Waziri Ummy: CoronaVirus bado ipo, tuendelee kuchukua tahadhari

Waziri Ummy: CoronaVirus bado ipo, tuendelee kuchukua tahadhari

Kwa kweli Mungu ametufanyia mambo makuu. Walioathirika na corona tupo ila tumekua wachache zaidi ya kile wengi walichotarajia. Tunamshukuru Mungu kwa kuilinda nchi yetu, na tumshukuru rais wetu John Pombe Magufuli kwa maono sahihi ya kuchukua tahadhari na kusali
Tuliokua tunabeza kumwomba Mungu tukisubiri idadi ya vifo kuongezeka tusisahau kufanya toba😁😁😁
 
Hivi inawezekana ikawa tumetumia mbinu gani kulishinda hili janga hivi, Kwa mbinu yoyote tuliyotumia kwanini tusi share na ulimwengu ili kunusuru dunia na hili janga

Sent using Jamii Forums mobile app
Tumetumia mbinu ya kutopima na kutangaza maana ilikuwa inaongeza taharuki kwa raia. Mitaani nasikia wagonjwa wapo, ila hii ni kwa mujibu wa radio mbao!!
 
Mmm hizi siasa mimi ninawatu ofisini mpaka sasa hawajawa cleared na C-19 bado inasomeka positive.Mchukue tahadhari za afya jamani kwa faida ya afya yako.
 
Juzi na jana jamaa zangu wa karibu wawili wamefariki kwa corona na wote eneo moja la Bulyanhulu. Endeleeni kuficha sie taarifa tunazo kwa kile kinachoendelea. Kwa sasa kutoa taarifa ya kifo cha corona huko ni uhaini. Si vizuri kuweka picha zao na majina yao hapa ila mlio na ndugu Kakola Bulyanhulu ulizeni
Kituo/Hospital gani huko Bulyanhulu iliwapima ikatoa majibu kuwa Wana Corona?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kwa kweli Mungu ametufanyia mambo makuu. Walioathirika na corona tupo ila tumekua wachache zaidi ya kile wengi walichotarajia. Tunamshukuru Mungu kwa kuilinda nchi yetu, na tumshukuru rais wetu John Pombe Magufuli kwa maono sahihi ya kuchukua tahadhari na kusali
Tuliokua tunabeza kumwomba Mungu tukisubiri idadi ya vifo kuongezeka tusisahau kufanya toba😁😁😁
ESOPO
 
nashangaa Marekani wanaandamana na wengi wao hawana hata barakoa wala hamna cha sanitazer wala nini, usikute huu ugonjwa umekaa kiakili zaidi
 
Wanalihadhaa Taifa, mkono wa Mungu utawafikia sooner rather than later![emoji120]
 
Watu wenye Corona hawaendi hospital maana wananyanyapaliwa. Wengi wako nyumbani wanatumia asili. Ninavyoandika hapa amezikwa shemeji huko Moshi alikufa Corona huko kanda ya ziwa. Jumatano wiki hii anazikwa mwingine huko Marangu na mwili utapelekwa na watu wa afya kutoka Arusha. Mwingine atazikwa Rombo Ijumaa hii mwili utatolewa Moshi. Je serikali inayo taarifa kamili za hali ya ugonjwa nchini? Watanzania tuchukue tahadhari Korona ipo na inaenda kasi sana. Vaa barakoa , kula virurubisho, piga nyungu, epuka mikusantiko. Cha kusikitishaha toka ile tarehe 24 May walipotangaza hali si mbaya wagonjwa wamebaki 9 basi 99% ya watanzania wameyarudia maisha ya kawaida. Life ni kama kawaida vijiweni mpaka daladala hakuna barakoa tena. Soko la Temeke Stereo nilipata hata yale mtanki ya maji ya kunawa hayana maji muda mrefu sana. Nihatari sana hii.
Mtaani kwetu kuna wagonjwa watatu. Hospitali wameandikiwa wanaumwa Severe pneumonia. Wamepewa vidonge wajitibu nymbani. Wana dalili zote za Covid 19. Nilichoshangaa ni kuwa kwa kuwa kwa sababu hakuambiwa wanaumwa nini wala hawavai barakoa hapo nyumbani wala kujitenga. Kwa vile wana nafasi ni mimi nisiye daktari niliwahauri kujitenga na wanaowahudumia kuchukua hatua. Mmoja ameanza kuwa na nafuu na familia zao hamna aliyeonesha dalili ya kuathirika hadi sasa. Ugonjwa huu upo. Tuchukue tahadhari.
 
Wale wa juzi waliorudishwa na kukabidhiwa kwa mamlaka kutoka Kenya na Uganda wako wapi? Serikali hii bhana ina mambo ya ajabu sana.
Data za uhakika tuzipate kwa madaktari wakuu wa mahosipitali.Tuanze na Agakhan Dsm sasa hivi.Saa hii.Mbali na hapo politics hapana.Maisha ya Watanzania ni ya thamani sana.
 
Herd immunity. Wiki hii mate wangu alifariki kwa COVID-19, wiki iliopita jirani zangu 2 walifariki pia. Na ofisini tuna mgonjwa mmoja (driver). What wanders around comes around.
Hivi inawezekana ikawa tumetumia mbinu gani kulishinda hili janga hivi, Kwa mbinu yoyote tuliyotumia kwanini tusi share na ulimwengu ili kunusuru dunia na hili janga

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ugonjwa Umepungua Sana yaani wamebaki wagonjwa wanne tu TZ Nzima ila Mipakani huko Kila siku "MADEREVA WA NCHI NYINGINE" wanakutwa na Korona.
HAPO HAATA MIMI NASHANGAZWA,INAWEZEKANA VIFAA VYA WENZETU KENYA ,UGANDA ,BURUNDI NI VIBOVU?
 
Mtaani kwetu kuna wagonjwa watatu. Hospitali wameandikiwa wanaumwa Severe pneumonia. Wamepewa vidonge wajitibu nymbani. Wana dalili zote za Covid 19. Nilichoshangaa ni kuwa kwa kuwa kwa sababu hakuambiwa wanaumwa nini wala hawavai barakoa hapo nyumbani wala kujitenga. Kwa vile wana nafasi ni mimi nisiye daktari niliwahauri kujitenga na wanaowahudumia kuchukua hatua. Mmoja ameanza kuwa na nafuu na familia zao hamna aliyeonesha dalili ya kuathirika hadi sasa. Ugonjwa huu upo. Tuchukue tahadhari.
Yaani Mkuu wangu ni hatari. Hata kuwapima was naona hawafanyi. Huyo mgonjwa wa Arusha alianza kuumwa wiki 2 zukizopita na Hospital alikuwa anaenda ila anapewa dawa tu wala hakupimwa. Alipofariki ndiyo wamepima mwili na kuthibitisha corona hivyo watumishi wa afya wanasafirisha mwili kutoka Arusha hadi Marangu. Ndugu zanguni tujilinde na kujikinga. Ukiona dalili kazana mno kula virutubisho na nyungu. Tulia nyumbani kula limao ma tangawizi kila 3 hrs au hata 2hrs na mboga na matunda
 
Muongo mkubwa.watu wanakufa Sana kwa changamoto za upumuaji. serikali imegoma kupima watu.
 
Back
Top Bottom