Waziri Simbachawene: Watanzania fanyeni kazi na mtafute pesa. Maisha sio Magumu

Acha uwaziri kama maisha ni rahisi. Nimeamini wajinga ni wengi katika baraza la cuba.
 
Boniface Simbachawene amewachana live watu waache visingizio na watafute pesa kwa kufanya kazi zaidi kwani maisha sio magumu Bali mahitaji ya pesa yameongezeka.

My Take
Watu waambiwe ukweli hakuna kupakwa mafuta Kwa mgongo wa chupa.😂😂

=====

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe.George Simbachawene amewataka wananchi kufanya kazi kwa bidii ili kujiingizia kipato cha kuweza kumudu gharama za maisha.

Amesema ni wajibu wa kila mmoja kwa nafasi yake kufanya kazi kwa bidii ili aweze kupata fedha za kumuwezesha kumudu huduma muhimu katika jamii.

Mhe. Simbachawene ametoa wito huo wakati akizungumza na wananchi wa Kata ya Mbuga iliyopo katika Jimbo la Kibakwe, Wilaya ya Mpwapwa mkoani Dodoma, ikiwa ni ziara yake ya kikazi ya kuzungumza na kusikiliza changamoto zinazowakabili wananchi wa jimbo lake.

"Ukiwa huna fedha ikitokea umeumwa, utashindwa kupata matibabu na kuweza kuhatarisha uhai wako, hivyo ni bora kila mmoja wetu akahakikisha anafanya kazi ili apate fedha za kumudu mahitaji muhimu," amesema Waziri Simbachawene.

Amesema kila mwananchi kwa nafasi yake ni muhimu akahakikisha anajikita katika kuzalisha mali ili aweze kupata fedha.

Amefafanua kuwa hakuna maisha magumu kama inavyodaiwa na watu wengi isipokuwa mahitaji ya fedha yameongezeka kutokana na kukua kwa maendeleo.

Kufuatia hatua hiyo, Mhe. Simbachawene amewataka wananchi hao kuacha tabia ya kukaa bila kufanya kazi badala yake waitumie ardhi yenye rutuba waliyojaaliwa kuwa nayo kwa ajili ya shughuli za kilimo ili waweze kujikwamua kiuchumi.

Chanzo: EA Radio
Amelewa??
 
Yeye anafanya kazi gani ?!!!

Yeye angefanya kazi yake vema tunayomlipa kwa Kodi zetu yeye na wenzake wangekuja na Sera za watu kupata Ujira kwa kufanya shughuli na hivyo wanachopata (income) kingeendana na matumizi kuongezeka....

Hivi yeye anadhani amekaa hapo ili afanye kitu gani ? Kuleta hizi Porojo ?
 
Kazi nyingi zinategemea umeme wa uhakika mfano vinyozi unawakatia umeme kwa masaa 12 wafanyeje kazi ndugu Waziri?
 
Ye kawekeza sana kwenye mabar
Hongera zake

Ova
 
Sa100 amefanya mawaziri wake wote wameshiba hadi wamevimbiwa...ni mwendo wa kuja..mba tu ptuu ptuu ptuuuuuu.
 
Boniface Simbachawene amewachana live watu waache visingizio na watafute pesa kwa kufanya kazi zaidi kwani maisha sio magumu Bali mahitaji ya pesa yameongezeka.

My Take
Watu waambiwe ukweli hakuna kupakwa mafuta Kwa mgongo wa chupa.😂😂

=====

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe.George Simbachawene amewataka wananchi kufanya kazi kwa bidii ili kujiingizia kipato cha kuweza kumudu gharama za maisha.

Amesema ni wajibu wa kila mmoja kwa nafasi yake kufanya kazi kwa bidii ili aweze kupata fedha za kumuwezesha kumudu huduma muhimu katika jamii.

Mhe. Simbachawene ametoa wito huo wakati akizungumza na wananchi wa Kata ya Mbuga iliyopo katika Jimbo la Kibakwe, Wilaya ya Mpwapwa mkoani Dodoma, ikiwa ni ziara yake ya kikazi ya kuzungumza na kusikiliza changamoto zinazowakabili wananchi wa jimbo lake.

"Ukiwa huna fedha ikitokea umeumwa, utashindwa kupata matibabu na kuweza kuhatarisha uhai wako, hivyo ni bora kila mmoja wetu akahakikisha anafanya kazi ili apate fedha za kumudu mahitaji muhimu," amesema Waziri Simbachawene.

Amesema kila mwananchi kwa nafasi yake ni muhimu akahakikisha anajikita katika kuzalisha mali ili aweze kupata fedha.

Amefafanua kuwa hakuna maisha magumu kama inavyodaiwa na watu wengi isipokuwa mahitaji ya fedha yameongezeka kutokana na kukua kwa maendeleo.

Kufuatia hatua hiyo, Mhe. Simbachawene amewataka wananchi hao kuacha tabia ya kukaa bila kufanya kazi badala yake waitumie ardhi yenye rutuba waliyojaaliwa kuwa nayo kwa ajili ya shughuli za kilimo ili waweze kujikwamua kiuchumi.

Chanzo: EA Radio
Ardhi IPO mvua au irrigation Iko watu tulime
 
Simbachawene Ni mjinga snaa waziri asiyetambua changamoto zinazo wakabili vijan umeme hkn unategemea nn kwa wafetua tofali na welding ?
 
Back
Top Bottom