Masanilo
Platinum Member
- Oct 2, 2007
- 22,286
- 4,523
Kwani Anna Abdalla wakati wa Mkapa alipata wapi muda wa kuwa mbunge, waziri wa afya na M/kiti UWT?. Only in TZ is possible wenzetu wenye wito wa huduma huamua kujiuzulu nafasi nyingine na kubakia na mota ili awe effective, ila kwa bongo nafasi hizi ni ulaji na si huduma hata hamsini mtu anazimudi si ni kuhudhuria vikao tu nani atashindwa?.
Kujilimbikizia madaraka ni moja ya dalili ya umasikini wa demokrasia, angalia raisi alivyo na madaraka mengi? Kuna kipindi Makamba alikuwa Mbunge, Katibu wa CCM, Mkuu wa Mkoa, Mwenyekiti wa usalama bara barani, kamanda wa ulinzi na usalama...na vyeo vingine vingi, si kwamba yeye ni mtendaji mzuri kuliko wengine walioyopo bali ni ujinga wa kulewa madaraka na kubeza demokrasia, ukiangalia utendaji ni hakuna kitu. Sasa mh Sophia Simba, ni Mbunge, waziri na sasa mkiti wa wanawake wa CCM Tanzania? Mtu huyu huyu aliyeshindwa kumudu uwaziri leo hii anaongezewa majukumu mengine hivi hakuna mwanamke mwingine mwenye uwezo zaidi yake? Hata kama hawakujitokeza kugombea basi raisi ampunguzie madaraka ya uwaziri ili aweze kuwatumikia vyema huko UWT-CCM
Kaaazi kweli kweli...
Ushi