Mtu darasa la saba anashinda anagonga meza, hakai ofisini masaa yote, ati kwakuwa tu ni mhe analipwa 11Mil,
Dakitari, Mwl, Askari wanaokimbizana na uhai wa taifa wanachezewa wanalipwa posho ya mbunge ya siku moja.
Ifike wakati sasa wabunge wapunguzwe, wawe sawa kwa idadi na RCs na wafanye kazi full time, fedha inayookolewa huko ipelekwe kwa madakitari, walimu na askari
Binafsi namwona ni female Kinana, shujaa wa pili ndani ya siku zisizozidi 7, sauti za raia hazikusikilizwa na mamlaka husika zimekuwa zikiziba masikio, PCCB na wale wa usalama are sleeping wanasubiri wapelekewe form za malalamiko, mzee kutoka Tanga yuko hoi atajaza hizo fomu saa ngapi mpaka akafike pccb ameshakufa njiani masikini
Angeanza kuwashughulikia ndani kwa ndani, angegusa ndevu za simba, tazama unapotaja "JKCI" unamgusa nani
Kuna taasisi haitimizi majukumu yake, imewalinda traffic police for decades, Ummy lazima aiseme kinamna
Tamko la Ummy limeziamsha sekta nyingine pia kutambua kuwa sasa hali siyo shwari kuna sehemu ina ufa
Kitendo cha yeye kutamka hadharani, amenawa mikono akimaanisha kuna genge linalinda watu wao
Mishahara ya madakitari ni duni, ikumbukwe ni 6 years sasa watumishi wanaishi kwa viwango vya zamani na hapo gharama za maisha zimepanda sana tena mfululizo
Kiongozi shupavu na mkali akiiongoza taasisi ya urais, basi rushwa katika utumishi wa umma huwa zinapungua sana. Kinyume chake rushwa hutamalaki na kugeuka kuwa chanzo kikuu na mbadala cha mapato.