Waziri Tabia Mwita: Ukarabati Uwanja wa Amani Una Lengo la Kuufanya Ukidhi Viwango vya Kimataifa

Waziri Tabia Mwita: Ukarabati Uwanja wa Amani Una Lengo la Kuufanya Ukidhi Viwango vya Kimataifa

Stephano Mgendanyi

JF-Expert Member
Joined
May 16, 2020
Posts
2,833
Reaction score
1,301
Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo (SMZ) Mhe. Tabia Maulid Mwita amesema ukarabati unaoendelea kufanyika katika uwanja wa amani una lengo la kuimarisha na kuufanya kuwa wa kisasa na wenye kukidhi viwango vya kimataifa.

Ameyasema hayo alipokuwa akiwasilisha taarifa ya utekelezaji wa malengo ya wizara kwa kipindi cha miezi mitatu kuanzia Julai hadi September 2023 kwa kamati ya kudumu ya ustawi wa jamii ya baraza la wawakishi huko ukumbi wa baraza la wakilishi chukwani.

Amesema ukarabati huo unatekelezwa kwa fedha za serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar ambapo wizara inatekeleza mradi huo kupitia mkandarasi wa kampuni ya Orkun kwa thamani ya dolla za kimarekani millioni ishirini na mbili na laki moja (22,100'000us)

Amefahamisha kuwa utekelezaji wa mradi huo wa uwanja wa amani tayari umefikia asilimia 85 na unatarajiwa kukamilika mwezi disemba 2023.

Kwa upande wa ukarabati wa uwanja wa gombani pemba umeanza utekelezaji wake kwa mwaka wa fedha 2022/ 2023 na umefikia asilimia 83 ambapo bajet ya shillingi billioni mbili na bilioni mianane na hadi sasa jumla ya shilling 2,408,216'117 zimelipwa kwa mkandarasi kwa ajili ya utekelezaji chini ya kampuni ya ujenzi ya salim construction LMD Osaju COMPANY LMD.

Akieeleza zaidi mafanikio mengine yaliyopatikana kwa kipindi cha mwaka mmoja kuanzia Julia 2022 hadi juni 30 2023 Tabia amesema wameimarisha shuhuli za uchapaji ikiwemo kuongeza idadi ya maombi ya huduma za uchapaji kutoka katika taasisi za serikali asilimia 32 ikilinganishwa na mwaka wa fedha 2021/ 2022.

Pia wakala imefanikiwa kurudisha kwa baadhi ya wateja wake wakubwa ambao kwa muda mrefu walikosa Imani na huduma za wakala ikiwemo bank ya watu wa zanzibar (pbz) mamlaka ya mapato zanzibar (ZRA) na wakala wa matukio ya kijamii.

Kwa upande wake mwenyekiti wa kamati ya ustawi wa jamii ya baraza la wakilishi Sabina Fulfil Thani ameipongeza wizara ya habari, vijan, utamaduni na michezo kwa kufanya vizuri na kuwataka watendaji kuendelea kusimamia na kufanya kazi kwa bidii kwa kila idara husika ili kufikia malengo yanayotakiwa na serikali.

WhatsApp Image 2023-11-16 at 17.58.02(2).jpeg
WhatsApp Image 2023-11-16 at 17.58.02(1).jpeg
WhatsApp Image 2023-11-16 at 17.58.02.jpeg
WhatsApp Image 2023-11-16 at 17.58.01(1).jpeg
 
Back
Top Bottom