Waziri Ummy, Usipotoshwe maamuzi yako kuhusu ADDO na wafamasia mtawaumiza Watanzania

Iko hivyoo... na ndivyo inavyo takiwa iwe.Maana kila mtu ana jukumu lake na heshima Kwa Kila mtu ichukue mkondo wake.Hakuna haja ya kuona mtu ni mkubwa zaidi ya mwingine.
Mkubwa ni mgonjwa aliye waajiri wote hao!; bila wagonjwa hawana Ajira
 
Hivi wewe ni daktari kweli?

Too low from you , yaani unasema kazi mfamasia ni kusambaza dawa really? Upo hospitali gani kwanza?

Yaani mnaziona dawa ni kama pipi eh mtu anakaa wiki 6 eti ADDO atoe dawa sababu ni daktari au nesi halafu aliyesoma dawa miaka yake 4-5 awe msambazaji??

Kuna haja wafamasia wa kitanzania waamke wamelala sana hasa hapo barazani ndio maana wanasaliti wenzao walioko chini huku wao wakinufaika.

Huku kwa watu anything related to drugs is entitled to a pharmacist au 100% directly otherwise atakuwepo anafanya supervision na sio vinginevyo.

Niliona video ya ujinga wa hizo ADDO wamekariri tu rangi ya vidonge hasomi hata prescription wala kuchukua history hawezi ndio mnaona wako sawa?
 
Nilidhani ni mimi tu mimeshangaa sana eti huyu ni daktari ! ambaye hajui kazi ya mfamasia hospitali ni ipi .
 
Nilidhani ni mimi tu mimeshangaa sana eti huyu ni daktari ! ambaye hajui kazi ya mfamasia hospitali ni ipi .
Tena anajitangaza kabisa yeye ni Profesa!

Na inawezekana kabisa akawa ni profesa kweli, na hiyo inaonyesha kiasi gani nchi yetu ilivyoporomoka katika viwango.
 
Tena anajitangaza kabisa yeye ni Profesa!

Na inawezekana kabisa akawa ni profesa kweli, na hiyo inaonyesha kiasi gani nchi yetu ilivyoporomoka katika viwango.
Aibu sana huyu ngoja nimuangalie kwenye database ya mct nione kama nitamuona alisoma wapi.
 
Professor kaandika vizuri sana, wafamasia hata wa hapa JF wanahisi kusoma pharmacology basi ndo kuweza kutibu au kutoa dawa kwa mgonjwa. Mwingine anafikia hatua ya kutoa ya moyoni kwamba madaktari wanagoogle dawa, huo ni ujinga.

Prof ametoa hoja kulingana na description ya kazi ya kila mmoja ila wengine wanabisha tu sababu anasoma pharmacology muda mrefu.
 
Wewe hapo ni 'valium', lakini naona huelewi hata hiyo 'pharmacology' ya diazepam' ipoje.

Ni Famasia yupi ambaye anadai kuwa kujua 'pharmacology' ndiko kutibu"? Ni Famasia yupi ambaye analilia majukumu ambayo siyo yake katika kumhudumia mgonjwa?
Hata hujui kwamba katika kutibu si jukumu la taaluma moja tu, hili nalo hulijui mpaka uelezwe?

"Description ya kazi" ya daktari ni kutoa dawa (dispense) kwa mgonjwa, toka lini na kwa sheria gani? Description ya kazi ya daktari ni kutunza dawa katika mazingira yanayotakiwa? Toka lini na wapi?

Hapa hakuna hoja ya kusoma 'pharmacology' au nini, ni swala la majukumu yaliyo wazi kwa kila mmoja wa watu wanaomhudumia mgonjwa. Mgonjwa siyo mali ya daktari, hawezi kuhodhiwa na daktari kama mali yake na kutaka afanye kila kitu yeye pekee kwa mgonjwa huyo.
 
