Waziri Simbachawene: Wanaomchafua Rais Samia mitandaoni watafutwe na kufikishwa Mahakamani

Waziri Simbachawene: Wanaomchafua Rais Samia mitandaoni watafutwe na kufikishwa Mahakamani

CCM wanaanza kutafutana wenyewe kwa wenyewe. Maneno ya Tundu Lissu yanatimia, watawala dhalimu wagandamizi wa haki wakimalizana na sisi wapinzani watahamia kuwasaka wenziwao ndani CCM.
 
Kukamata watu kwa kutoa maoni yao? tunarudi kwenye ukoloni na udikteta uchwara...
 
Michango ya kuwatoa watakaokamatwa itapitishwa kwenye mitandao ya kijamii .
 
Mtaani watu wanasemana vibaya leo kwenye mitandao..

Walitukanwa akina mwinyi, mkapa, kikwete, magufuli washindwe huyu!
Viongozi wajikite zaidi kutatua changamoto zinazo ikabili jamii yao!

Ubunifu wa kuongoza hasa kipindi hiki cha utandawazi utawafanya wawe viongozi bora na sio bora kiongozi.
 
Matusi ata mm naunga mkono wakamatwe tu.
Kejeri hapa kidogo kuna kaugumu maana nyingine huwa sio kejeri bali ukosoaji/utoaji maoni unaokuja kwa njia ya utani(hii kutokana na uoga wa kujieleza direct kwa mhusika)
 
Huo ndio upuuzi tusiotaka kuusikia

Watangaze kwanza nchii hii ni ya kidekta ya kikomunisti sio ya kidemokrasia


Then tuendelee kuanzia hapo

Mnarudi makosa yale Yale ya kutukuza watu kupitiliza Hadi wanafikia stage kudhurumu haki za watu kuishi

Hii sio sawa na hatutokubali
 
Kwahiyo wataanza kuscan mitandao yote kuwatafuta watz au maana kuna watz wanatukanwa na wasomali mtandaoni
 
Kwanini ahangaike kutafuta wa mitandaoni wakati wapo kina Polepole na Gwajima wanaomchafua rais na kumpinga hadharani.
Tunarudi kulekule, raisi anapaswa kuhangaika kukuza uchumi.na sio kuhangaika na wanaomkosoa
 
Waziri wa Mambo ya Ndani ya nchi Mhe. George Simbachawene, ameelekeza vyombo vyote vya ulinzi na usalama nchini kuwatafuta watu wote wanaowachafua wenzao mitandaoni hasa wanaomdhihaki Rais wa Tanzania na Serikali na hatua kali zifuatwe na kuwafikisha mahakamani kwa haraka.

Waziri Simbachawene ameyasema hayo mapema leo Alhamisi Jijini Dodoma wakati akizungumza na viongozi wa idara zote za ulinzi na usalama nchini ambapo ameelekeza kufanyike msako wa haraka kuwabaini watu hao na kuwakamata kwakua kumeibuka tabia ya watu kutumia vibaya mitandaoni hiyo kwa kisingizio cha uhuru wa kujieleza.

Katika hatua nyingine Waziri Simbachawene ameagiza msako wa wezi mitandaoni kwa kuwa inakadiriwa kuwa kwa siku milioni 500 zinakua kwenye wizi wa kimatandao huku akikataza wananchi kutoa fedha kwa ajili yakufuatilia polisi taarifa za simu zao zilizoibiwa.

View attachment 1940215
Rais Samia Suluhu akiwa na Waziri Simbachawene.
Gwajiboy mmeshamkamata?
 
Back
Top Bottom