Waziri Ummy Mwalimu: Maambukizi COVID-19 ya ndani kwa ndani yameanza, Watanzania wajiandae kwa maambukizi ya Jumuiya

Waziri Ummy Mwalimu: Maambukizi COVID-19 ya ndani kwa ndani yameanza, Watanzania wajiandae kwa maambukizi ya Jumuiya

Kama serikali hamna strategy,xia watu wasitoke mkoa kwenda mkoa kwa kibalimaalumu

Hilo ndio lingekua la msingi sio kuzuia Jambo fulani gafla wangekuwa na utaaratibu wa kuwaanda raia kwa maamuzi ya baadae... Mfano Kama watazuia raia kusafiri kwa siku kadhaa au kwa muda fulani watu wasitoke nje... Watoe taarifa mapema ili raia wajiandae.
 
Zile wiki mbili nadhani sasa zinaelekea kutimia,huu ndo wakati hasa wa ku apply safe distance na kuosha mikono.

Nimegundua kwenye uoshaji mikono wahudumu mfano wa maduka, bar etc hawaoshi mikono kabla na baada ya kumuhudumia mteja mmoja.

Wakati wait ndo wanakamata pesa kutoka kila mtu, hii Ni hatari maana mfano uko bar,umeagiza beer,umenawa, muhudumu kakufungulia bia,kumbe mikono yake imeshika pesa za mtu mwingine na iko taitend, anaacha virusi kwenye chupa,wewe unakamata chupa unakunywa huku unaperusi mtandaoni, bila kujua umeshika virus na umehamishia kwenye simu.

Unamaliza bia unalipa,unanawa na kuondoka huku ukiperusi,umesahau Sasa simu Ina virus,unapeleka virus kwako,unaingia ndani unashika kitasa cha mlango, umeacha virus.

Unashika chupa ya chai,umeacha virus,hivyo yeyote atakaeshika hizo sehemu anaingia kwenye mlolongo

Asee na nipo hapa napiga senge laga moja. Ni kweli unachosema... acha nisepe home.
 
Ameongea kwa unyenyekevu kuonesha hatari inayoweza kujitokeza kuanzia wiki ijayo.

Binafsi nimeona kabisa akiwa anatarajia viongozi wa dini watatumia busara kubwa kuamua kuwepo kwa ibada ama lah.

Kufuata masharti ya distancing kwa vipimo vilivyowekwa kuanzia mita moja,ni jambo gumu pengine haliwezekani kabisa katika makanisa yetu.

Watu ni wabishi,wana kiburi cha uzima,wakiamini nchi za wazungu zimeadhibiwa kutokana na uasi wao,na hivyo kwetu sio rahisi hali kama ile kutokea.

Suala la kuvaa barakoa(mask) linaonekana sasa kupata nguvu sana.Na ametoa wito watu watakaotoka nje wavae barakoa ili kuzuia mambukizi kwenda kwa wengine ama wao kupata maambukizi.Je kanisani watu watavaa barakoa?

Ni hekma na busara tu za viongozi wa dini sasa zinatakiwa kwani naona serikali imewapa Uhuru.

Itakuwa vibaya kuruhusu watu wako wakusanyike na wapate maambukizi au wasambaze maambukizi yanayoweza kuleta maafa makubwa.

Mungu hadhihakiwi.


Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom