Waziri Sophia Simba - Mwenyekiti Mpya UW-CCM (Taifa)

Waziri Sophia Simba - Mwenyekiti Mpya UW-CCM (Taifa)

1. Haya ndio baadhi ya matatizo aliyotuachia Mkapa, alipoamua kwa ubabe kuwa mwenyekiti wa UWT na katibu wake wawe wabunge automatically ili kumuokoa rafiki wa kusini mwenziwe Mama Anna Abdallah, ambaye alishajua mapema kua hawezi shinda ubunge kwenye jimbo tena,

- kule kwenye ubunge kuna dola $ 30,000 kila baada ya miaka mitano na shangingi moja la bure kila five years, toka Mkapa alete huu ubabe wake hizo nafasi mbili UWT zimekua mbinde tupu, na aibu kwa taifa licha ya CCM kama chama.

2. Now comes this, hawa wakina mama wawili inafahamika wazi ndani ya uongozi wa CCM na serikali on a national level, kwamba afya zao sio nzuri sana, infact ingekua majuu wasingekua viongozi wangetakiwa wapumzike pembeni na kuwaachia wenye afya safi, lakini bongo kwa vile ni bora liende tu wana gutts hata za kugombea uongozi zaidi, ingawa sasa hivi wote pia ni viongozi anyways!

3. Uwezekano wa Simba kushinda huu uchaguzi ni mdogo sana kuliko alivyotegemea mwanzoni, kwamba atasaidiwa na nguvu ya mtandao ile nguvu sasa haipo maana wenye nguvu wote huko sasa hivi wanajaribu kujitayarisha na msafara wa Kisutu, resources zote sasa zimeelekezwa huko kwa hiyo hakuna wa kumsaidia, Muungwana kwenye kuelekea 2010 hataki kabisa kugombana na kundi la asilia, ambali ndilo hasa linalomfadhili kisiasa sasa hivi ambako ndiko Mama Janet anakotokea,

- The dataz ni kwamba hata huu uchaguzi umesogezwa tarehe kwa makusudi kwa kushinikizwa na wabunge wa asilia ili waweze kumsaidia Mama Janet, maana watakuwepo Dodoma tayari kwa next kikao cha bunge, ninasema hivi the whole thing is pathetic, Rais Kikwete huu ni wakati muafaka wa kuondoa wabunge wa bure, wote wakagombee kwa wananchi na kusiwe na haya mambo ya kupewa ubunge wa chee maana haya ndio matokeo yake,

Hawa wawili ni vyema wote wakapigwa chini na kama ikibidi, basi wagombee wa visiwani tu kama vile kinana na jm walivyoamua kwenye uchaguzi wa vijana.

Thanxs!

FMES

1.Baada ya Mkapa; Viongozi,watendaji na wanachama wamechukua hatua gani kusahihisha jambo hili tunaloshuhudia likisababisha mambo ya aibu si kwa CCM lakini kwa nchi pia? Au waliopo wamelinyamazia kwa manufaa yao binafsi pia? Kulifanyia marekebisho yenye tija inagharimu pesa na muda kiasi gani? Tuendelee tu kulaumu Mkapa hata kwa yale ya kulekebisha kesho asubuhi au tuwalaumu waliopo?

2. Kwa upande wa uwiano wa wabunge bungeni, Vyama vya upinzani vinanufaikaje na utaratibu huu (Mwenyekiti UWT kuwa moja kwa moja mbunge) kikatiba. Naomba kueleweshwa
 
Kwa watu kama hao walionusa UN systems hawana muda mchafu wa kuanza kugombea tu cheo tudogo kama hutwo, twenye majungu mengi.

Unajua siasa zina watu wake, wacheza ngoma, wakakate viuono hao mwake. Akina Tibaijuka etc hawawezi.
 
Na Mwandishi Wetu (Mwanakijiji.com)

Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais (Utawala Bora) Mhe. Sophia Simba ndiye mwenyekiti mpya wa Umoja wa Wanawake wa CCM Tanzania. Bi. Simba amewashindwa wapinzani wake kwa kupata kura 470 ambayo ni sawa na asilimia ya 54.5 ya kura zote zilizopigwa. Mshindani wake mkubwa Bi. Janeti Kahama (MB-Viti Maalum) amepata 383 sawa na asilimia 44.4 na Bi. Joyce Masunga amepata kura 10 sawa na asilimia 1.1 ya kura 872. (Taarifa kamili yaja)
Ukumbi wa Mkutano ulilipuka kwa furaha baada ya Mhe. Simba kutangazwa mshindi huku muziki wa taarabu ukirindima kukoleza furaha ya ushindi huo. Ngoma za watu wa mwambao ikiwemo segere zilisindikiza tangazo hilo la ushindi. Wimbo ulioonekana kuzikosha nyoyo za wajumbe zaidi ni pamoja na ule wa "Msumari umechoma kotekote". Ushindi wa Bi. Simba umekuja baada ya mchakato uliojaa vijembe, malumbano, na tuhuma za kila aina na ambao kwa watu wengine ulionekana kutishia hatima ya jumuiya hiyo hasa katika suala la uongozi wake.

Ka "nzi" ka KLHN ambako kalikuwemo ndani ya mkutano huo wa uchaguzi na hivyo kutupasha kwa uhakika kanadokeza kuwa hata kabla ya kupigwa kura wapambe wa Bi. Sophia walionekana kuwa na uhakika wa matokeo ya ushindi wakiamini kuwa mgombea wao ndiye anakubalika zaidi hasa na viongozi wa Taifa akiwemo Rais Jakaya Kikwete.

"Unajua Bi.Sophia ndiye Waziri anashughulikia utawala bora, na utawala bora umeonekana ukifanya kazi katika masuala ya mafisadi hivyo ni wazi aliingia kwenye kinyang'anyiro hicho akiwa na ujiko mkubwa" amesema mjumbe mmoja kutoka mojawapo ya mikoa ya pwani na ambaye alikuwa karibu na kampeni ya Bi. Simba.

Akizungumza na tovuti hii kwa masharti ya kutotajwa jina lake kwani siyo msemaji wa UW-CCM, mjumbe huyo amesema kuwa Bi. Sophia asingeweza kushindwa uchaguzi huo ukizingatia nafasi yake.

"Kwanza yeye ni Mbunge wa kuteuliwa na Rais, na hivyo hajapigiwa kura mahali popote wakati wenzake Janeti na Joyce ni Wabunge wa Viti Maalum ambao nafasi zao zinatokana na mfumo wa uchaguzi ndani ya Chama." Amefafanua mjumbe huyo aliyezungumza kwa kujiamini.

"Pili, akiwa mbunge wa kuteuliwa na Rais amepewa Uwaziri wa Wizara nyeti nchini inayosimamia pia taasisi muhimu kama TAKUKURU na Usalama wa Taifa, hivyo anapoingia kwenye kinyang'anyiro ni vigumu kumuona kama mgombea mwingine," Amesema mjumbe huyo.

Naye mjumbe mwingine toka Songea ambaye alikuwa kambi ya Bi. Kahama ameonesha kusikitishwa na mchakato mzima wa uchaguzi wa Mwenyekiti wa TAifa akidai kuwa kilichotokea ni "Aibu". Alipobanwa na mwandishi wetu afafanue kwa nini anatumia neno hilo moja kuelezea kilichojiri Dodoma, mjumbe huyo amesema kuwa "Huwezi kuwa na wagombea watatu ambapo mmoja wao anapigiwa debe na Rais wa nchi".

Akifafanua zaidi mjumbe huyo amehoji mambo kadhaa. "Kwanza, pale Sophia Simba alipopitishwa kugombea Uenyekiti ingempasa amuombe Rais kupumzika kwa muda shughuli za Uwaziri wake na hivyo kutokuwa na access na vyombo nyeti kama TAKUKURU na Usalama wa Taifa". Kwa maelezo ya mjumbe huyo tuhuma za rushwa katika uchaguzi huo zisingeweza kuchunguzwa kwa uhuru zaidi wakati mmoja wa mawaziri wenye nguvu sana ni mmoja wa wagombea. "Pili" aliendelea mjumbe huyo, "Wakati Rais anatangaza vigezo vya nani achaguliwe, alitangaza kuwa mojawapo ni kuwa 'msomi', sasa ukiangalia kati ya wagombea wote hao ni Bi. Sophia ndiye anaonekana msomi zaidi.".

Pamoja na hayo inaonekana kwa namna au nyingine "damu mbaya" kati ya wagombea wakubwa wawili (Bi. Kahama na Simba) yaweza kudumu kwa muda mrefu zaidi licha ya baadhi ya wapambe wao kuonekana wakiserebuka pamoja. Kwa mujibu wa watu mbalimbali wanasubiri kuona ni jinsi gani Bi. Simba ataiongoza jumuiya hiyo na hivyo kujijengea imani kwa karibu nusu ya wajumbe ambao walionekana kumuunga mkono Bi. Kahama.

