Waziri Simbachawene: Wanaomchafua Rais Samia mitandaoni watafutwe na kufikishwa Mahakamani

Waziri Simbachawene: Wanaomchafua Rais Samia mitandaoni watafutwe na kufikishwa Mahakamani

mshale21

JF-Expert Member
Joined
Apr 8, 2021
Posts
2,126
Reaction score
5,068
Waziri wa Mambo ya Ndani ya nchi Mhe. George Simbachawene, ameelekeza vyombo vyote vya ulinzi na usalama nchini kuwatafuta watu wote wanaowachafua wenzao mitandaoni hasa wanaomdhihaki Rais wa Tanzania na Serikali na hatua kali zifuatwe na kuwafikisha mahakamani kwa haraka.

Waziri Simbachawene ameyasema hayo mapema leo Alhamisi Jijini Dodoma wakati akizungumza na viongozi wa idara zote za ulinzi na usalama nchini ambapo ameelekeza kufanyike msako wa haraka kuwabaini watu hao na kuwakamata kwakua kumeibuka tabia ya watu kutumia vibaya mitandaoni hiyo kwa kisingizio cha uhuru wa kujieleza.

Katika hatua nyingine Waziri Simbachawene ameagiza msako wa wezi mitandaoni kwa kuwa inakadiriwa kuwa kwa siku milioni 500 zinakua kwenye wizi wa kimatandao huku akikataza wananchi kutoa fedha kwa ajili yakufuatilia polisi taarifa za simu zao zilizoibiwa.

 
Wachumia matumbo wa mitandaoni watakuja na matusi yao ya mafumbo kumkejeli Waziri husika wa hii mada.
 
Hebu angalieni hio tv hapo pichani muone Ni Nani alikua anaongea hapo kideoni.
 
😁😁😁
1631782898_1631782897-picsay.jpg
 
Anajichafua mwenyewe, asitafute visingizio.
Tuleteeni wasomi wa IVY legue, hawa wa UDSM hamna kitu. Wamebaki kujihami kwa nguvu ya dola.
 
Back
Top Bottom