Waziri Ummy Mwalimu: Maambukizi COVID-19 ya ndani kwa ndani yameanza, Watanzania wajiandae kwa maambukizi ya Jumuiya

Mkuu tuombe radhi,pesa yetu ni ya quality ya hali ya juu sana haiwezi sambaza virusi vya corona.mdudu akigusa tu either anakufa au anateleza na kudodoka by BOT
 
Unamuomba
Your browser is not able to display this video.

huyu au mwingine?
 
Hatujachelewa Sana,kinachohitajika full lockdown hasa miji mikubwa dar,mz,Arusha,mbeya kwa mda wa siku 14,hii itazuia maambukizi mapya na wale walioambukizwa hizo siku zinatosha ugonjwa kuwa incubated na hivyo watajulukana na kuwa isolated
Mkuu wanaccm walikuwa wanasema watanzania ni wabangaizaji ukiweka total lockdown utawaua wote kwa njaa,so acheni uvivu kapigeni kazi
 
Makanisa na misikiti isitishe ibada zao kwa muda
 
Tutakosa Kodi,Kuna watu hawatalipwa mishahara
 
Zenji naona wameshatangaziwa kufunga misikiti
 
Hapo ndipo utawajua kama viongozi wa dini wapo kwa ajili ya watu au wapo kipesa. Aliyepo kipesa atapata tabu sana kusema ibada basi mpaka upepo upite. Ila waumini tutakuwa tushajiongeza kitambo.
 
Tumeambiwa na Waziri wa Afya, Mhe,Ummy Mwalimu kuwa ugonjwa wa corona unaweza kuambukizwa kwa njia ya hela hii maana yake kunawa mikono pekee hakutoshi na sasa tumeanza kusisitizwa tutumie mask(barakoa).

Swali linakuja,watanzania wangapi wamepata taarifa hii mpya na ni wangapi watakuwa wameandaa mask za kuvaa wanapoenda kwenye nyumba za ibada hasa siku ya kesho watapomiminika katika makanisa kwa Ibada ya Ijumaa kuu?

Kutokana na taarifa hii mpya na kwa kuzingatia tahadhari tuliochukua ni ya kunawa mikono tu kabla ya kuingia katika nyumba zetu za Ibada,nashauri serikali ichukue maamuzi magumu ya kuzuia ibada zote kwa muda(kuanzia kesho) kama walivyozuia mikusanyiko mingine, vinginevyo huko mbeleni tutakuja kulaumiana na serikali ndio itakuwa ya kwanza kulaumiwa unless janga hili halitakuwa tishio hapa nchini.

Tutambue wenzetu huko Ulaya sasa wanatembea na mask hivyo tusijichukulie kirahisi jambo hili.

Tusisubiri mazingira ya ugonjwa yatulazimishe kuchukua tahadhari fulani fulani, bali tutumie mazingira ya ugonjwa kuona umuhimu wa kuchukua tahadhari hizo angali mapema.

Majuto ni mjukuu;maji yakimwagika,hayazoleki.
 
Ibada inafanyika mara moja kwa wiki kwa muda wa masaa yasiyozidi mawili halafu mnasema zisitishwe! Mbona masoko yako wazi siku zote kwa masaa hadi kumi na mbili kila siku lkn hamsemi yafungwe?

Vv

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Utakuwa mganga wa kienyeji bila shaka.

Maana nilisikia ibada huwa zinawaharibia mizimu yenu
 
Huyu mama anajaribu kuwazuga Watanzania sasa kama anakiri ugonjwa umeletwa kutoka nje kwanini saivi aseme tunaambukizana wenyewe kwa wenyewe sio kutoka nje tena??,, Sasa kama ni ivyo lawama zitaendelea kubaki kwao kwanini waliruhusu apo kabla wageni kuingia kuleta maradhi? sasa anajaribu kuleta lawama kwa watanzania nadhani ameongea kauli mbaya sana na kuna jambo linafichwa fichwa watanzania amkeni
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…