"Hapa bwana kuna dalili za kambi hizi mbili kuendelea hadi 2010" amesikika mjumbe mmoja.

Sasa hivi wajumbe na viongozi mbalimbali wanaendelea kutoa shukrani zao na pongezi pamoja na nasaha katika kuelekea kuhitimisha mkutano huo.
 
Sophia Simba ndiye Mwenyekiti mpya wa UWT kwa mujibu wa Kipindi cha HArakati cha TBC saa 10 hii.

soo safu ya ccm ni

mwenyekiti :jakaya khalfan mrisho kikwete

makamu mwenyekiti : pius msekwa

makamu mwenyekiti: amani abeid karume

katibu mkuu: yusufu mkamba..

mwenyekiti wazazi:Abdah bulembo

mwenyekiti wanawake: sofia simba

mwenyekiti vijana: masauni omari masauni

......haya sasa nione tena watu wanasema oooooh CUF wadini ,,....its just the matter of numbers ...imetokezea ccm asilimia 85 ya top brass ni waislamu......pia tunakubali..kwa kuwa wamechaguliwa au vipi....

.....mwaka 2005 ccm waliwanyanyasa sana CUF na hii ajenda ya TOP brass
 
Hujui unachokisema ni MDINI mkubwa wewe. Kwa taarifa yako Sofia Simba sio Muislamu ni MKRISTO wa MISHENI KOTA.
 
Sophia Simba Asilimia 54.5 (kura 470), Janeth Kahama Asilimia 44.3 (kura 383) Joice Masunga kura 10 (Asilmia 1.1).

Kura zilizopigwa 872 na tisa ziliharibika. Lakini jana kulikua na wajumbe 888 na hivyo inaonekana wajumbe 106 hawajapiga kura ama waliondoka wakijua uchaguzi ni leo wakapigwa bao na JK aliyeamua hakuna KULALA.

Mkuu halisi, hizi hesabu zako zinaniletea kizunguzungu. Kwa nini wasiopiga kura wawe 106 wakati tofauti kati ya wapigakura 872 na 888 ni 16 tu!!!
 
Hujui unachokisema ni MDINI mkubwa wewe. Kwa taarifa yako Sofia Simba sio Muislamu ni MKRISTO wa MISHENI KOTA.

Mbona unakurupuka ndugu ? Mwandishi hakusema Sophia Simba ni Muislamu au roho yako inakusuta ? Yeye kasema tu asilimia 85% ni Waislamu ..basi.
 
Hujui unachokisema ni MDINI mkubwa wewe. Kwa taarifa yako Sofia Simba sio Muislamu ni MKRISTO wa MISHENI KOTA.

...kaka ..mbona unakuja juu namna hiyo..tena kwa maandishi mekundu....mimi nimetoa safu ya viongozi wa ccm......i did not singled any of them ...nimewataja kwa pamoja..sasa iweje wewe uje kumuongelea mmoja tu sophia simba.??..kwa nini sio pius...?.....you can write more than that.....

....pamoja na kuwa sijaongelea sofia..NA sijui ni dini gani ..ila ni wazi inajulikana kuwa sofia alikuwa anaishi upanga...na mwanzoni amepata kuwa diwani wa kuteuliwa wilaya ya ilala[manispaa]....kabla ya kuteuliwa ubunge mwaka 2000-2005..mara ya kwanza......na amepata kuwa mke wa aliyekuwa MSTAHIKI MEYA WA JIJI -KITWANA KONDO.....

ameanzia kazi NDC ...miaka hiyo kama secretary ...kabla ya kujiendeleza kielimu ...kwa kwenda kusoma marekani........
 
