Kiingereza cha Waziri, katika nchi ambayo Kiingereza ni lugha rasmi, si kizuri, huwezi kukitetea.
Na pengine kama hujazoea Kiingereza kizuri, huwezi kuona mapungufu.
So, from the outset Ulega kakosea, aliyemteua Ulega kakosea. Hilo kwangu halina mjadala. Waziri anatakiwa kujua Kiingereza. Akisafiri nje ataongea Kiswahili? Hata kama atatafsiriwa, kama Kiingereza chake cha matata, ataweza kusoma na kuelewa mambo ya nje ya Tanzania? Kutokujua Kiingereza, hata kama kuna watafsiri, kunapunguza efficiency ya mawasiliano.
Hiki Kiingereza angeongea Waziri wa DR Congo, ningeweza kumtetea kuwa nchi yao hawaongei Kiingereza. Lakini kwa nchi ambayo Kiingereza ni lugha rasmi, Kiingereza hiki si kizuri, lakini pia si Kiingereza fulani ambacho hakieleweki Waziri anasema nini.
Sasa hapo tunapaswa kujiuliza swali.
Of course in the perfect world tunatakiwa kuwa na Waziri anayejua Kiingereza vizuri na anayewabana anaotakiwa kuwabana kwa Kiingereza kilichonyooka kabisa.
Lakini je, ukiwa na Waziri kama Ulega mwenye Kiingereza cha kuvuta kwa manati, ungependa afanye nini? Asifanye kazi yake ya kuwabana anaotaka kuwabana mpaka aweze kuongea Kiingereza cha Mfalme Charles kwa lafudhi ya Received Pronunciation ya James Naughtie wa BBC?
Labda vijana wa sasa hamjui habari ya Bunge la Tanzania kuanza kukubali Kiswahili ilianzaje.
Mbunge wa Kinondoni ( nafikiri Kinondoni), Bibi Titi Mohammed, alikuwa bungeni akitaka kuwakilisha watu wake vizuri, akitaka kudai umeme upelekwe Magomeni watu wa Magomeni wafaidi kuwa na taa za umeme.
Lakini Bibi Titi Mohammed, ingawa alikuwa na ari kubwa sana ya kuwasikisha hoja yake hii bungeni, hakuwa msomi, hakujua sana Kiingereza.
Bobi Titi Mohammed akawa na uamuzi mgumu sana. Je, asimame na kudai anachotaka kudai kwa Kiingerwza ambacjo hakijui vizuri na anaweza kuboronga maneno akachekwa na watu? Au akae kimya na kuogopa kuharibu Kiingereza, lakini kwa kukaa kimya hivyo, aiachie nafasi ya kupigania haki za wananchi waliomtuma bungeni?
Bibi Titi Mohammed akaamua kusimama na kuongea kwa Kiingereza hicho hicho cha manati alichokijua.
Hapo ndipo aliposimama na kutoa hotuba iliyopata umaarufu ya "fire in the bottle". Akisema kwamba "We want fire in Magomeni...We want fire in small bottles".
Watu wajawa hawaelewi, anamaanisha nini kwa kusema "We want fire in small the bottles"?
Wakaja kugundua kuwa alikuwa anadai umeme ili watu wa Magomeni wapate taa za umeme, "fire in small bottles" ni zike taa za umeme.
Sasa hapo utamcheka Bibi Titi kuwa alikuwa hajui Kiingereza? Au utamsifia kuwa huyu alikuwa shujaa wa kupigania maslahi ya wananchi waliomtuma, hata pale ambapo hakujua Kiingereza vizuri, alisimama hivyohivyo ili nradi kawakikisha watu wake tu?
Serikali ililiona hili tatizo. Watu wetu wwngi hawajui Kiingerwza, kwa nini tunalazimisha bunge liwe ka Kiingereza?
Wakabadilisha mfumo wakaruhusu wabunge kuongea Kiswahili.
Ulega kaharibu lugha. Hapo siwezi kumtetea.
Vipi kuhusu substance?
Kuna watu wamezungumzia substance ya alichoongea Ulega?
Au tumeishia kucheka lugha tu?