Waziri TAMISEMI na uongozi Halmashauri ya Wilaya Hai tupieni macho suala hili

Waziri TAMISEMI na uongozi Halmashauri ya Wilaya Hai tupieni macho suala hili

Isalu

JF-Expert Member
Joined
Nov 3, 2022
Posts
504
Reaction score
665
Kwa masikitiko makubwa naomba kuwasilisha taarifa hii kwenu uongozi wa halmashauri ya wilaya Hai, kuhusiana na namna watendaji ktk Kijiji cha Mungushi wanavyohujumu mapato ya Kijiji yanayotokana na uuzwaji wa viwanja ktk eneo la Kijiji.

Yameuzwa maeneo mengi sana na karibia Kijiji kinajaa wakazi wapya lakini mapato ya 10% ya Kila eneo linalouzwa yanayotakiwa kuingizwa hazina ya Kijiji Kwa ajili ya maendeleo ya Kijiji yanaishia mifukoni mwa viongozi wa Kijiji wasio na uadilifu na uaminifu.

Yapo Majengo mawili ya walimu ktk shule ya msingi Mungushi ambayo yameshindikana kukamilika kwa kukosa fedha kwa miaka mingi na fedha hizi za percent za mauzo ya viwanja zingetosha kabisa kukamilisha nyumba hizi za walimu na hata kuongeza nyingine Ili walimu waondokane na adha ya kusafiri kutoka mbali ambako pia wamepanga nyumba.

Tunaomba Mkuu wa wilaya Hai uingilie kati suala hili na mapato ya Kijiji yafanye kazi Kwa maendeleo ya Kijiji na sio kuishia mifukoni mwa wachache kwa manufaa binafsi. Ikibidi waziri Tamisemi tunaomba ufuatilie jambo hili,Maana pia hakuna jambo lolote lililofanyika la kimaendeleo Kijiji I kwetu hadi sasa. Kwa ujumla hakuna kinachofanyika.
 
Back
Top Bottom