Watu wenye Corona hawaendi hospital maana wananyanyapaliwa. Wengi wako nyumbani wanatumia asili. Ninavyoandika hapa amezikwa shemeji huko Moshi alikufa Corona huko kanda ya ziwa. Jumatano wiki hii anazikwa mwingine huko Marangu na mwili utapelekwa na watu wa afya kutoka Arusha. Mwingine atazikwa Rombo Ijumaa hii mwili utatolewa Moshi. Je serikali inayo taarifa kamili za hali ya ugonjwa nchini? Watanzania tuchukue tahadhari Korona ipo na inaenda kasi sana. Vaa barakoa , kula virurubisho, piga nyungu, epuka mikusantiko. Cha kusikitishaha toka ile tarehe 24 May walipotangaza hali si mbaya wagonjwa wamebaki 9 basi 99% ya watanzania wameyarudia maisha ya kawaida. Life ni kama kawaida vijiweni mpaka daladala hakuna barakoa tena. Soko la Temeke Stereo nilipata hata yale mtanki ya maji ya kunawa hayana maji muda mrefu sana. Nihatari sana hii.