Ambition plus
JF-Expert Member
- Feb 23, 2018
- 6,101
- 11,381
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Mkuu tuombe radhi,pesa yetu ni ya quality ya hali ya juu sana haiwezi sambaza virusi vya corona.mdudu akigusa tu either anakufa au anateleza na kudodoka by BOTZile wiki mbili nadhani sasa zinaelekea kutimia,huu ndo wakati hasa wa ku apply safe distance na kuosha mikono.
Nimegundua kwenye uoshaji mikono wahudumu mfano wa maduka, bar etc hawaoshi mikono kabla na baada ya kumuhudumia mteja mmoja.
Wakati wait ndo wanakamata pesa kutoka kila mtu, hii Ni hatari maana mfano uko bar,umeagiza beer,umenawa, muhudumu kakufungulia bia,kumbe mikono yake imeshika pesa za mtu mwingine na iko taitend, anaacha virusi kwenye chupa,wewe unakamata chupa unakunywa huku unaperusi mtandaoni, bila kujua umeshika virus na umehamishia kwenye simu.
Unamaliza bia unalipa,unanawa na kuondoka huku ukiperusi,umesahau Sasa simu Ina virus,unapeleka virus kwako,unaingia ndani unashika kitasa cha mlango, umeacha virus.
Unashika chupa ya chai,umeacha virus,hivyo yeyote atakaeshika hizo sehemu anaingia kwenye mlolongo
UnamuombaKama Mh. Mwalimu waziri wa Afya alivyosema maambukizi yamehamia kuwa ya ndani, ninamshauri na kumuomba Mh. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, aliangalie suala la mikusanyiko ya nyumba za Ibada kwa mapana.
Kiukweli nyumba za Ibada zinapaswa kuacha kuendelea kukusanya waumini ikizingatiwa mikusanyiko ni moja ya njia za kuongeza maambukizi kwa umma. Ushauri wangu mikusanyiko ya nyumba za Ibada izuiwe. Mh. Rais unaweza kuwaita viongozi wa Imani tofauti na kuwaeleza hili kabla hali haijawa mbaya!
Mkuu wanaccm walikuwa wanasema watanzania ni wabangaizaji ukiweka total lockdown utawaua wote kwa njaa,so acheni uvivu kapigeni kaziHatujachelewa Sana,kinachohitajika full lockdown hasa miji mikubwa dar,mz,Arusha,mbeya kwa mda wa siku 14,hii itazuia maambukizi mapya na wale walioambukizwa hizo siku zinatosha ugonjwa kuwa incubated na hivyo watajulukana na kuwa isolated
Makanisa na misikiti isitishe ibada zao kwa mudaAmeongea kwa unyenyekevu kuonesha hatari inayoweza kujitokeza kuanzia wiki ijayo.
Binafsi nimeona kabisa akiwa anatarajia viongozi wa dini watatumia busara kubwa kuamua kuwepo kwa ibada ama lah.
Kufuata masharti ya distancing kwa vipimo vilivyowekwa kuanzia mita moja,ni jambo gumu pengine haliwezekani kabisa katika makanisa yetu.
Watu ni wabishi,wana kiburi cha uzima,wakiamini nchi za wazungu zimeadhibiwa kutokana na uasi wao,na hivyo kwetu sio rahisi hali kama ile kutokea.
Suala la kuvaa barakoa(mask) linaonekana sasa kupata nguvu sana.Na ametoa wito watu watakaotoka nje wavae barakoa ili kuzuia mambukizi kwenda kwa wengine ama wao kupata maambukizi.Je kanisani watu watavaa barakoa?
Ni hekma na busara tu za viongozi wa dini sasa zinatakiwa kwani naona serikali imewapa Uhuru.
Itakuwa vibaya kuruhusu watu wako wakusanyike na wapate maambukizi au wasambaze maambukizi yanayoweza kuleta maafa makubwa.
Mungu hadhihakiwi.
Sent using Jamii Forums mobile app
Tutakosa Kodi,Kuna watu hawatalipwa mishaharaIliporipotiwa kesi ya kwanza ya uwepo wa mgonjwa wa Corona, kama kawaida yetu tukaanza kumsingizia Mungu atalinusuru taifa letu ili kukwepa kuingia gharama za ziada ktk kukabiliana na gonjwa hili. Tulisikia uropikaji wa wanasiasa eti hatuwezi kuzuia wageni kuja nchini kwa sababu ya tamaa ya fedha za kigeni.
Kuna msemo ktk lugha ya Kiingereza usemao, "Truth is stranger than fiction", nafikiriki ndipo hasa walipokwana viongozi wetu na wale wafuasi wao wenye kupenda kusifu na kuabudu tu. Nahisi akili sasa zitaanza kuwarudi na kuchukua hatua stahiki ili kuokoa maisha ya wananchi.
Ni vyema Jiji la DSM likaingia kwenye karantini mara moja, ili watu wasiweze kuingia ama kutoka kwa siku angalau 21.
Sent using Jamii Forums mobile app
mkuu hawa watu ni wabishi haijawahi kutokea yaani kama vile serikali iliyopo wameiweka waoMakanisa na misikiti isitishe ibada zao kwa muda
Zenji naona wameshatangaziwa kufunga misikitiAmeongea kwa unyenyekevu kuonesha hatari inayoweza kujitokeza kuanzia wiki ijayo.
Binafsi nimeona kabisa akiwa anatarajia viongozi wa dini watatumia busara kubwa kuamua kuwepo kwa ibada ama lah.
Kufuata masharti ya distancing kwa vipimo vilivyowekwa kuanzia mita moja,ni jambo gumu pengine haliwezekani kabisa katika makanisa yetu.
Watu ni wabishi,wana kiburi cha uzima,wakiamini nchi za wazungu zimeadhibiwa kutokana na uasi wao,na hivyo kwetu sio rahisi hali kama ile kutokea.
Suala la kuvaa barakoa(mask) linaonekana sasa kupata nguvu sana.Na ametoa wito watu watakaotoka nje wavae barakoa ili kuzuia mambukizi kwenda kwa wengine ama wao kupata maambukizi.Je kanisani watu watavaa barakoa?
Ni hekma na busara tu za viongozi wa dini sasa zinatakiwa kwani naona serikali imewapa Uhuru.
Itakuwa vibaya kuruhusu watu wako wakusanyike na wapate maambukizi au wasambaze maambukizi yanayoweza kuleta maafa makubwa.
Mungu hadhihakiwi.
Sent using Jamii Forums mobile app
Khaa, kwa hiyo umeambiwa huu ugonjwa wanapata wachafu?Awo viongozi wasisubiri sadaka za watu wafunge makanisa yao ...ibaki misikiti tu waislamu uwa wanazingatia usafi sana.
Sijui kwanini huwa tunawacheka waliokuwa wafuasi wa Kibwetere!!!!Ibada inafanyika mara moja kwa wiki kwa muda wa masaa yasiyozidi mawili halafu mnasema zisitishwe! Mbona masoko yako wazi siku zote kwa masaa hadi kumi na mbili kila siku lkn hamsemi yafungwe?
Vv
Sent using Jamii Forums mobile app