- Lets cut the chase hapa, Sophia hajawahi kuwa mke wa Idd Simba, never! na wala sio Mu-Islam, Sophia ni Mkatoliki na amekua girlfriend wa Kitwana Kondo kwa muda mrefu sana lakini sio mkewe wa ndoa, na amefikia hata kuzaa naye watoto, mmoja wao yupo jela kwa muda mrefu sana kule Carlifornia. Sophia amesoma sheria Mlimani wakati mmoja na muungwana, na Lowassa.
- Connection yake kwenye power na hasa na muungwana, inakuja through Kitwana Kondo former meya wa Dar na mbunge wa zamani Kigamboni, a very influencial man toka hata wakati wa Mwalimu kutokana na his knowhow na ishus za Waisilamu, hasa jijini Dar. Yeye ndiye the go to guy kwa marais wote since Mwalimu, kwenye kuzima na kuziwahi ishus tata za Wa-Isilamu mjini Dar, hasa kwenye kuzima maandamano na utata wa never ending kwenye Bakwata.
- Kwenye huu uchaguzi kumetokea ishus nyingi sana ambazo zinatatanisha sana, kwa mfano in public Muungwana hakuwa mkweli na exactly nani aliyemtaka hapa kushinda, lakini kumbe it was very clear in private aliyemtaka ni Sophia, Mafisadi fearing the public blacklash kama ya uchaguzi wa Uv-CCM na wao pia wamecheza un-ugly game ya kutoa signal kwa wahusika wengi wa uchaguzi kuwa wanam-support Mama Janet, huku wakimpa Sophia kitita cha hela zisizo na mfano kwa siri ili kushinda. At one point during uchaguzi jana, hela zilikuwa zinagawiwa openly huku maa-agent wa idara wakiwazuia watoa hela wa Mama Janet na kuruhusu wa Sophia tu kutoa mapesa hayo ya rushwa, sasa the small picture hapa ni kwamba kwenye vita vya ufisadi, tumepiga hatua mbili nyuma.
- Lakini the big picture ni je Muungwana ameamua kurudi tena kwa marafiki zake, yaani mafisadi? Na je aliwahi kuachana nao for real? I mean sio siri kua hapa wote wamemsaidia mgombea mmoja, sasa was it co-ordinated au ilikuwa kila mmoja ki-vyake? Huu uchaguzi ni kama zile chaguzi mbili za huko nyuma kuelekea kwenye uchaguzi wa mwisho wa rais, yaani Nchimbi na UV-CCM na mwenyekiti wa CCM mkoa wa Dodoma, ambapo ndipo hasa mafisadi walipoanza kuonyesha makucha yao rasmi kama vile huu uchaguzi wa jana uwt. Huu uchaguzi sasa sio siri tena kuwa ulikuwa ni agenda ya urais 2010 na pia 2015 na the number one looser jana alikuwa ni Membe, namba mbili ni lile kundi la wapiganaji kina Mwakyembe na the likes, namba tatu mpiganaji Mengi, nne ni sisi wananchi ambao tumekuwa mstari wa mbele sana baada ya kutiwa nguvu na uchaguzi wa UV-CCM, ingawa kwa wanaomjua vizuri Muungwana wanasema this is him kumridhisha kila mtu na kuendeleza popularity yake, maana nasikia aliposema tu anataka mgombea msomi meaning Sophia, basi uchaguzi ukaisha pale pale na infact ilikuwa ni marudio ya maneno ya Mkapa kwenye uchaguzi wa rais uliopita, tuchague rais kijana.
- Walioshinda jana tena big time ni Lowassa, Mkapa, Makamba, Nchimbi, na hasa Masha, maana sasa the hope is back tena na urais. Uchaguzi huu wa UWT unaweka pabaya sana ile operation Kisutu I mean itaenda vipi forward wakati waziri wa utawala bora yaani TAKUKURU na Usalama, anapohusika kwenye this very ugly rushwa na the very abuse of power?
- I mean talking about abuse of power ya kina Mramba na yona mbona wanakuwa cha mtoto kulinganisha na what waziri wetu did here, tena akiwa na support ya rais na hizi instituion mbili muhimu za dola tunazoziaminia kwenye vita ya kusafisha mafisadi? Unajua nitawashangaa sana wanaopelekwa Kisutu, kama hawata cite ishus kama hizi za abuse of power kwenye huu uchaguzi katika kujitetea kwao against serikali, kwa sababu serikali inapata wapi hapa moral na legal authority kuwa-prosecute on abuse of power wakati na wao wanafanya hayo hayo na hasa kwenye huu uchaguzi? Sisemi kwamba sasa kina Mramba wawe off the hook, no way hao bado tunakomaa nao tu mpaka kieleweke lakini hapa serikali imetuchanganya kama haikujichanganya yenyewe.
- Again, kama demokrasia inavyotaka tunamtakia heri Auntie Sophia na ushindi wake, lakini hivi ni kweli the end in this uchaguzi unaweza uka-justify the means? Na ni under nani's expense? Wote wawili Auntie Sophia na Mama Janet, hawakufaa kuruhusiwa kugombea huu uchaguzi, kwa sababu wametumia rushwa kubwa sana tena isiyo mfano kwa nafasi ndogo sana ya uwt, sasa urais ujao itakuwaje?
Mungu Ibariki Tanzania.