Hili andiko la Prof.naona limetembea hadi whatsupp ya kuna mtu kanitumia leo
 
Pharmacology nisehemu ndogo Tuu ya dawa

ili uwe equipped kwenye dawa basi lazima ujue yafuatayi

(1) Pharmaceutics
(2) Basic Pharmacology and Clinical Pharmacology
(3)Pharmaceutical/Medicinal chemistry
(4) pharmacy practice
(5) Toxicology
Note: Pharmacist anasoma pia PHARMACOGNOSY hii ni kama Pharmacology ila based on herbal medicines tena deep......


ila Daktari anasoma Basic Pharmacology (which is simple Pharmacology)...... Kwa akili ya kawaida tutakuwa WAJINGA kumlinganisha Daktari na pharmacist kwenye ishu zote zinazohusu dawa......

PHARMACIST IS THE DRUG DEALER .......FULL STOP
 
Kwa kufuata maelekezo ya elimu aliyonayo, daktari hawezi kuandika pcm 4g tds kisha mfamasia akatoa tu kama ng'ombe anatoa mbolea.
Duh.
Hivi atakuelewa kweli ulichompa hapo?

Na hii ndiyo shida ya wengi, kudhani kwamba kwa vile daktari anaandika, basi hiyo ni 'final authority', hawezi kurekebishwa na aliye na ufahamu zaidi yake juu ya mambo ya dawa.
Hili ndilo tatizo kubwa linalowasumbua vihiyo wengi katika taaluma hiyo.

Huyu anayejitangaza hapa kama MD, Profesa ni mfano halisi wa kundi hilo.
 

Hila mtupu! Daktari kazi yako ni hospitalini!! Siyo kwenye duka la dawa!! Lazima kuwepo na mgawanyo wa majukumu!! Pharmacy zote zihudumiwe na wafamaia. Ninachoweza kukuelewa ni kuwa wanunuzi wa dawa wawe na prescription za daktari kwa baadi ya magonjwa na si kila ugonjwa!! Halafu wanunuzi wa dawa leo hii wana uzoefu wa miili yao na aina ya dawa ambayo kwa kawaida huwa inawasaidia. Mode of action ya dawa na drug interaction ni eneo la mfamasia!! Daktari unataka ufanye kazi ya mfamasia wakati hujaisomea, HAPANA, baki HOSPITALI!! Muuguzi ndiye anaweza kuuza dawa chini ya uangalizi wa mfamasia kwa kutumia prescription walizopewa wagonjwa na madaktari.
Uzoefu wa nchi za ulaya ni huu: Madaktari hufungua Medical consultation offices!! Mtu akihitaji kununua dawa anaenda kwanza kwa daktari, ambaye amesheheni vifaa vya uchunguzi tu na hana dawa yoyote. Yeye atatoa prescription halafu mgonjwa ataenda pharmacy kununua dawa. Si lazima mfamasia kumtumia muuguzi maana mfamasia anaweza kusoma prescription na kutoa dawa. Akiamua kumtumia muuguzi ni sawa lakini isiwe lazima.
 
Ni aibu kuona tunafika level ya kubishana Nani auze duka la dawa. Kwamba wafamasia wanaosomea kutengeneza madawa na kusimamia mnyororo wa dawa na Quality assurance wanachukukulia kuuza duka la dawa as their primary role. Totally shameful!
After all hoja ya hapa ilikua, why a non pharmaceutical medical personnel anayehitaji kuuza DLDM alazimike kusoma ADDO ? Ni kitu gani Cha ziada anachofundisha kwenye kozi hiyo ya wiki sita ambacho hakukisoma kwenye pharmacology course aliyosoma kwa mwaka mzima?
 
Prof. Patrick Koboko MD, MMED,Phd (kama anavyojiita) awaombe radhi Wafamasia, kwa upotoshaji wa makusudi kwa mhe. Waziri wa Afya na umma wa watanzania kuhusu ADDO na taaluma ya ufamasia.

