisha vyombo vya usafiri wa abiria kama Mabasi yaendayo mikoani.

Pamoja na kuwa usafiri na usimamizi wake uko chini ya Wizara ya mambo ndani hatuoni hatua yoyote inayochukuliwa na Waziri mwenye dhamana Mh Simbachawene. Sio tu kuchukua hatua bali hata kulizungumzia tu yuko kimya.

Kwa maoni yangu na jinsi navyoona ripoti hizi naweza kusema baada ya vifo vya corona Ajali tanzania inashika namba mbili.

Tusifanye siasa kwenye maisha ya watu. Mh Rais anakopa pesa kila siku zije nchini kusaidia watanzania sasa kama watanzania wanateketea kwa ajli kila siku huku wengi wakiachwa na ulemavu wa kudumu itakuwa haina maana.

Utendaji wa Mh Simbachaweni uko chini ya kiwango kuliko hata wa Kangi Lugola.
 
Takwimu za nani au wapi zinaonesha Covid-19 inaongoza kwa vifo Tanzania?
 
Kwani waziri ni dereva wa hayo magari yanayopata ajali?
Duuuuuuuuui.....hili jibu hata mtoto wangu DEUS wa darasa la awali hawezi kujibu hv, kwamba hujui jeshi la polisi Hasa trafiki Ndio wanatakiwa kusimamia usalama barabarani? Na kwamba Hao WOTE wapo chini ya wizara ya Mambo ya ndani ambayo Boss wao Ndio huyo waziri mtajwa? Halafu utakuta na wewe Ni kiongozi sehemu.
 
Amejibu kisiasa. Anapenda siasa
 
Back
Top Bottom