Waziri Simbachawene: Wanaomchafua Rais Samia mitandaoni watafutwe na kufikishwa Mahakamani

Mitandaoni! Ina maana hata simu za mkononi? Mbona waliomchafua JPM kwa njia ya simu baadaye wanaanza kupewa uwaziri?
 
Nadhani Mama alishasema akosolewe kwa staha. Sidhani kama kuna mtu kamtusi mama, ila naona Mh. Simbachawene anaona reshuffles inanukia.
 
Na wanaomchafua Mbowe kuwa gaidi wao wasifiwe natuzo wapewe!!

*Kweli naomba niende hajandogo kwanza (in kiungai's voice)
#uongoaibu
 
Hakuna haja. Hiyo nguvu bora vyoo vya magereza viboreshwe kwa ajili ya vizazi vijavyo.
 
Hamtokubali wewe na Nani?
 
Vyombo vyote? Amepata wapi hayo mamlaka ya kuamuru vyombo vyote

Sent from my SM-A207F using JamiiForums mobile app
 
Waanze na Polepole, Gwajiboy na Ndugai. Hao wanamponda mama yetu waziwazi bila kificho.
 
Ngoja tuwaache kwanza ili niwape ujumbe huu.Heshimuni Mamlaka iliyopo kwani yatoka kwa Mungu!.
 
Facebook kuna watu hadi walikua wana mtukania maumbile yake mi nadhani sio sawa, uhuru wa kujieleza lazima uwe na mipaka.
Yeye mwenyewe aliwatukana wachezaji wa kike wa mpira wa miguu kuwa wana vifua flat! Anajidai kwa kuwa na mzigo wa maziwa kifuani!
 
Yeye mwenyewe aliwatukana wachezaji wa kike wa mpira wa miguu kuwa wana vifua flat! Anajidai kwa kuwa na mzigo wa maziwa kifuani!
Kama una weza kumuambia mama yako hivo basi sawa. Ila ile hotuba nadhani watu hawakusikiliza vizuri kupata context, na vyombo vya habari vili potosha. Simtetei mama ila tue na heshima na tujibishane kwa hoja na kuheshimiana.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…