Waziri Ummy Mwalimu: Maduka ya Dawa nje ya hospitali yaliyo ndani ya mita 500 kuondolewa

Waziri Ummy Mwalimu: Maduka ya Dawa nje ya hospitali yaliyo ndani ya mita 500 kuondolewa

Maduka yote ya dawa nje ya hospitali yanatakiwa kuwa umbali wa mita 500, sheria hii niliipitisha kabla sijaondoka Wizarani, maduka yaliyo ndani ya Mita 500 ndani ya Hospitali Nchi nzima tunakwenda kuyaondoa, Hospitali dawa hakuna, kwanini maduka ya nje dawa zipo? Haikubaliki"

Pia soma

Ni wivu tu wa maduka binafsi..huyu waziri kakosa ubunifu naona ni moja ya waziri vilaza..hivi ukisogeza hata 1km ndio madawa yatapatikana hospitali..au hayo maduka private yatakosa madawa.

Boresheni na toeni pesa..na simamieni vzr msd..kama imeshindwa kazi kama hamna pesa..semeni tu sio kuleta siasa uchwara..kwenye huduma za dawa kwa wagonjwa.

Waziri bure huyu.

Nchi hii kuja kuendelea kwa vilaza kama hawa tusahau.

#MaendeleoHayanaChama
 
Maduka yote ya dawa nje ya hospitali yanatakiwa kuwa umbali wa mita 500, sheria hii niliipitisha kabla sijaondoka Wizarani, maduka yaliyo ndani ya Mita 500 ndani ya Hospitali Nchi nzima tunakwenda kuyaondoa, Hospitali dawa hakuna, kwanini maduka ya nje dawa zipo? Haikubaliki"

Pia soma

Hii kauli ya ovyo kabisa nimewahi kuisikia nchi yenyewe maskini kule hospitali dawa hawana bima zenyewe mpaka mtu awe kaajiriwa, pale temeke operation mdogo laki 5, muhimbili kule ndio kabisa leo uzuie maduka ya dawa mita 500 kutoka hospitali kwa lipi kubwa.,

Ni vile kiongozi akiwa kwenye madaraka anaona hali yake anavyoishi na familia yake ndivyo watu wengine wanaishi., Kama mumeboresha mahospitali kiasi basi hao wenye maduka wataondoa maduka yao automatically watakosa wateja mana hospitali kuna kila kitu
 
Hospital za binafsi zinapeta tu hata duka la dawa liwe mita 0.

Siku hizi kwenye hospital za umma,dawa unaletewa kwenye chumba cha daktari na unalipia humohumo,hauendi tena dirisha la dawa.
 
Leo, Waziri Ummy Mwalimu amesema Maduka yote ya dawa nje ya hospitali yanatakiwa kuwa umbali wa mita 500. Amesema Sheria hii aliipitisha yeye kabla sijaondoka Wizarani na kuongeza kuwa Maduka yaliyo ndani ya Mita 500 ndani ya Hospitali Nchi nzima wanakwenda kuyaondo.

Waziri Ummy amehoji: "Hospitali dawa hakuna, kwanini maduka ya nje dawa zipo? Haikubaliki"

Pia soma

Kila anayeingia anaingia na yake
 
Naona mnagawana mbao😊😊😊😊😊😊.
Tuseme tu uwezo wa chama kuendelea kuongoza Nchi unatia Mashaka!
Nakuona Pro umeanza kuhama taratibu taratibu, awamu iliyopita ulikuwa huambiwi kitu! 😜
 
Kwahiyo yakiwa nje umbali wa mita 500 ndio dawa zitakosekana kwenye hayo maduka? Au mimi kuna kitu sijaelewa?
Ahahahaha yakiwa ndani ya mita 500 inaonekana maduka binafsi yanatumia magnetic-field kuhamisha madawa toka msd ya hospitali za serikali hivyo wagonjwa hukosa dawa, ngoja tuone yakiwa zaidi ya hizo mita labda dawa zitakwepo watu hatutaambiwa hakuna dawa kanunue
 
Kufanya biashara TANZANIA inahitaji moyo

Sent using Jamii Forums mobile app
Tena uwe na moyo wa chuma haswa, Mimi huwa nawavulia kofia watu waliofanikiwa kibiashara bongo hii na najifunza vingi kutoka kwao.

Serikali na taasisizake na mamlaka zake zote zipo kwa ajili ya makatazo, mazuio, ukamataji, ukusanyaji, ufungiaji, bila kujali mfanyabiashara huyu anabaki na nini na anasaidiwa na nani ikiwa kila mtu yupo kwa ajili ya uharibifu.
 
Ni hatari Sana mkuu

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mi nafikiri wange focus kwenye kwanini dawa hakuna hospitali. Then wakisha jua tatizo liliko walitatue kama ni wizi basi wahusika wawajibishwe. Kama kweli ni uhaba wa madawa serikali iweke bajeti dawa zipatikane.

Sioni mantiki ya kuyaondoa maduka. Kuna wakati dawa zinakua hamna kutokana na uzembe wao wenyewe basi uo mda hayo maduka hugeuka mkombozi iweje yatolewe?
Ina maana mpaka sasa hawajui
 
Sheria mbovu iliyotungwa ina malengo ya kutuadhibu tusiokuwa nacho. Wenye nacho watafaidika mara mia. Ukikosa dawa utapanda bajaj au bodaboda kwenda kuifuata. Huenda maduka hayo ni ya wale wasioyatumia maduka hayo zaidi ya kutuuzia siye. Maduka yakiwa mbali hata bei watajipangia bila kuwaonea haya wahanga. Sipendi sana kutumia neno "wanyonge" lakini kwa hili wahanga tunaweza kuitwa hivyo.
 
Back
Top Bottom