Yoshua Nguyahambi, Darasa la Saba B

Ndugu zangu nawasalimu kwa jina la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Nimeisoma kwa makini Makala ndefu ya mtu anayejiita Prof. Patrick Koboko, nashawishika kukiri wazi kwamba Profesa (Kama anavyojiita) amefanya upotoshaji wa makusudi kwa mhe. Waziri wa Afya na Umma wa watanzania kuhusu Addo na taaluma ya ufamasia.

Kwanza, katika makala yake amedai kazi ya mfamasia ni Kutunza na kuifadhi dawa, kusambaza maeneo yenye uhitaji pamoja na kutengeneza dawa viwandani na siyo kutoa dawa moja kwa moja kwa mgonjwa, ameenda mbele zaidi na kusema kazi ya mfamasia siyo drug administration eti hii ni kazi ya watu wengine, ameendelea kudai kwamba mfamasia hajasomea magonjwa wala wadudu wanaosababisha maradhi na hajasomea dalili za magonjwa, huu ni upotoshaji wa kijinga na makusudi kabisa uliofanywa na mtu wa ngazi ya uprofesa, angekuwa kwenye nchi za wenzetu angeshaitwa na kunyang'anywa uprofesa mara moja!

Hivi katika akili ya kawaida tu ya la saba B, kama yangu, mtu anaweza kukutengezea dawa kiwandani kama alivyodai anayejiita profesa, bila kujua issue za drug administration, epidemology, Anatomy, Physiology, Parasitology, Pathology, microbiology, biochemistry, Parasitology? Yaani mtu akutengenezee Paracetamol na asijue namna ya kuitoa kwa mgonjwa? Anasahau kabisa wao (wafamasia) watengenezaji wa dawa ndio wanawaandalia leflet zinazoonyesha namna dawa inavyopaswa kutumika, athari zake, n.k. Profesa wakati unaandaa makala hii ulikuwa wapi? Au ulikuwa na hangover ya K-vant?. Wakati mwingine tunapoamua kuandika makala sensitive na zinazogusa moja kwa moja Umma wa watanzania tusisukumwe na jicho la wivu, husda na kijino pembe kwa taaluma za wengine.

Profesa Patrick Koboko MD, MMED,PhD(kama anavyojiita) amenifanya mimi darasa la saba B nirudi kuangalia tena Prospectus ya vyuo vinavyotoa course za ufamasia, kuangalia je madai yake aliyoyatoa kuhusu wa wafamasia yana ukweli? Ni halali? Mathalan ukisoma prospectus ya chuo kikuu cha Muhimbili ya 2019/2020 – 2020/2021 ukurasa wa 75, kuna maneno yasomeka hivi, nanukuu "Pharmacy education embraces the search, development, formulation, analysis, storage and distribution of products for maintenance and restoration of good health as well as provision of information and guidance on proper use of medicines."

Sio kazi yangu darasa la saba B kumtafsiria maneno hayo, lakini ni wazi kuwa wafamasia ndio wanataaluma pekee wanaondaliwa sio tu kwajili ya yale aliyosema, wafamasia wanapaswa kuyafanya lakini pia kwajili ya kulea na kutoa taarifa sahihi za matumizi sahihi ya dawa, Prof. Koboko (kama anavyojiita) alipaswa alijue hili mapema hata kabla hajafikiria kuandika makala yake. Kwahiyo kama darasa la saba B nampa home work profesa Koboko (kama anavyojiita) aende aipitie tena Prospectus ya Muhimbili na vyuo vingine vinavyo offer digrii ya ufamasia, aangalie vizuri kwa kulinganisha na hizo taaluma nyingine ni wapi kwenye Prospectus hizo mfamasia haandaliwi kutoa dawa kwa mgonjwa? Litakuwa kosa kubwa la karne kama usimamizi wa dawa, vifaa tiba na vitendanishi vitaondolewa kwenye mikono ya wafamasia kwa maana ya Baraza la famasi, kwasababu ya ushauri wa ki husda na kijino pembe ulitolewa na huyo anayeitwa Profesa, kwa sababu kwa mfumo wa elimu ya Tanzania ni wafamasia pekee ndio wameandaliwa kwa jukumu hilo. Profesa kama anavyojiita alipaswa kulifahamu hili.

KUHUSU ADDO.

Arudi aangalie vizuri kwanini wizara ya afya iliamua kuanzisha mafunzo hayo, ingawa ni kweli kuna mapungufu lkn haiondoi nia njema ya Serikali kupitia wizara ya Afya iliyoamua kuanzisha mafunzo hayo, ambapo awali yalikuwa chini ya TFDA sasa hivi TMDA, na baadae uratibu wake ukahamishiwa baraza la famasi kwasababu wao ndio wadau & walezi sahihi wa mambo yote yanahusiana na dawa, vifaa tiba na vitendanishi

Upo ushahidi wa wazi kabisa wa baadhi ya maduka haya ya dawa muhimu ambayo wanataaluma wenzetu (wasio wafamasia) wameyageuza kuwa Zahanati bubu kinyume kabisa kanuni zinazoruhusu uanzishaji wa maduka ya dawa muhimu unavyotaka, na ndicho anachojaribu kushauri Profesa (kama anavyojiita) kuwa maduka haya yageuzwe kuwa zahanati bubu kwa kupewa matabibu na Manesi bila kufundishwa chochote kuhusu malengo ya uanzishwaji ya maduka haya, kama nilivyosema awali litakuwa kosa kubwa la karne kuupokea ushauri huo bila kuzingatia ukweli niliouanisha kwenye makala yangu.
 
Kila mtu akae kwenye nafasi yake na afanye kazi yake kwa usahihi..That's all.
 
Hakuna mfamasia anayesema kuwa wanaweza kutoa kila aina ya dawa kwa kila aina ya ugonjwa bila prescription ya daktari. Ila ukweli ni kwamba anayejua madhara ya dawa zaidi ni mfamasia wala si daktari. Tatizo lililopo ni daktari kutaka kufanya kazi kwenye pharmarcy kwa kujitawala bila uangalizi wa mfamasia!! Daktari baki hospitalini, mfamasia baki kwenye pharmacy!! Daktari una hila za kula ugali wa kidaktari na ule ugali wa kifamasia, HAPANA!! Daktari analalamika mfamasia kugawa dawa kwenye duka la madawa, hivi ni nani anaweza kusema kuwa mfamasia hawezi kusoma prescription ya daktari? Kwani huko hospitalini si kuna pharmacy pia? Ni nani huwa anasimamia na kutoa dawa kwenye chumba cha kutolea dawa cha hospitalini??
 
Nataka ifahamike kuwa muuguzi na daktari kuruhusiwa kuuza dawa kwenye duka la dawa muhimu ni kwa sababu ya upungufu wa wafamasia! Ningeshauri wasiruhusiwe, na huduma hii ibaki kwa wafamasia ngazi ya cheti na stashahada!

Bodi ya famasi imewapiga teke sana wataalamu wa dawa ngazi ya cheti na stashahada!! Kila fani ile kutokana na urefu wa kamba yao!! Madaktari na wauguzi wabaki hospitalini na wataalamu wa madawa ngazi ya cheti, stashahada na shahada wabaki wakishughulika na maduka ya dawa katika ngazi mbali mbali!
 
Hakuna daktari mwenye jina kama hilo.. hapa TZ Kwa mujibu wa MCT website
 
Hakuna daktari mwenye jina kama hilo.. hapa TZ Kwa mujibu wa MCT website
Nimejaribu kusearch halijaja jina hilo ila kwa kifupi kama huyu ni professor kweli basi elimu ya Tanzania iko hoi taabani na sishangai kwa maprofesa wakipewa vyeo kusema wametolewa jalalani.

Na hapo anasema mfamasia kazi yake kusambaza dawa hivi huyu anajua kuna watu wanaitwa PharmD ?

Anajua scope ya hao wstu iko vipi?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…