Mkuu PM

Nimecheck kwenye mitandao, inaonyesha huyu dada anacertificate ya law kutoka UD na postgraduate studies on women's law kutoka Zimbabwe...sasa Marekani alisoma nini na lini? ama unataka kusema anacheti kingine cha kununua huko

http://www.afdevinfo.com/htmlreports/peo/peo_372.html

http://www.parliament.go.tz/bunge/Mp_Cv3.asp?PTerm=2005-2010&fpkey=235&vusername=GUEST")
 
Mkuu PM

Nimecheck kwenye mitandao, inaonyesha huyu dada anacerificate ya law kutoka UD na postgraduate studies on women's law kutoka Zimbabwe...sasa Marekani alisoma nini na lini? ama unataka kusema anacheti kingine cha kununua huko

Sophia Simba (Tanzania)

BUNGE::)

kaka i relied on my head unfortunatelly i did not take any link....thats why hata ukiangalia cv yake nimeweza kukumbuka kuwa amekuwa NDC,,...na diwani....na nakumbuka kusoma mahali kuwa amepata kusoma marekani.....inawezekana pia nikakosea...

lakini inaonesha kuwa ana LLB...hilo pia sikujuwa.....
thats why jk anasema wajumbe wachaguwe wasomi...nadhani mama janet sio msomi!
 
Hongera mwenyekiti mpya, hivi safari hii hakuna uwezekano wa kuwa na katinu mkuu mwanaume kama enzi zile?
 
Mbona unakurupuka ndugu ? Mwandishi hakusema Sophia Simba ni Muislamu au roho yako inakusuta ? Yeye kasema tu asilimia 85% ni Waislamu ..basi.

Acha ugando wa mawazo sasa utaipata hiyo namba ya 85% bila kujua dini za hao watajwa?
 
...kaka ..mbona unakuja juu namna hiyo..tena kwa maandishi mekundu....mimi nimetoa safu ya viongozi wa ccm......i did not singled any of them ...nimewataja kwa pamoja..sasa iweje wewe uje kumuongelea mmoja tu sophia simba.??..kwa nini sio pius...?.....you can write more than that.....

....pamoja na kuwa sijaongelea sofia..NA sijui ni dini gani ..ila ni wazi inajulikana kuwa sofia alikuwa anaishi upanga...na mwanzoni amepata kuwa diwani wa kuteuliwa wilaya ya ilala[manispaa]....kabla ya kuteuliwa ubunge mwaka 2000-2005..mara ya kwanza......na amepata kuwa mke wa aliyekuwa MSTAHIKI MEYA WA JIJI -KITWANA KONDO.....

ameanzia kazi NDC ...miaka hiyo kama secretary ...kabla ya kujiendeleza kielimu ...kwa kwenda kusoma marekani........

Sasa ulifikiaje conclusion kuwa top brass ya CCM ni 85% waislam kama hujui dini za Sofia Simba na Pius?

Kuolewa na Kitwana Kondo hakubadili ukweli kuwa ni MKRISTU
 
Sasa ulifikiaje conclusion kuwa top brass ya CCM ni 85% waislam kama hujui dini za Sofia Simba na Pius?

Kuolewa na Kitwana Kondo hakubadili ukweli kuwa ni MKRISTU

Mslam akimuoa mkristo anamslimisha. Hivyo Sofia Simba ni Mslam.
 
Yes,Gaidi JK umeongea clear na tumekusikia.
Jambo moja napenda ulifahamu ni kuwa ugaidi wako una kikomo.
Muda ukiwadia tutajitoa muhanga ikibidi kwa faida ya Taifa letu.
tumechoshwa na visa vyako.

Pole mama Kahama,ni pigo kwetu sote wakristo,tunaahidi kuwa pamoja nawe hasa ktk kipindi hiki kigumu kwako na kwetu sote.
Mshukuru angali huu hai na nguvu alizokujalia.Amina.

Ndg.Mtikila,kuwa ngangari,na hiyo kesi inayokukabili,si yako pekee,ni yetu sote wakristo.Wakijifanya wanajua zaidi zidi yako na yetu,hapata kalika hapo Tz.
 
Punguza munkari, twende taratibu ndugu vinginevyo utatuacha wengine. Unamaana JK Mdini?
 
Acha ugando wa mawazo sasa utaipata hiyo namba ya 85% bila kujua dini za hao watajwa?

Sina mpango wa kumkimbiza kichaa - people might never tell the difference lol. Inawezekana anajua dini zao lakini hajataja yupi ni yupi.
Hebu jiulize hiyo asilimia pungufu 15% inapatikanaje ? - ni elimu dunia tu.
 
Last edited:

Hujajibu swali ikiwa mleta hoja hajui dini za watajwa kawezaje kupata hizo asilimia? ni common sense tu...
 
Udini udini udini kila kukicha!!!! Udini unaipeleka pabaya JF na tusipokuwa makini tutapoteza umoja wetu na mshikamano tuliokuwa nao kutokana na watu wenye chuki binafsi kuhusu dini zetu kubwa mbili. 🙁
 
Back
Top Bottom