Waziri Ummy: CoronaVirus bado ipo, tuendelee kuchukua tahadhari

Waziri Ummy: CoronaVirus bado ipo, tuendelee kuchukua tahadhari

Waziri wa Afya Ummy Mwalimu amesema idadi ya wagonjwa wa Corona nchini waliobaki kwenye vituo vya matibabu imepungua mno.

Akizungumza Leo mkoani Tanga wakati wa ziara ya Waziri Mkuu Kassim Majaliwa mkoani humo amesema:

“Tanga hatuna mgonjwa wa Corona, Amana wamebaki 3, Mloganzila 1, Kibaha 0, Mwanza 0”.

Ummy amesisitiza kuwa Corona bado ipo na kuwataka watanzania kuendelea kujikinga.

“Na mimi nilisema pale Dodoma, katika Uwaziri wangu sikuwahi kupitia kipindi kigumu kama hiki cha Corona kwakweli nilihenya” amesema Waziri Ummy Mwalimu.
Huyu naye kituko, ! anadhani watanzania wote ni wajinga ! Anasahau kuwa wanaoumwa ni ndugu zetu ambao kwa mwenendo wa serikali tumeamua wafie majumbani! Akumbuke tuna watoto wetu humo ma haspitalini! Tunapata taarifa zote!
 
Back
Top Bottom