1. Haya ndio baadhi ya matatizo aliyotuachia Mkapa, alipoamua kwa ubabe kuwa mwenyekiti wa UWT na katibu wake wawe wabunge automatically ili kumuokoa rafiki wa kusini mwenziwe Mama Anna Abdallah, ambaye alishajua mapema kua hawezi shinda ubunge kwenye jimbo tena,
- kule kwenye ubunge kuna dola $ 30,000 kila baada ya miaka mitano na shangingi moja la bure kila five years, toka Mkapa alete huu ubabe wake hizo nafasi mbili UWT zimekua mbinde tupu, na aibu kwa taifa licha ya CCM kama chama.
2. Now comes this, hawa wakina mama wawili inafahamika wazi ndani ya uongozi wa CCM na serikali on a national level, kwamba afya zao sio nzuri sana, infact ingekua majuu wasingekua viongozi wangetakiwa wapumzike pembeni na kuwaachia wenye afya safi, lakini bongo kwa vile ni bora liende tu wana gutts hata za kugombea uongozi zaidi, ingawa sasa hivi wote pia ni viongozi anyways!
3. Uwezekano wa Simba kushinda huu uchaguzi ni mdogo sana kuliko alivyotegemea mwanzoni, kwamba atasaidiwa na nguvu ya mtandao ile nguvu sasa haipo maana wenye nguvu wote huko sasa hivi wanajaribu kujitayarisha na msafara wa Kisutu, resources zote sasa zimeelekezwa huko kwa hiyo hakuna wa kumsaidia, Muungwana kwenye kuelekea 2010 hataki kabisa kugombana na kundi la asilia, ambali ndilo hasa linalomfadhili kisiasa sasa hivi ambako ndiko Mama Janet anakotokea,
- The dataz ni kwamba hata huu uchaguzi umesogezwa tarehe kwa makusudi kwa kushinikizwa na wabunge wa asilia ili waweze kumsaidia Mama Janet, maana watakuwepo Dodoma tayari kwa next kikao cha bunge, ninasema hivi the whole thing is pathetic, Rais Kikwete huu ni wakati muafaka wa kuondoa wabunge wa bure, wote wakagombee kwa wananchi na kusiwe na haya mambo ya kupewa ubunge wa chee maana haya ndio matokeo yake,
Hawa wawili ni vyema wote wakapigwa chini na kama ikibidi, basi wagombee wa visiwani tu kama vile kinana na jm walivyoamua kwenye uchaguzi wa vijana.
Thanxs!
FMES
1.Baada ya Mkapa; Viongozi,watendaji na wanachama wamechukua hatua gani kusahihisha jambo hili tunaloshuhudia likisababisha mambo ya aibu si kwa CCM lakini kwa nchi pia? Au waliopo wamelinyamazia kwa manufaa yao binafsi pia? Kulifanyia marekebisho yenye tija inagharimu pesa na muda kiasi gani? Tuendelee tu kulaumu Mkapa hata kwa yale ya kulekebisha kesho asubuhi au tuwalaumu waliopo?
2. Kwa upande wa uwiano wa wabunge bungeni, Vyama vya upinzani vinanufaikaje na utaratibu huu (Mwenyekiti UWT kuwa moja kwa moja mbunge) kikatiba. Naomba kueleweshwa